Mkuu Mwanakijiji,
Hapa nakubaliana nawe, kama tuna mwanya wa kutaifisha hizo machine tufanye hivyo tena haraka sana.
Hakuna sababu ya huu mjadala wa hizi machine kuwa sinema ya miezi na miezi, tufike mahali tuchukue uamuzi na kumalizana nao.
Nadhani... itatuma ujumbe mzuri tu kwa wawekezaji.. don't mess with us no more. Wawekezaji kama wanafuata taratibu na wanafanya mambo yao kisheria hawana cha kuogopa.
Mwanakijiji hapa umenena. hakuna mtu anayeizungumzia kampuni watu wanaongelea majenereta tuu. Wakiongelea kampuni inaonekana ni kampuni ya kitapeli kwa hiyo inabidi waongelee mitambo tuu. Na Mhe Zitto alinisikitisha alipokuwa anasema kwamba hajali kuhusu mmiliki au kampuni yaani alikuwa anaonekana katumwa kabisaa. Na kwa nini hizo sheria zisitumike kwenye Dowans, maana serikali ina mkono mrefu ukiidanganya inaweza kuchukua hicho ulichowadanganya nacho ila naona kwa dowans serikali mkono umekatwa.Kwanini mnaiogopa Dowans? Hamtaki kuizungumzia kampuni mmebakia kuzungumzia majenereta; hamtaki kuzungumza nwa GE, Siemens, Kawasaki n.k watengenezaji ambao wamewaambia tayari yapo majenereta ambayo yanaweza kuletwa nchini ndani ya mwaka huu na kuanza kazi tena kwa bei ya ushindani, mbona hamtangazi tenda.. mnataka Dowans Dowans Dowans
Hili mmlianzisha wenyewe, next time msilete marafiki zenu kwenye biashara mkiahidi kuwapa utajiri ambao na wenyewe watauzungusha kwenu!
NO DOWANS, FIND OTHER ALTERNATIVES.. HAMUWEZI KUJIZUIA.. THEN CONFISCATE THEM SHERIA IKO UPANDE WENU!
Hapa sasa Mtanzania unaniacha gizani kabisa. Kwingineko kote umesema kununua mitambo hiyo ni jambo jema kabisa. Hapa tena unaunga mkono kutaifisha huoni kuwa hii hijakawa sawa hata kidogo. Kwa nini tutaifishe wakati ulishasema tutununue au lile fungu lililotengwa kwa ajili ya ununuzi huo limepotea?
Sawa tunahitajia mitambo ya Dowans;
DON'T BUY THEM, SEIZE THEM KWANI WAMEWADANGANYA! Kwanini mnatetemeka kwenye option hii. Vinginevyo si huwa tunaomba misaada ya kigeni, mwombeni Al-Adawi aitoe kama hisani kwa Tanzania. Vinginevyo waombeni wajomba zetu wanunue msitumie fedha za Watanzania.
Yote yanayoendelea hapa ni kutaka tununue tu? Why why why? Kwanini tuyanunue;wakati tunajua dowans haipo kisheria? Kwanini mmeng'ang'ani tuyanunue tu wakati kuna options za kuyataifisha baada ya kujua kuwa waliingia kwa uongo soma PPRA na sheria za kuhujumu uchumi..
why are you scared Mr. President; why are you tetemekaling Mr. Ngeleja. YOU WANT DOWANS' TURBINES? GO GET 'EM!
Mtamaliza huu mjadala. Lakini.. ooh no! we have TO BUY THEM!
Najua rafiki yenu naye kawakomalia, mlimuahidi mtanunua sasa imekuwa ngondo mwaanza kufunga milango. Kwanini msiamue kununua kutoka katika fedha zenu mifukoni mwenu kuonesha huo uzalendo wenu?
Kwanini mnaiogopa Dowans? Hamtaki kuizungumzia kampuni mmebakia kuzungumzia majenereta; hamtaki kuzungumza nwa GE, Siemens, Kawasaki n.k watengenezaji ambao wamewaambia tayari yapo majenereta ambayo yanaweza kuletwa nchini ndani ya mwaka huu na kuanza kazi tena kwa bei ya ushindani, mbona hamtangazi tenda.. mnataka Dowans Dowans Dowans
Hili mmlianzisha wenyewe, next time msilete marafiki zenu kwenye biashara mkiahidi kuwapa utajiri ambao na wenyewe watauzungusha kwenu!
NO DOWANS, FIND OTHER ALTERNATIVES.. HAMUWEZI KUJIZUIA.. THEN CONFISCATE THEM SHERIA IKO UPANDE WENU!
Kule tulikotoka ndio huko huko tunakokwenda!!
Kule tulikotoka ndio huko huko tunakokwenda!!