CALL FOR SUPPORT: To Build or not To Build - The Serengeti Highway saga

PART1
[video][/video]
HOTUBA YA KIKWETE MWISHO WA MWEZI JULAI 31, 2010 Videos, Watch Free HOTUBA YA KIKWETE MWISHO WA MWEZI JULAI 31, 2010 Videos Online : IN.com


President Kikwete starts to talk about the road Arounnd 09:26 (on the video timer)

Fellow countrymen, it is a fundamental policy of the government of Tanzania to link all the administrative regions (provinces/ states) of Tanzania by tarmac roads. In implementing that policy on the part of the Arusha and Mara regions, the government has decided to build a tarmac road, from Musoma , Bunda to Mto wa Mbu passing through Mugumu and Loliondo.

In recognizing that this road must pass through the Serengeti Reserve/ Park, and in recognizing the importance of environmental conservation in the Serengeti Reserve, the part of this road which will be inside the Serengeti reserve will not have tarmac. This part will be paved with gravel like all other roads in the Serengeti reserve as of now, as well as other roads in other reserves in the country.Fellow countrymen this decision of the government has caused a passionate debate among people with interests in the environment and wildlife conservationist.I am aware there are people opposed to the construction of this road, for sure they are vehemently opposed to it, and most of them are coming from outside of our country.

I would like to assure these friends of ours, that I am one of the chief environmental activists and a great admirer of the Serengeti reserve, I have visited the reserve many times, I think more than twenty times now. Because of that, I will be the last person to accept something that has a great negative impact to the Serengeti reserve to take place, I will not accept that. I am also passionate about the development of our country, and the development of our it's people, including the people living near the Serengeti reserve, but outside the reserve.

These countrymen deserve and have a right to get access to development just as their fellow countrymen do all over the country when they get tarmac roads. For one to deny them that right because of the Serengeti reserve, while they live outside the reserve, and they have been living outside the reserve all their lives, it is difficult to get agreeable/ fitting explanation to tell them so they can understand you. I would like my fellow environmental activists, and fellow admirers of the Serengeti reserve, to recognize this truth and give it it's proper weight. It is not wise to have a thinking that cares only for one side, without caring for the interests of the other side. We must have a thinking that
aims to consider the interests of both sides.

Fellow countrymen, sometimes when I hear these noises (protests) I wonder and ask myself many questions without getting adequate answers. The truth is that vehicles going to Musoma and Mwanza from Arusha do pass right through the center of the Ngorongoro and Serengeti reserves, and when you consider the length, from the Ngorongoro gate , where the vehicles enter into the Ngorongoro reserve all the way to where the vehicles leave at the 40 Ikoma gate, where the Serengeti reserve end, these vehicles traverse 204 kms inside the reserves, and if you will go to emerge at the gate on the way to Mwanza, one place called Kidabaga, the distance is even longer. But using this newly proposed road, vehicles will pass through the reserves for only a distance of 50 km, they will have passed through. The tarmac road from Bunda and Musoma through Mugumu will end at a place called Tabora B. And the one from Mto wa Mbu through Loliondo will end at a place called Klein's camp, and the distance from Klein's camp and Tabora B is the Serengeti reserve, which is a distance of 50 kms only, and the thinking is once we have this road vehicles will not pass through the center of the reserves for the distance of 204 kms, the only vehicles which will continue to pass through that area will be for those going to look at animals, so my fellows, is that enterprise that bad ?

Fellow countrymen those of us in government are ready to listen to different views, but their suggestions should also answer the questions and issues from the people of the districts of Ngorongoro and Serengeti who are living outside the reserves

END OF part 1 VIDEO,

Part 2

[video=dailymotion;xe7uuk]http://www.dailymotion.com/video/xe7uuk_hotuba-ya-kikwete-mwisho-wa-mwezi-j_news#from=embed[/video]

The people of Mugumu, meaning from the district of Serengeti are asking why shouldn't they get a good road, tarmac like their fellow Tanzanians, this is a legit question that needs appropriate answers. Fellow Tanzanians according to the Electoral Commision's timetable... he then goes on to talk about the election timetable and motivating people to vote.
 
The concern sio lami kwa ajili ya watalii kupita. The concern ni hiyo barabara ku'create some sort of heavy traffic pindi malori, magari yakiwa yanapita katika mbuga kubwa kama Serengeti. Kuna tatizo pia la poachers - ni sawa na unawarahisishia namna ya kuperuzi mbugani. And most importantly uwepo wa lami au barabara kubwa katika mbuga kama serengeti itahathiri the great wildebeest migration.
Jibuni hoja za Rais. Tayari Serengeti na mbuga nyingine zinapitwa na barabara sasa hivi. Hii mpya tofauti yake nini? Na kuathiri uhamaji wa wanyama, kasema kitakuwa ni kipande cha km 50. Mjibuni Rais kwa nini wanyama hawataweza kupita kwingine huko, Serengeti si kubwa bana? Kuwarahisishia majangiri, naona ni hoja dhaifu, ni sawa na kusema usinunue gari unakaribisha wezi. Imarisha ulinzi, tekeleza sheria.

Au serikali yetu inapata presha hii kutokana na mining interests?
"Au?" Kumbe huna hakika.
 
Jibuni hoja za Rais. Tayari Serengeti na mbuga nyingine zinapitwa na barabara sasa hivi. Hii mpya tofauti yake nini? Na kuathiri uhamaji wa wanyama, kasema kitakuwa ni kipande cha km 50. Mjibuni Rais kwa nini wanyama hawataweza kupita kwingine huko, Serengeti si kubwa bana? Kuwarahisishia majangiri, naona ni hoja dhaifu, ni sawa na kusema usinunue gari unakaribisha wezi. Imarisha ulinzi, tekeleza sheria.

"Au?" Kumbe huna hakika.

Mazee umeiangalia ramani ya barabara itakapopita au unajisemea tu ? Unafahamu chochote kuhusu migration patterns ? Unafahamu zikiwa disturbed nini kitatokea?

Yaani Kikwete katia aibu kweli, environmentalists wameleta hoja kibao zilizo complex, yeye kaja na ki solution cha shule ya msingi. I am not saying that I have concluded my thinking either way, I need to know the full environmental and economic impacts to do that - currently studying a similar road project in the Kruger and another that averted it in Russia- but all I am saying is that Kikwete hakuja na case, basically amekuja na a weak political strategy, wana protest barabara isipite Serengeti? waambie hatutaweka lami, anawafanya kama watoto kwamba "mtoto analilia kununuliwa kigari? Mpe kibox cha sabuni achezee. Mimi nilitegemea watu wa Ikulu wafanye researches za kujibu maswali magumu ya wanamazingira kama wanaendelea na hii project, hawakufanya hivyo.

Tusije kununua bad press itakayotugharimu kiuchumi na barabara itakayotugharimu zaidi kimazingira kuliko barabara hiyo inavyoweza kutusaidia kiuchumi.
 
The concern sio lami kwa ajili ya watalii kupita. The concern ni hiyo barabara ku'create some sort of heavy traffic pindi malori, magari yakiwa yanapita katika mbuga kubwa kama Serengeti. Kuna tatizo pia la poachers - ni sawa na unawarahisishia namna ya kuperuzi mbugani. And most importantly uwepo wa lami au barabara kubwa katika mbuga kama serengeti itahathiri the great wildebeest migration.

Kuna suggestion ya barabara ili ipite kusini mwa serengeti, ambapo itasaidia vijiji zaidi kuliko hiyo tunayong'ang'ania ya kaskazini. Tazama hapa. Au serikali yetu inapata presha hii kutokana na mining interests - migodi itakayotaka barabara ipitie kwao?

Jinsi watu wanavyoongezeka ni dhahiri mbuga zitazidi kuvamiwa na poachers na itafika muda hao wanyama watakuwepo zoo tu, lakini kama leo barabara inafungua njia za uchumi kwa watu waliofungiwa huko hicho ndo muhimu zaidi kuliko kuogopa kuathiri hizo njia za wanyama kuhama. Nature itawaambia wanyama wahame vipi, pia twaweza jenga barabara juu kwa juu sehemu za kupita wanyama.

Raia wanafaidika vipi na mapato ya utalii Serengeti? ama ndio pesa yote inaishia kwa jirani. Mbuga zinasimamiwa na serikali na serikali haina ufanisi wowote, sasa si bora hata hiyo barabara ijengwe ili kila anayeishi huko ajuwe memwenyewe cha kufanya.

Optional route sio practical
 
Mazee umeiangalia ramani ya barabara itakapopita au unajisemea tu ?
Nimeona ramani? Mitazamo ya wakosoaji wa kwenye makochi. Nimeona ramani? Napita humo kwenda mikoani!

Unafahamu chochote kuhusu migration patterns ? Unafahamu zikiwa disturbed nini kitatokea?
Naam, nijuvye mkuu.

... I need to know the full environmental and economic impacts to do that - currently studying a similar road project in the
Msalie mtume. Kumbe na wewe hujui. Hiki kituko kinadai mradi una madhara kumbe na chenyewe kinakiri hakijui kitu ndio kwanza kinapitia pitia kurasa.

...Mimi nilitegemea watu wa Ikulu wafanye researches za kujibu maswali
Unajuaje hawajafanya? Kama madai ya Ikulu ni ya kitoto basi jibu hoja za Rais: sasa hivi tayari kuna mabarabara yanapita mumo humo Serengeti, na mbuga nyingine, reli la Tazara linakata katikati ya Selous, km kibao, njia mojawapo ya Dar-Mwanza inakatisha Ngorongoro na Serengeti umbali wa kutosha. Hii njia mpya tofauti yake nini? Jibu!

Tusije kununua bad press itakayotugharimu kiuchumi ...
Na labda ndio tutajifunza kusimama kivyetu kama wa Cuba na wa Libya.

Kuna siku Tanzania ilijulikana kwa kutoogopa taswira mbaya Magharibi, Reagan aliwekwa kiti moto na Watanzania kwenye mkutano Mexico, Henry Kisinger alikuja Dar amefungiwa chakula cha safari nzima akaambiwa rudi na vifuko vyako vya chakula au utakula cha Ikulu na hoteli za hapa, Wajerumani walitushinikiza ki mfumo dume wakitishia kukatisha misaada ya miundombinu ya umeme kama tukiendelea kukataa wasisimike kambi ya kijeshi, Tanzania ikawaambia ng'oeni mitarimbo yenu ya umeme haraka sana, msitufanye wake zenu kwetu. Hatuandiki sera kutokana na watawala dunia wa Magharibi wanavyotaka.
 
Serikali yetu imeamka na imegundua kuwa haina budi kuanza kujenga barabara nzuri kwenye mikoa mbalimbali nchini. Kama una kumbukumbu nzuri, juhudi hizi zilianza kwa kujenga daraja ambalo lilitakiwa kuunganisha Tanzania na Msumbiji — tunajua matokeo yake.

Wakati tunajua fika kuwa barabara nyingi nchini ni mbovu kupita kiasi, na ambazo zinajengwa huonekana kama zinachukua miaka kukamilika, tuzungumzie mpango wa kujenga barabara itakayokuwa inaunganisha Arusha na Musoma; takribani kilomita 480 za barabara ya lami.

serengeti-map21.jpg


Ndio, kama ulivyoona hapo juu, barabara hii itakuwa inakatiza kwenye mbuga ya wanyama ya Serengeti.

Napenda kuwakumbusha wahusika kuwa kuna watu ambao kama wangekuwa na uwezo wa kupigana vita na kuichukua hii mbuga, wangeshaichukua kabla ya mimi na wewe hata hatujaona mwanga wa jua. Watanzania na Wakenya, hii mbuga ina thamani kuliko tunavyofikiria. Wapi kwengine utaona idadi kubwa ya nyumbu na pundamilia wakihama kutokana na mabadiliko ya majira?

nyumbu-300x200.jpg

Sasa, nitajaribu kuweka hisia pembeni na kuuliza wahusika maswali ya msingi ili tufahamu kama wanajua wanachofanya:

* Wamesema kuwa wamefanya feasibility study na matokeo yake ni kwamba barabara hii haitaathiri uhamaji wa nyumbu na pundamilia. Tungeomba basi tuone hiyo ripoti na watueleze njia walizotumia kufikia hitimisho na ukubali wa kujenga hiyo barabara. Kama ni simulation programs, watupe basi na sisi tujaribu kuangalia kama kuna ukweli wowote.
* Mpaka sasa hivi sidhani kuna mtu ambaye ana kiburi cha kusema anajua tabia za wanyama (kila kitu). Hizi documentary films tunazoona zinatupa tu mwangaza wa tabia za wanyama. Sasa, sielewi kwanini wanaongea kama wanajua kila tabia za nyumbu na pundamilia.
* Watu wa Tanapa wanadai hii barabara itasaidia kukwamua wakazi wa Arusha na Musoma kiuchumi au kibiashara. Sawa. Lakini faida za hii barabara ni kubwa kuliko athari za aina yoyote ile zitakazoweza kuletwa na hii barabara? Tungependa kuona namba na taarifa kamili.
* Nchi za Magharibi zimeanza kupika kelele (na mimi nawaunga mkono); sasa wakianza kugoma kuja Serengeti kutokana na hili sakata itakuwaje? Mara ya mwisho nadhani nilisikia kuwa chanzo kikubwa cha mapato Tanzania ni utalii. Kuna uwezekano mkubwa kuwa huu mpango ukiendelea, idadi ya watalii inaweza ikapungua kwa kasi ya ajabu…

Ukiacha haya yote, ukimya wa Watanzania kwenye hili suala ni kitu kinachosikitisha sana kusema ukweli. Yaani watu wa Magharibi ndio wanaongoza kwa kupiga kelele. Hivi, tunadhani juhudi au kelele zao ni upumbavu tu au hatujui faida za mbuga kama ya Serengeti? Tuwaache viongozi wetu wafanye wanachotaka kwasababu watu wa Magharibi wanatuletea ukoloni mamboleo?

Nitaishia hapa kwa leo.

Oooh, kabla sijasahau. Lile bonde na Ngorongoro nalo ni kero. Itakuwa jambo la busara wakijenga overpass kuunganisha Ziwa Natron na Ziwa Magadi.

source: VijanaFM
 
Jibuni hoja za Rais. Tayari Serengeti na mbuga nyingine zinapitwa na barabara sasa hivi. Hii mpya tofauti yake nini? Na kuathiri uhamaji wa wanyama, kasema kitakuwa ni kipande cha km 50. Mjibuni Rais kwa nini wanyama hawataweza kupita kwingine huko, Serengeti si kubwa bana? Kuwarahisishia majangiri, naona ni hoja dhaifu, ni sawa na kusema usinunue gari unakaribisha wezi. Imarisha ulinzi, tekeleza sheria.

"Au?" Kumbe huna hakika.

Soma ripoti kuhusu hili suala linalotoa onyo kuhusu uharibifu utakaotokea kwa ujenzi wa aina yeyote wa lami kuelekea mbugani Serengeti:

African Wildlife Foundation Report

Frankfurt Zoological Society Report
 
Wanyama wa instincts pia....hata ukijenga ukuta mpaka wote na Kenya watatafute alaternative hata kama iwe kwenda Ruaha:yawn:
 
Jibuni hoja za Rais. Tayari Serengeti na mbuga nyingine zinapitwa na barabara sasa hivi. Hii mpya tofauti yake nini? Na kuathiri uhamaji wa wanyama, kasema kitakuwa ni kipande cha km 50. Mjibuni Rais kwa nini wanyama hawataweza kupita kwingine huko, Serengeti si kubwa bana? Kuwarahisishia majangiri, naona ni hoja dhaifu, ni sawa na kusema usinunue gari unakaribisha wezi. Imarisha ulinzi, tekeleza sheria.

"Au?" Kumbe huna hakika.

Tindikali mpango wa rais mwanzoni ulikuwa kujenga lami/highway ipite ndani ya Serengeti reserve kukatisha mbuga from EAST-WEST. Alisema haya wakati akitoa ahadi kwenye kampeni yake iliyopita - wakati huo huo anasema yeye ndiye mkereketwa namba 1 wa mazingira. Kumbuka kuwa mamilioni ya nyumbu na pundamilia wanakatiza mbuga kila mwaka SOUTH-NORTH kwenye hiyo 'great migration'

Barabara za lami unazosema zinapita mbugani si ukweli wote, nyingi ni changarawe na ni kwaajili wa watalii kuperuzi mbugani. Ni mikumi tu ambapo nimeona A7 Highway inapita, na kukata kipande kidogo tu cha hifadhi; Tazama hapa. Nyingi zinapita pembezoni mwa hifadhi. Kwa serengeti, utajengaje highway inayoelekea (kwa pande zote) sehemu ya hifadhi halafu uache kipande ndani ya mbuga na ku'expect athari watu wanazohofia kutoweka? Mlolongo wa malori (ya petroli, mizigo) utabaki pale pale, magari yatakimbizana kwa kasi pungufu kidogo tu- na since traffic itakuwa kubwa, eneo hili la pembezoni litaanza kujenga miji midogo midogo. In no time, hamna cha serengeti wala nini.

Watu wenyewe tunajua hatutembelei mbuga despite kiingilio kwetu ni USD 1 na wageni USD 50 - kwahiyo umuhimu wa mbuga hii kwa utalii ni mkubwa.
 
Nimeona ramani? Mitazamo ya wakosoaji wa kwenye makochi. Nimeona ramani? Napita humo kwenda mikoani!

Naam, nijuvye mkuu.

Msalie mtume. Kumbe na wewe hujui. Hiki kituko kinadai mradi una madhara kumbe na chenyewe kinakiri hakijui kitu ndio kwanza kinapitia pitia kurasa.

Unajuaje hawajafanya? Kama madai ya Ikulu ni ya kitoto basi jibu hoja za Rais: sasa hivi tayari kuna mabarabara yanapita mumo humo Serengeti, na mbuga nyingine, reli la Tazara linakata katikati ya Selous, km kibao, njia mojawapo ya Dar-Mwanza inakatisha Ngorongoro na Serengeti umbali wa kutosha. Hii njia mpya tofauti yake nini? Jibu!

Na labda ndio tutajifunza kusimama kivyetu kama wa Cuba na wa Libya.

Kuna siku Tanzania ilijulikana kwa kutoogopa taswira mbaya Magharibi, Reagan aliwekwa kiti moto na Watanzania kwenye mkutano Mexico, Henry Kisinger alikuja Dar amefungiwa chakula cha safari nzima akaambiwa rudi na vifuko vyako vya chakula au utakula cha Ikulu na hoteli za hapa, Wajerumani walitushinikiza ki mfumo dume wakitishia kukatisha misaada ya miundombinu ya umeme kama tukiendelea kukataa wasisimike kambi ya kijeshi, Tanzania ikawaambia ng'oeni mitarimbo yenu ya umeme haraka sana, msitufanye wake zenu kwetu. Hatuandiki sera kutokana na watawala dunia wa Magharibi wanavyotaka.

Huyu jamaa ni fanatic. Mimi namwambia kuhusu ramani ya barabara inayotaka kujengwa - ambayo haipo sasa hivi- yeye ananiambia anapita humo!

Mimi namwambia sijaamua upande mmoja au mwingine, nataka kujua zaidi, yeye anasema nishasema tayari kwamba barabara ina madhara.Labda anisaidie kunionyesha wapi nimesema hivyo.

Tatizo hapa kuna watu wana ego ziko zinaweza kuchezewa kama za watoto wadogo, Kikwete akishatumbukiza tu karata ya kisiasa ya kusema "wanaopinga wengi wanatoka nje ya nchi" basi kila mtu anataka kuwa ngangali bila kufikiri, eti tuwe kama Gaddafi wa Libya.

Hawajui hata huyo Gaddafi wa Libya naye kasalimu amri under international pressure.

Hawajui kwamba hata ukiondoa swala la mazingira, useme mimi ni mchumi nisiyejali mazingira (mchumi mbaya sana kwa sababu uchumi kimsingi ni kutumia mali vizuri) bado kuna uwezekano kwamba argument inayosema kwamba barabara hii italeta mabaya zaidi ya mazuri kwa uchumi wa Serengeti na Tanzania.

Huyu Tindikali ana kichaa cha kiburi kwa watu wa magharibi kama babu yake Nyerere, na yeye akiletewa swala kitu cha kwanza kufikiria ni sovereignty. Tulishauza sovereignty zamani kwa kushindwa kujitegemea kiuchumi, hata hii barabara yenyewe tunayojidai kujipiga kifua kwamba tusiambiwe lolote na watu wa nje hatuijengi kwa hela zetu, leo hii mchina akisema hatoi hela za ujenzi tutawarudia hao hao wazungu tunaowatukana hapa cap in hand kuomba msaada ili kuijenga barabara hii hii.

Watu wanaoelewa vizuri sovereignty wanajua hakuna kujitawala kisiasa bila kujitawala kiuchumi. Na katika kujitawala kiuchumi inabidi ujue kufanya biashara ya kimataifa kama utalii.

Ama sivyo tutabaki ngangali, utalii unaweza kushuka, Serengeti inaweza kuharibika, barabara isitupe faida ya kutosha, tukabaki tunakosa vyote, tunaendelea kugawana umasikini kama kawaia yetu.

.
 
Soma ripoti kuhusu hili suala linalotoa onyo kuhusu uharibifu utakaotokea kwa ujenzi wa aina yeyote wa lami kuelekea mbugani Serengeti:

African Wildlife Foundation Report

Frankfurt Zoological Society Report

Kwa wale wanaodhani Serikali inafanya la maana, nadhani ingekuwa vizuri mkisoma ripoti ya TANROADS kwanza (kuhusu hii barabara), halafu muilinganishe na hizo hapo juu:

http://vijana.fm/wp-content/uploads/2010/07/Serengeti_Road_Report.pdf

Nadhani mdahalo utaelekea kuzuri...
 
Ah asavali waijenge hiyo barabara kwani hao Wanyama hawatusaidii lolote sisi walavumbi,sana sana hela itokanayo na hao wanyama inaenda kwa wazungu na wabaka uchumi wao waliopo hapa Tanzania

Maneno ya kipumbavu kwa mustakabali wa taifa letu.
 
katika kila hizi issue tungepata mtu wa kutupa ENVIRONMENT ASSESMENT REPORT kwa project kama izi, maana ku jugde kua ina madhara au la lazima iyo report iweke wazi badala ya kila mtu kutoa quote ya maneno flan aliyoyadownload kwa net! nilipinga initially lakini nikagundua ckufanya uchambuzi sahihi kwanza ni kupata iyo pepa iliyoandaliwa kwanza

Ilishawekwa kwenye thread nyingine. Mods unganisheni threads za Serengeti highway tuwe na mtiririko mzuri.
 
..kuna watu wanafikiri kwamba hao wanyama, especialy, nyumbu, eventually wata-adopt na kujifunza kuvuka hiyo highway.
 
..tatizo Raisi hakueleza kwanini barabara inayokatiza mbugani Serengeti ni better kwa mazingira na uhifadhi wa mbuga hiyo kuliko barabara inayopendekezwa na wanaharakati ambayo haikatizi mbugani.
 
BARABARA HIYO ITAJENGWA, HATA KAMA WANYAMA WATAKOSA NYASI! NA SIO HIVYO TU, RELI NAYO ITAJENGWA KATI YA ARUSHA NA MUSOMA!

LEO HII kuna barabara ya Musoma - Arusha! Inapita katikati ya Mbuga za Wanyama Serengeti! Hii haina lami!

Kuna barabara ya Morogoro - Iringa! Inapita katikati ya Mbuga za Wanyama za Mikumi! Hii ina lami!

Rais Kikwete alisema hiyo itakayojengwa sehemu za Serengeti haitawekwa lami! WEKA LAMI, TENA YA KUDUMU MIAKA HATA 20 BILA KUKARABATIWA NA KUHUDHI HAO WANYAMA!
 
Back
Top Bottom