Cameroon yashindwa kuqualify CAN 2012 licha ya ushindi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Cameroon yashindwa kuqualify CAN 2012 licha ya ushindi

Discussion in 'Sports' started by Sinkala, Oct 7, 2011.

 1. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Cameroon imeichapa DRC mabao 3-2 ugenini mjini Kinshasa, lakini haitaenda CAN 2012 kutokana na kuwa ya pili bila hata ya kujali matokeo ya pair nyingine ya mechi kati ya Mauritius na Senegal. Cameroon imemaliza mechi sita kwa kupata pointi 11 huku Senegal ina pointi 13 hata kabla haijaivaa Mauritius. Mechi hizi hazikuchezwa pamoja kwa kuwa hakukuwepo uwezekano wa kupanga matokeo.

  Cameroon inasubiri miujiza kuingia katika kapu la washindi wa pili walio na matokeo bora (best run-up) lakini ni kama vile haupo uwezekano, kwani katika timu tatu za best run-up, tayari mmoja (Sudan) ameshaondoa matumaini hayo kwa kuwa wa pili kwa pointi 13. Timu nyingine zilizo za pili na mchezo mmoja mkononi kwenye makundi yao lakini zina pointi 11 sawa na Cameroon ni Libya na Tunisia, huku Nigeria na Angola zikishinda kwenye makundi yao zitafikisha point 12
   
 2. m

  mwacheni77 JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 764
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  This is football,wajipange upya
   
 3. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,128
  Likes Received: 3,317
  Trophy Points: 280
  Vizuri sana, it means Alex Song atabaki arsenal.
   
 4. u

  utantambua JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mwaka wa shetani kwa vigogo. Egypt nae si hayumo CAN 2012? Saaaafi
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Haha tanzania tutakwalifai na kuchukua hili kombe 2012 .usicheze na sisi kabisa
   
 6. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  nadhani ni impact ya yale machafuko, maana mwarabu yule mziki wake si kitoto!
   
 7. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Taifa starz vp wamo??
   
 8. PingPong

  PingPong JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2011
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 933
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  taifa stars hukumu yao ni jumapili, wanacheza ugenini na morocco, uwezekano wa kupenya ni mdogo sana.
   
 9. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #9
  Oct 8, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  staz wana matumaini bado?
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  staz ni crap
   
 11. u

  utantambua JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kweli inawezekana yale mambo yaliwatoa kwenye concentration kabisa.

  Vipi south africa kakwalifai wadau?
   
 12. M

  Mwera JF-Expert Member

  #12
  Oct 8, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kenya nao wamewabania uganda ambao ndio walikua na muelekeo wa kuwakilisha east africa huko CAN 2012 lakini wamewabania wametoka sare ya 0-0,na angola ameshnda 2-0,kwa matokeo hayo uganda amekosa nafasi,alitakiwa ashinde na amekosa magoli mengi sana waganda,sasa east africa tutaendelea kuwa waangaliaji na washangiliaji wa mataifa mengine.
   
 13. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  what CAN will this be???
   
 14. u

  utantambua JF-Expert Member

  #14
  Oct 8, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sad news
   
 15. M

  Mwera JF-Expert Member

  #15
  Oct 8, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  KTK vigogo wa africa ambao hawakupata nafasi ya kushiri CAN hapo mwakani ni MISRI,CAMEROUN,NIGERIA,CONGO DRC,NA HATA SOUTH AFRICA ANA NAFASI FINYU SANA YAKWENDA,ILA KILichonisikitisha ni kenya kuwabania vilivyo uganda wakati kenya walikua hawana nafasi yoyote,ila uganda alihitaji goli 1 na point3 awe amefuzu,sasa amefuzu angola,east africa tunaendlea kuwa watazamaji bila mwakilishiwetu hata 1.
   
 16. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #16
  Oct 8, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Tanzania tungeachana na mechi za kimataifa kwa muda kidogo tujipange na team za watoto under 17 na 20 baada 8yrs tuanze upya...
  Kwa sasa tunapoteza pesa bure hao wazee wanacheza kkuangalia tv tu sio kufundishwa na makocha....hawafundishiki wakiwa wameshakomaa
   
Loading...