Calculation ya kodi iangaliwe upya

Calculation ya kodi iangaliwe upya

Barya

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2012
Posts
949
Reaction score
1,196
Naanza kwa kusema kuwa mi ni mwanachama wa CCM tokea mwaka 2002 na mwanachama hai kabisa,

Usomaji wa namba huu unatuumiza watu wengi sana tena ambao ni wachanga katika biashara, binafsi sipendezwi na jinsi mtu anavyokamuliwa hela ya kutosha hasa kama unaingiza vitu kutoka nje, sijapenda kabisa

1. Pale airport dar es salaam, mtu ukiwa na mzigo wa sh 38,000,000 kodi ya kutozwa ni zaid ya milion 10 hela ambayo nimekuwa nikitozwa mpaka kushangaa, hii inaumiza sana , maana ukamuaji huu umepitiliza sasa,

Nina evidence za kutosha, jana mzigo umekuwa cleared airport, thaman yake ni sh 62,500,000 lakin nashangaa nimetozwa hela 43% kama malipo ya hapa na pale, TBS 15% TRA 18% Sijui cargo clearance fee asilimia kadhaa, sijui argent fee, jumla nimelipa ths 26,300,000 sasa hapo tunaumizana sasa vitafutwe vyanzo vingine tofauti na kubana sisi ambao ndo tunaansa alafu mnatukamua, pia sitaki kutaja mazingira mengine yalotokea pale ya kitu kidogo maana nikiwataja watashindwa kunipitishia mzigo Wangu tena na saa nyingine kubambikiwa kesi ya madawa au nyara za serikali

Tunaingizwa hasara sana, maana mpaka sasa mizigo yangu imekwama, na mbaya zaid storage fee unaendelea kuwa kubwa kisa kodi zisizo eleweka,

Mi naona wangekuwa waungwana tu

Kwa trend hii naona mheshiniwa BADO ANA KAZI KUBWA YA KUFANYA KUVUMBUA VYANZO VINGINE VYA KODI, japo nasisi inabidi kulipa kodi stahiki,
 
Pole mkuu, kumbe wewe ni ccm duu mimi nilishahama hiki chama kisicho jua kutafuta vyanzo vingine vya mapato,watu wanakaa na kufikiria vitu vidogovidogo tu wanaacha madini na mali asili zingine za nchi hii zikiwaneemesha watu weupe
 
Haha kweli kibila tatizo langu siwekezi sana katika kutegemea vyama ndo maana unakuta niko na chama hicho hicho miaka yote maana siko active katika siasa, lakin nataka kujiuliza we mtu ndo una kamtaji kako umejikwamua uanze kutoka.mtu anakutoza robo na zaid ya hela ile, pia nje ya hapo mizigo inachelewa kutoka hadi inakatisha tamaa
 
Naanza kwa kusema kuwa mi ni mwanachama wa CCM tokea mwaka 2002 na mwanachama hai kabisa,
Usomaji wa namba huu unatuumiza watu wengi sana tena ambao ni wachanga katika biashara, binafsi sipendezwi na jinsi mtu anavyokamuliwa hela ya kutosha hasa kama unaingiza vitu kutoka nje, sijapenda kabisa
1. Pale airport dar es salaam, mtu ukiwa na mzigo wa sh 38,000,000 kodi ya kutozwa ni zaid ya milion 10 hela ambayo nimekuwa nikitozwa mpaka kushangaa, hii inaumiza sana , maana ukamuaji huu umepitiliza sasa,

Nina evidence za kutosha, jana mzigo umekuwa cleared airport, thaman yake ni sh 62,500,000 lakin nashangaa nimetozwa hela 43% kama malipo ya hapa na pale, TBS 15% TRA 18% Sijui cargo clearance fee asilimia kadhaa, sijui argent fee, jumla nimelipa ths 26,300,000 sasa hapo tunaumizana sasa vitaftwe vyanzo vingine tofauti na kubana sisi ambao ndo tunaansa alafu mnatukamua, pia sitaki kutaja mazingira mengine yalotokea pale ya kitu kidogo maana nikiwataja watashindwa kunipitishia mzigo Wangu tena na saa nyingine kubambikiwa kesi ya madawa au nyara za serikali

Kwa trend hii naona mheshiniwa BADO ANA KAZI KUBWA YA KUFANYA KUVUMBUA VYANZO VINGINE VYA KODI, japo nasisi inabidi kulipa kodi stahiki,
Namba inasomeka sawa sawa. Hakuna aliekulazimisha kuichagua push up.

Kumbuka kale kanyimbo cha mtaisoma namba ulichokuwa unakakenulia meno na mbaya zaidi ulidhani push up ndio zinahitajika ikulu ukasahau akili kubwa iliyokuwa na mipango madhubuti ya kuendeleza nchi.

Acha dawa iwaingie.
 
Mi sifichi siwez kupigia kura mtu asiye na nia njema katika uongizi wake, nakomea hapa
 
Namba inasomeka sawa sawa. Hakuna aliekulazimisha kuichagua push up.

Kumbuka kale kanyimbo cha mtaisoma namba ulichokuwa unakakenulia meno na mbaya zaidi ulidhani push up ndio zinahitajika ikulu ukasahau akili kubwa iliyokuwa na mipango madhubuti ya kuendeleza nchi.

Acha dawa iwaingie.
Pia uchaguzi siyo kitu cha kuendeleza sana kama kampeni katika maisha ya kawaida
 
Haha kweli kibila tatizo langu siwekezi sana katika kutegemea vyama ndo maana unakuta niko na chama hicho hicho miaka yote maana siko active katika siasa, lakin nataka kujiuliza we mtu ndo una kamtaji kako umejikwamua uanze kutoka.mtu anakutoza robo na zaid ya hela ile, pia nje ya hapo mizigo inachelewa kutoka hadi inakatisha tamaa

Hatupaswi kutegemea siasa mojakwamoja ili tupate maendeleo ya mtu mmoja mmoja ila kumbuka siasa safi ndio msingi wa maisha bora kwa mwananchi.

wewe muda huu unalalamika kuwa wanakupiga hela sana sasa uoni impact ya siasa hapo ambayo tena inagusa maisha yako moja kwa moja tusijidanganye kuwa siasa tuwaachie wanasiasa mimi nina amini siasi kwa upande mmoja inaweza amua maisha ya mwananchi.

Mfano leo hii mimi nalima lkn kwa kuwa tu, tuna siasa mbovu pembejeo za kilimo nazipata kwa shida, mara ziwe feki haya baada ya kutoa mazao shambani nakuja kukutana na soko bovu ushuru kila mahali sasa hapo mimi ntajikwamua vipi na maisha yangu mkuu
 
Na utulie sindano zikuingie lazima muishi kama mashetani
 
Sio hapo tu Tanzania ni nchi pekee duniani ambapo ukitoka Ku register kampuni.....

Uwezi kwenda moja kwa moja na certificate yako bank na kufungua account ya kampuni....

Mpaka upite TRA eti wakukadilie kodi na ulipe sasa unajiuliza kodi inatakiwa ilipwe kwenye faida .

Sasa hiyo faida ya kampuni iko wapi wakati kampuni yenyewe haijafungua hata account?....

Tukiwaambia mazingira ya kufanya biashara Tanzania ni magumu bora ukaaka ulaya ukabeba box mnabisha....
 
Kila kitu ni sera na hizo tozo ni moja wapo ya sera zitokanazo na siasa. Usipofushe na kijani ukasahau kuna maisha njee ya mdudu wa kijani.
Kweli lakin kaka wanapokosea wakosolewe lakin hata wangekuwa UKAWA pia kuna jambo wangefanya likamuumiza Mwana UKAWA haimaanishi kuwa wangefanya kwa hundred percent
 
Inakatisha tamaa

Hata mm ni CCM long ago.. kwani CCM tunalipa kodi..? Ok nimekumbuka, kipindi hiki cha JPM hakuna cha CCM wala nani.. wote ni kulipa kodi tu.. nimekumbuka..

Lipa kodi kwa maendeleo ya nchi yetu.. hata ukiwa CCM yapaswa kulipa..
 
Sawa lakin si kwa calculations hiyo
 
Kelvin ipi nia yako iliyokusababishia kutaja UANACHAMA WAKO?/ ili iwaje?,au kipi kitokee?,au ndio itaipa uzito hoja yako?/

Alitaka akiwa CCM asilipe kodi au apunguziwe.. ndio nia yenyewe.. ndio maana alianza yeye ni CCM hai.. ha ha haaaa..
 
Back
Top Bottom