Car Service Episode 1/10: Engine na Gearbox Oil!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
31,139
Reaction score
88,800
Wakuu. Poleni na kila kitu.

Nimeona leo tuwe na open discussion ya engine na gearbox oil service. Kama kuna mtu ana ujuzi na uzoefu wa aina aliyitumia na mabadiriko aliyoyaona inaweza kua msaada kwa mwingine.

Kwa kuanza, mi nitatoa flashback kidogo na experience yangu ndogo kwenye hivyo vitu.

ENGINE OIL
Hii nadhani ndio kila mtu akisikia neno service ya gari, kitu cha kwanza kinachomjia.
Engine oil inawekwa kwenye engine ikiwa na malengo ya moving parts za engine, kupunguza msuguano na joto, kusafisha engine, na kulinda engine isipate kutu.

Interval ya kubadilisha:
Kutegemea na aina ya oil ukiyoweka, tunategemea utabadirisha kila baada ya miezi 6 au kilometa elfu 5 hadi elfu 10. Ila kwa mazingira ya joto mfano Dar, tunashauriwa ata kubadirisha kilometa kidogo nyuma ya uliyokua recommended. Mfano wamesema elfu 5, basi ukipendezwa elfu 4.5 sio mbaya.

Aina za engine oil:
Kuna aina mbalimbali za engine oil. Na itategemea gari lako linataka aina ipi, ila kwa kifupi makundi makuu ni matatu:
1. Mineral oil: Hii ni oil ya kawaida, bei rahisi, inafaa kwa magari ya zamani (mfano: Castrol GTX 20W-50, Total Classic 20W-50)

2. Semi-synthetic: Hii ina mchanganyiko, performance bora kidogo (mfano: Shell HX7 10W-40, Total Quartz 7000 10W-40)

3. Fully Synthetic: Hii ni kiwango cha juu zaidi, engine inakuwa smooth, change interval ndefu (mfano: Castrol EDGE 5W-30, Mobil 1 0W-20, Liqui Moly TopTec 4200 5W-30, Toyota Genuine 0W-20)

Ukiangalia engine oil unakuta kuna namba kama 5W-30 au 10W-40. Hizo zisikutese, maana zinaeleza jinsi oil itakavyo-behave kwenye baridi au joto.

Tukieleza kwa urahisi, hiyo namba ya meanzo na “W” (mfano 5W) inaonyesha jinsi oil itakavyoflow injini ikiwa baridi (mfano asubuhi). Kwahiyo namba ndogo (kama 0 au 5) inamaanisha itaanza kuflow haraka zaidi. Ile namba ya pili (mfano 30 au 40) inaonyesha jinsi oil itskavyoendelea kua nzito joto likikolea. Namba kubwa inamaanisha itaendelea kua nzito na kufanya kazi yake vizuri. Kwa hali ya Tanzania yenye joto, oil kama 10W-40 au 5W-30 ni option zuri kwa magari mengi.

Viscosity zinazofaa kwa Tanzania:
0W-20 : Hii kwa magari mapya/hybrids (Honda Fit GP5, Toyota Aqua) kwasababu engine ina jizima na kuwaka mara kwa mara inahitaji oil nyepesi sana.

5W-30 : Hii range ndio maarufu zaidi. Hapamagari ya kisasa yanatumia. (Swift K12B, Corolla, Axio, Demio, 3 series etc).

10W-40 : Hii naiona kwenye magari ya zamani au yenye mileage kubwa. Ila utashauriana zaidi na fundi.

Bei ya wastani (kwa lita):
Mineral: Tsh 12,000–15,000
Semi Synthetic: Tsh 18,000–25,000
Fully Synthetic: Tsh 25,000–40,000

Magari mengi yanachukua lita 3.5–5 nashauri sana upitie manual ya gari lako.

Pia kuna wimbi la oil feki sana. Nashauri usimuachie fundi afanye kila kitu, nenda kununua mwenyewe kwenye maduka makubwa au vituo vya mafuta (Total, Puma, nk).
Pia kila ukibadirisha oil, badiri na oil filter. Hii inauzwa elfu 15 hadi 30 mara nyingi.
Na mwisho, kagua level ya oil kwa dipstick au kama unasoma kwenye car computer kabla haujaondoka.

GEARBOX OIL / TRANSMISSION FLUID
Hii ni oil inayowekwa kwenye gearbox kwa malengo ya kulainisha na kupunguza msuguano ndani ya gearbox, Kupooza system ya gear, na kwa Automaticau CVT inasaidia kubadilisha gear smoothly.
Interval ya kubadilisha:
Manual: kila 40,000–60,000 km
Automatic/CVT: kila 35,000–40,000 km au miaka 2

Maeneo yenye joto, kama tulivyosema kwenye engine oil, ukibadirisha mapema ni vema zaidi.

Aina za oil kulingana na gearbox:
Hapa kwenye aina hauna ujanja ujanja. Ni lazima utafute specifications ambazo mtengeneza gearbox ameshsuri.
Mfano, kwa Manual Gearbox:

  • 75W-90 GL-4 / GL-5 (mfano: Castrol Axle EPX 80W-90, Shell Spirax S4 75W-90, Total Transmission Gear 8 75W-90)
Wakati Automatic (ATF) gearbox, mifano:
  • Dexron III, Mercon V (mfano: Castrol Transmax Dex III, Shell Matic J, Total Fluide ATX)
CVT Gearbox:
Hizi ziko sensitive zaidi. Ni lazima uweke special CVT fluid tu, mfano: Suzuki CVT Green 2, Honda HCF-2, Toyota CVT-TC / CVT-FE, Idemitsu CVTF.

Bei ya wastani (kwa lita):
Manual: Tsh 20,000–30,000
Automatic/CVT: Tsh 35,000–60,000
(Gearbox nyingi CVT zinachukua lita 4–6)

Kama engine oil, gearbox oil pia ina feki nyingi tu. Nashauri ukanunue mwenyewe na sio umuachie fundi kwenye maduka makubwa.
Kwa watumiaji wa Toyota, uzuri Kariakoo kuna Toyota shop nzuri na wanauza genuine products tu, pale mtaa wa Msimbazi. Magari mengine pia kuna dealers na distributors wadogo wadogo.
Pia ukienda garage fundi afanye drain & refill, si kuongeza tu juu.

Pia angalia rangi ya oil inatakiwa iwe clear red/green, si brown au black.

Pia fundi asafishe magnet ya drain plug.

Na mwisho, usichanganye ATF na CVT fluids.

Kwa yoyote mwenye kitu cha kuongeza, marekebisho au ushauri au maswali kuhusiana na engine oil na gearbox oil za magari, karibu sana.

Kuhusu engine oil za magari, pia kuna uzi hapa mzuri sana:
Zifahamu Engine oil
 
Brother.
Kuna siku nilienda kununua oil ya engine kituo cha mafuta cha Total kwanza nilikuta bei nzuri kuliko hata mtaani walivyokuwa wananiuzia.
 
Uzuri mzuri, ukifungua bonet ya gari za toyota “cvt” kuna maneno ya KiJapan yameandikwa kwa translation ni “unless driven under unnormrmal conditions, do not change gearbox oil” hii inamaana gani?
 
Uzuri mzuri, ukifungua bonet ya gari za toyota “cvt” kuna maneno ya KiJapan yameandikwa kwa translation ni “unless driven under unnormrmal conditions, do not change gearbox oil” hii inamaana gani?
"Kama huendeshi katika mazingira yasiyo ya kawaida usibadili oil ya ya gearbox"
Labda anamaanisha usibadili type ya gear box oil tofauti na iliyokuwa recommended

Ngoja wajuzi waje
 
Brother.
Kuna siku nilienda kununua oil ya engine kituo cha mafuta cha Total kwanza nilikuta bei nzuri kuliko hata mtaani walivyokuwa wananiuzia.
Kama unaweza, tumia Total zinazofanya service mfano ile ya Shekilango. Wako poa sana na bei rafiki sana. Gharama za ufundi ni bure kwasababu umenunua oil kwao.
 
Uzuri mzuri, ukifungua bonet ya gari za toyota “cvt” kuna maneno ya KiJapan yameandikwa kwa translation ni “unless driven under unnormrmal conditions, do not change gearbox oil” hii inamaana gani?
Ni kweli ata gearbox za kawaida wameandika ivyo.
Lakini hayo maneno tu. Wanashauri ubadirishe after umbali flani.
 
Reactions: Cyb
Oil services ni bora kwenda kwa service centers zenye reputation nzuri mfano total. Mtaani kuna oil fake nyingi sana, kuna vijana wanapita njiani kununua vidumu na oil chafu, wanaenda kuzifanyeje..sisi hatujui, ila oil fake ni nyingi sana!!!!
 
Kwa kuongezea nyama hasa Kwa wale watumiaji wa Castrol oil kwenye magari Yao ya petrol watumie
CASTROL OIL 5W-30 FULLY SYNTHETIC ( Castrol oil wanazo type mbalimbali za 5W-30 FULLY SYNTHETIC Kwa magari ya diesel , magari ya gesi na engine za D-4 ..oil hii inaitwa MAGNATEC)

pia Kwa kampuni ya LIQUI MOLY Wana oil zao Kwa magari ya petrol na diesel Kwa mfano watumiaji wa magari ya petrol watatumia LIQUI MOLY 5W-30 FULLY SYNTHETIC MOLYGEN na watumiaji wa diesel wanatumia liqui moly 5W-30 FULLY SYNTHETIC SPECIAL TEC ingawa hapa kwenye diesel kuna Aina nyingine ya oil ya inaitwa TOP TEC hi ni oil ambayo inategemea na umri wa gari husika.

 
Asante kwa ushauri mkuu. Vipi Prius 3rd Gen unashauri engine oil brand gani?
 
Asante kwa ushauri mkuu. Vipi Prius 3rd Gen unashauri engine oil brand gani?
Brand sio issue sana kutegemea na budget yako. Ila lazima iwr full synthetic 0W20.
Sasa unaweza enda na cheap option kama Atrantic ila unaweza kwenda Premium kama Castrol au L.Molly, budget yako tu.
Ila lazima iwe 0W20 oil nyepesi kwasababu Prius ina EV mode Kwahiyo safari ya let say 10 km unaweza kuta imewaka nakuzima zaidi ya 7 times sasa lazima oil iwe nyepesi ili ikiwakaka engine oil rahisi kuzunguka.
 
Shukrani sana. Huu ujumbe umfikie mtumia diesel Brian blvk
 
Msaada changamoto.Gati yangu ni Suzuki Swift CVT nimebadili vearbox.Seal ya shaft ya mbele ina leakage.Nimebadili karibu mara tatu bado inaleak.Je chanzo ni nini.
Ila seal ya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…