CALL FOR SUPPORT: To Build or not To Build - The Serengeti Highway saga

Dokta wa ukweli chukua nchi huyu dokta feki kshindwa linda mipaka ya nchi yetu kabisaaa
 
Well said Mr Chama i appeciate your post.let take an example of ATC &TRC....kampuni halina ndege hata moja ila lina wafanyakazi na kila siku wanaenda kazini na mwisho wa mwezi wanakula mshahara? wtf are we doing ? tu improve kwanza barabara ambazo tunazo tayari na ni mbaya hazipitiki kuliko kun'gan'ganiza barabara ndani ya mbuga wajameni

Tatizo kubwa la serikali hii ya CCM imejaa viongozi ambao ni uozo na hawana uchungu wa nchi wapo kwa ajili ya kuijtarisha kwa maslahi yao binafsi, dhana nzima ya utaifa na uzalendo haipo.

Haya mashirika mawili ni kigezo kikubwa cha nchi yetu kuanguka kwenye sekta nzima ya usafirishaji. Ninachojiuliza kwa nini hawataki kujifunza kutoka kwa nchi nyingine za Afrika? Nchi ambazo zimepata mafanikio kwenye sekta ya anga zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa baada ya kuuza hisa kwa mashirika makubwa ya kimataifa, mfano hai ni Ethiopian na Kenya Airways.

Leo hii mapato ya kigeni ya Ethiopian airways yanachangia zaidi 1/4 ya budget ya nchi, kuna sababu kwa shirika la reli kufa wakati nchi za jirani Uganda, Rwanda na Burundi zote zinategemea reli yetu mapato yanakwenda wapi haya ni matokeo ya kuweke wakurugenzi kwa kujuana, Bodi zimejaa wabunge ambao ni darasa la saba kweli tutafika?

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Hivi hawa the socalled cönsultants wana uchungu wa kweli kuhusu ecosytem ya Serengeti? Ukweli wa mambo ni kwamba hawana badala yake wana an hidden agenda ya kukwamisha maendeleo ya kiutalii TANZANIA.

Majirani zetu hawatutakii mema Tanzania wanatumia mbinu za kila aina kwa kutumia watu wa Ulaya kuhujumu nchi yetu kiuchumi kupitia campain za eti Kulinda mazingira. Kumbuka vurugu za wafugaji zilizo wahi kutokea Loliödo mchochezi alikuwa Mkenya.

Wakenya hawa hawa waliwahi kupinga eti hoteli nzuri zisijengwe kwenye mbuga za Serengeti kisa kulinda eti mazingira. Wanayasema haya huku wenyewe wamejenga barabara nzuri na mahoteli ya kifahari huko kwao Masai Mara.

Je hao wanyama wa Masai Mara wanatoka wapi kama siyo Serengeti - hawa jirani zetu ni wanafiki, wahujumu, wafitini na wana inbuilt notion ya kuona Watanzania kama wajinga na wazubaishi, hapa siyo kwamba nawasema vibaya ukweli wa mambo kwamba hawahitakii mema Tanzania period.

Labda nitoe mfano hai ya kuonyesha determinatinn yao ya kuhujumu nchi yetu kiuchumi:

Mwaka juzi walifanya lobbing kimataifa ili pembe za ndovu zilizo kamatwa Vietnam zisihuzwe kwenye open market hili taifa linufaike, sasa hivi wako mbioni kujenga uwanja wa ndege karibu kabisa na Kilimanjaro airport na kuvunja makubariano yaliyo wahi kufikiwa kwamba jambo kama hilo lisifanyike - kwani wanajali?

Jakaya yuko sahihi kabisa afumbe macho na masikio afanye mambo ambayo anaona yatanufahisha taifa hili na vizazi vijavyo hasiwasikilize hawa prophets of doom namely "Ecosystem Consultants" kuhusu Serengeti hawa jamaa kama nilivyo eleza humu wana a hidden Agenda and don't you forget that the brains behid this SCAM is our jirani don't underrate 'em wako determined and highly organised.
 
Tanzania yote ina hifadhi za taifa, siyo rahisi kujenga barabara tz bila kupitia hifadhi za taifa. mikumi , udzungwa, katavi zote humo barabara zimepita hifadhini na hatujaona tatizo lolote.Hivyo barabara hiyo ijengwe na hakuna madhara yoyote na zaidi ya hayo itasaidia usafiri wa uhakika wa kwenda hifadhini.
 
Eti "" The United States has expressed concerns to Tanzania's government about the impact of its plan to build road through the Serengeti that environmentalists say could affect the famed wildebeest migration and threaten endangered species"" this to me seems another nonsense.

Hivi hawa wamarekani wanatoa wapi ujasiri wa kusema wanalinda mazingira na hao species wanazosema.....hivi hawajui kweli ni kiasi gani cha uharibifu wanachangia ktk kuvuruga mfumo wa hali ya hewa(ambao unazidi kuumiza viumbe walioko Serengeti na sehemu nyingine) kwa kudondosha mabomu Iraq, Afghanistani, Pakistani na sasa Libya...hivi wanadhani sisi ni mambumbumbu kiasi cha kutoona wanayofanya.....

Mkuu heshima kwako!! Hawa jamaa ni wahuni na wasanii kweli. Hadi leo wamegoma kuadhere the Kyoto Protocol. Juzi kwenye COP 15 pale Copenhagen wameleta usanii tena. Afu walivyo washenzi wanajifanya kutoa msaada wa kupambana na hali hiyo kupitia kwa REDD (Reduced Emissions from Deforestation and Forest Degradation) ingawa Norway ndio financier mkubwa.

Nchi zenye viongozi wenye umaskini wa akili kama zetu ndio ziko kipaumbele kukimbilia pesa hizo huku zikishindwa kuzimabia ukweli nchi kama Marekani kua zenyewe ndio zenye uwezo wa kupunguza tatizo kwa kuacha kutoa hewa ya ukaa......

Hivyo ni kweli Marekani ni msanii anajua kabisa chanzo cha tatizo, lakini anataka kusingizia ujenzi wa barabara kama ndio itaharibu bioanuai (biodiversity).

Asante
 
Tanzania yote ina hifadhi za taifa, siyo rahisi kujenga barabara tz bila kupitia hifadhi za taifa. mikumi , udzungwa, katavi zote humo barabara zimepita hifadhini na hatujaona tatizo lolote.Hivyo barabara hiyo ijengwe na hakuna madhara yoyote na zaidi ya hayo itasaidia usafiri wa uhakika wa kwenda hifadhini.


Mkuu heshima kwako!!

Matatizo yapo katika barabara hizo. Jaribu kutafuta evidences za road kills katika hifadhi, utapata information zaidi.

Ila jambo la msingi hapa la kuangalia ni kulinganisha uwiano wa faida zinatokana na utunzaji wa maliasili hizo na faida zitakazotokana na ujenzi wa barabara hiyo kwa taifa. Kwa kuliangalia suala hili kwa undani zaidi ndipo tutaweza kuwa na concrete arguments juu ya ujenzi wa barabara au utunzaji wa maliasili!

Asante
 
Back
Top Bottom