Canada yawa nchi ya pili duniani kuhalalisha matumizi ya bangi hadharani

Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
7,237
9,871
Kuna wakati nilimwambia rafiki yangu kuhusu hizi "TV show" za askari wakifyeka mashamba ya bangi iliyostawi vizuri kuwa zitakuja kuwa "majuto ni mjukuu" Leo jumatano wananchi wa Canada watanunua na kuvuta bangi kwa ajili ya "burudani" kabla ya hapo bangi ilikuwa inatumiwa kama tiba kwa walioandikiwa na daktari. Canada ni nchi ya pili baada ya Uruguay kuruhusu kumiliki na kuvuta bangi.

Dunia ni kijiji sasa ipo siku wataalam wetu watakuja kugundua kuwa bangi sio "haramu" kama walivyoambiwa na hao ambao leo wameamua kutumia.

Nimewahi kuhudumia wodi ya wagonjwa wa akili kwa miaka 2, sikumuona mgonjwa aliyekuwa na tatizo la ugonjwa wa akili kwasababu ya utumiaji bangi peke yake.

Watanzania tunahitaji mjadala wa kitaifa pamoja na tafiti huru kuhusu matumizi ya huu mmea!


======

CANADA YAWA NCHI YA PILI DUNIANI KUHALALISHA MATUMIZI YA BANGI HADHARANI

Maseneta 52 wa Baraza la Seneti wamepigia kura ya ndio muswada wa kuruhusu rasmi matumizi ya bangi hadharani kisheria huku 29 wakipinga

Katika taifa jirani la Marekani, majimbo 9 na wilaya ya Columbia yanaruhusu matumizi ya bangi kwa ajili ya starehe na majimbo 30 yanaruhusu bangi kwa ajili ya tiba

Kumiliki bangi ilikuwa ni kosa kisheria nchini humo tangu mwaka 1923 lakini matumizi ya kama dawa yaliruhusiwa kisheria tangu mwaka 2001

Sheria hiyo imeeleza kuwa Watu wenye miaka kuanzia 18 wataruhusiwa kubeba bangi hadi gramu 30, huku pia wakiruhusiwa kulima hadi mimea minne nyumbani kwao

Uruguay ilikuwa nchi ya kwanza kuruhusu uzalishaji, uuzaji na uvutaji bangi Desemba 2013
 
Kuna mgombea alishajinadi akishinda atahalalisha bangi na gongo sijui bado ana mpango wa kugombea?
 
hicho ni kielelezo cha ustaarabu na uugwana wa wa canada!! ni huku kwenye nchi masikini na mbumbumbu ndio tunakabana makoo, kila kitu kizuri ni dhambi au haramu!
 
Back
Top Bottom