Car Service Episode 2/10: Coolant na brake fluid zinatakiwa kubadilishwa kila baada ya miaka miwili au km 40,000!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
31,139
Reaction score
88,799
Wakuu, kwema?

Wengi tunabadirisha engine oil kila mara, lakini tunasahau fluids zingine muhimu sana, mfano coolants na brake fluids.
IMG_8657.jpeg

Leo kwenye muendelezo wetu wa service, tuzungumzie coolant na brake fluid ambazo zikipuuzwa zinaweza kuharibu engine au system ya breki au zikakupa majanga makubwa.

Coolant na Kazi zake:
IMG_8656.jpeg

Hii ni fluid inayowekwa kwenye gari kwa madhumuni ya kupooza engine (na components zake), kuzuia kutu kwenye radiator na block.
IMG_8651.png

Interval:
Badilisha kila baada ya miaka 2 au km 40,000–60,000 kutegemea na mazingira.
IMG_8648.jpeg

Unavyobadirosha usichanganye rangi tofauti, mfano nyekundu na green. Kwahiyo ni vema kujua gari lako linatumia coolant ya rangi gani.

Kutegemea na gari lako, magari mengi yanapokea lita 4-6 ila pia yapo makubwa kama Harrier au Prado yanameza lita 7-9.
IMG_8650.jpeg

Ukienda kununua lazima ujue unapewa concentrate coolant (ambayo utachanganya na distilled water 50/50) au ready to use coolant ambayo wameshachanganya wewe unamimina tu.

Bei zake mara nyingi ni 20,000 hadi 35,000 kwa lita na vitup vingi vya mafuta utazipata.

Ukienda garage hakikisha wamefanya flush (kusafisha system kabla ya kujaza mpya), na pia hakikisha air bubbles zimeisha baada ya kujaza na please usimix colors.

Brake Fluid na Kazi yake:
IMG_8654.jpeg

Hii fluid inawekwa kwenye system ya breki kwa malengo ya kupeleka pressure kutoka kwa pedal hadi brakes pindi unapokanyaha. Mara nyingi unyevu (humidity) inapelekea ipoteze uwezo wake wa kufanya kazi na kuathiri perfomance ya breki.

Interval:
IMG_8653.jpeg

Unashauriwa kubadirisha kila baada ya miaka 2 au km 40,000. Kutegemea na maelezo ya gari yako, utatumia DOT 3 au DOT 4 tu, usichanganye.
IMG_8652.jpeg

Magari mengi yanapokea lita 1 kushuka chini, na bei zake haizidi elfu 20 kwa lita moja.
IMG_8655.jpeg

Hii ukienda garage hakikisha amefanya bleeding asifanye topup na ikibaki usirudi nayo home kama una watoto.

Me naona niishie hapa. Kama kuna mtu ana cha kuongeza karibu.
 
Mfano oil ina isha haraka ni kama ina vuja lakini ukiagalia hakuna sehemu inayo vujisha shida nini?
 
Kama nimesahau rangi ya coolant niliyoweka mara ya mwisho inakuwaje hapo!
 
Mfano oil ina isha haraka ni kama ina vuja lakini ukiagalia hakuna sehemu inayo vujisha shida nini?
Kuna magari tunasemaga yanachoma oil. Mfano, BMW 320i zinatabia iyo kinoma, especially gasket ikizingua. Tunachofanya uwa tunajazia.
 
Nina mpango huo wa kubadilisha coolant mwezi December, nimefanya Kwanza utafiti wa coolant Sahihi Kwa gari yangu ila naona bado wauzaji wengi hawana ujuzi wa kutosha juu ya biashara zao.

Ukienda Kwa mafundi wengi ndiyo kabisaa hakuna wanachojua yaani kwakifupi bado tunahitaji elimu zaidi juu ya vyombo vya moto
 
Wakuu, kwema?

Wengi tunabadirisha engine oil kila mara, lakini tunasahau fluids zingine muhimu sana, mfano coolants na brake fluids.
View attachment 3484893
Leo kwenye muendelezo wetu wa service, tuzungumzie coolant na brake fluid ambazo zikipuuzwa zinaweza kuharibu engine au system ya breki au zikakupa majanga makubwa.

Coolant na Kazi zake:
View attachment 3484884
Hii ni fluid inayowekwa kwenye gari kwa madhumuni ya kupooza engine (na components zake), kuzuia kutu kwenye radiator na block.
View attachment 3484885

Interval:
Badilisha kila baada ya miaka 2 au km 40,000–60,000 kutegemea na mazingira.
View attachment 3484886
Unavyobadirosha usichanganye rangi tofauti, mfano nyekundu na green. Kwahiyo ni vema kujua gari lako linatumia coolant ya rangi gani.

Kutegemea na gari lako, magari mengi yanapokea lita 4-6 ila pia yapo makubwa kama Harrier au Prado yanameza lita 7-9.
View attachment 3484887
Ukienda kununua lazima ujue unapewa concentrate coolant (ambayo utachanganya na distilled water 50/50) au ready to use coolant ambayo wameshachanganya wewe unamimina tu.

Bei zake mara nyingi ni 20,000 hadi 35,000 kwa lita na vitup vingi vya mafuta utazipata.

Ukienda garage hakikisha wamefanya flush (kusafisha system kabla ya kujaza mpya), na pia hakikisha air bubbles zimeisha baada ya kujaza na please usimix colors.

Brake Fluid na Kazi yake:
View attachment 3484888
Hii fluid inawekwa kwenye system ya breki kwa malengo ya kupeleka pressure kutoka kwa pedal hadi brakes pindi unapokanyaha. Mara nyingi unyevu (humidity) inapelekea ipoteze uwezo wake wa kufanya kazi na kuathiri perfomance ya breki.

Interval:
View attachment 3484890
Unashauriwa kubadirisha kila baada ya miaka 2 au km 40,000. Kutegemea na maelezo ya gari yako, utatumia DOT 3 au DOT 4 tu, usichanganye.
View attachment 3484891
Magari mengi yanapokea lita 1 kushuka chini, na bei zake haizidi elfu 20 kwa lita moja.
View attachment 3484892
Hii ukienda garage hakikisha amefanya bleeding asifanye topup na ikibaki usirudi nayo home kama una watoto.

Me naona niishie hapa. Kama kuna mtu ana cha kuongeza karibu.
Ahsante kwa somo nzuri mkuu, nina Harrier tako la nyani nimeanza kuitumia toka mwezi wa pili, lakini kuanzia mwezi uliopita nikiangalia kwenye rejeta upande wa kulia juu kushuka chini kama kuna nyufa ndogo ambayo gari ikiwa inatembea nadhani ile coolant inavyozunguka inavuja pale kwa mbali, hali inayopelekea coolant kupungua, unaweza niambia chanzo kinaweza kuwa ni nini? Solution yake inaweza kuwa nini?, ahsante tena kwa elimu nzuri
 
Pole mkuu. Ngumu kujua bila kuona picha, ila inamaanisha kuna leakage kwenye rejeta.
Ungepata garage wafanye pressure test tungejua wapi inavuja na kama leakage ndogo tunaweza kutumia radiator sealant.
Chanzo inaweza kua zile plastic parts zimechakaa, au pressure, au kugongwa au coolant chafu kuziba.
Ebu tujaribu kwanza kwa fundi tuone uzito wa tatizo uzuri radiator sio kitu cha kufa mara moja inaanza taratibu kuvuja hadi utakavyoona inakua too much ndio unaweza nunua mpya au reconditioned.
 
Nina mpango huo wa kubadilisha coolant mwezi December, nimefanya Kwanza utafiti wa coolant Sahihi Kwa gari yangu ila naona bado wauzaji wengi hawana ujuzi wa kutosha juu ya biashara zao.

Ukienda Kwa mafundi wengi ndiyo kabisaa hakuna wanachojua yaani kwakifupi bado tunahitaji elimu zaidi juu ya vyombo vya moto
Hivi ni model gani? Nikumbushe
 
Mimi mpaka Leo sijajua bado coolant gani ni Sahihi kwenye Subaru forester XT 2009 engine code SH 5
Wenyewe OEM wanataka Subaru Supercoolant, rangi ya blue. Tatizo kuipata maana ndio inayowekwa kwenye gari na Subaru wanasa inakaa hadi miaka 11 au km 200,000.
IMG_8681.jpeg

Ukikosa wanasema tumia nyingine za blue zenye formula sawa (phosphate organic acid technology (P-OAT)) na hazina silicate, ila usitumie ya KIJANI coz ina silicane na inaharibu gaskets.

Pambana na page 400 za usermanual hizi hapa 😂😂
 
Attachments

Back
Top Bottom