CAG: Wabadhirifu, mafisadi sasa kukiona

CAG: Wabadhirifu, mafisadi sasa kukiona

kibogo

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
9,739
Reaction score
4,746

UTUH.jpg

Mr Utouh

Bagamoyo. Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Jasper Nicholaus Mero amesema pamoja na pongezi ambazo Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi inapokea, wananchi wa kawaida wameonyesha kutoridhishwa na hatua zinazochukuliwa dhidi ya watu wanaobainika kufuja mali za umma, kutumia mamlaka yao vibaya kwa mujibu wa ripoti za CAG.

Akizungumza jana katika ufunguzi wa kongamano la matumizi ya ripoti za ukaguzi kwa vyombo vya uchunguzi na wataalamu mbalimbali, Mero alisema kongamano hilo linalofanyika kwa mara ya kwanza ni sehemu ya utekelezaji wa shughuli za mradi wa kuongeza mapambano dhidi ya rushwa chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID).

Alisema kongamano hilo la siku mbili linalowahusisha maofisa wa DCI/PCCB 40, mahakimu 20, mawakili wa serikali 20 pamoja na wengine linalenga kutoa elimu kwa maofisa hao ili kupambana na walaghai, walarushwa na mafisadi.

"Tukiwa wadau katika maendeleo ya nchi yetu, tunao wajibu mkubwa wa kusimamia uwajibikaji na utawala bora. Ni vyema sasa tukatumia fursa hii ya mahusiano ya kisheria kuboresha utendaji kazi wetu ili kurejesha imani ya wananchi tunaowatumikia," alisema Mero.

Aidha, alisema mpango huo utaongeza ufanisi zaidi katika utekelezaji wa matakwa ya sheria ya ukaguzi.

"Kifungu cha 27 cha sheria ya ukaguzi wa umma ya mwaka 2008 kama kilivyofanyiwa mabadiliko na Sheria ya Fedha no. 10 ya mwaka 2010, kinawataka wakaguzi wanaofanya kazi kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, mara tu anapobaini kuwapo kwa viashiria vya ulaghai, kughushi au rushwa wanapokuwa wanafanya ukaguzi kutoa taarifa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu juu ya suala hilo," alisema.


My take
Kama kweli taasisi hii ingekuwa ina meno nafikiri tungeshuhudia wale wote waliohusika katika ufisadi wa EPA, RICHMOND, DOWANS, MEREMETA, KAGODA na sasa hivi ESCROW wakiwa gerezani hadi sasa lakini cha ajabu nguvu zao wanazimalizia kwa vidagaa wakiacha haya mafisadi papa ambayo yamesababisha hadi nchi inakosa misaada kutoka kwa wahisani.
 
Siasa hizo tumezizoe,yaani badala ya kupeleka report ya escrow bungeni yeye kaenda kuvuta bahasha bagamoyo
 
huyo Naibu kwanza anajipigia debe yy ili wamteue kuwa MKAGUZI MKUU, baada ya bosi wake UTOAH Kustaafu.
 
Siasa hizo tumezizoe,yaani badala ya kupeleka report ya escrow bungeni yeye kaenda kuvuta bahasha bagamoyo

eti ""kuvuta bahasha"".

Umenifurahisha kamsemo hako bulaza!!
eh!eh! . so funy aisee!
 
HUYU Naibu wa CAG anaongea UTUMBO HAPA...we are keenly waiting for ESCROW REPORT...ASAP...m.@vi kweli huyu...!!!
 
huyo Naibu kwanza anajipigia debe yy ili wamteue kuwa MKAGUZI MKUU, baada ya bosi wake UTOAH Kustaafu.

Jenerali wala haiko ivo,huyu ni just DAG(Deputy Auditor General) tu kwa ajili Local Government!wa kujipigia debe pengine angesemwa Bwn.Mwakapalila ambae ndio Kaimu CAG
 
Siasa hizo tumezizoe,yaani badala ya kupeleka report ya escrow bungeni yeye kaenda kuvuta bahasha bagamoyo

Alisema eti iko mezani kwake bado anaisoma...

Then hajamaliza kuisoma kaja na huu "mkwara wa mende kuangusha kabati"
 
HUYU Naibu wa CAG anaongea UTUMBO HAPA...we are keenly waiting for ESCROW REPORT...ASAP...m.@vi kweli huyu...!!!

Mkuu CAG siyo kosa lake ila la wanaomtuma.
Wakiona ripoti inawagusa hawaitoi kamwe ili ishughulikiwe.
Ni kama polisi anayetumwa kuchunguza wizi,ikikutwa ameiba mjomba naye alikumegea, ripoti inapotezwa.

Na huo ndo ukweli wenyewe ama sivyo tungejua mwisho wa EPA, RADAR , MEREMETA na sasa IPTL Escrow .
Waliofaidika hawawezi kujiumbua wakati ripoti ziko mikononi mwao.
 
panya watakiona vp,ikiwa huyo paka hana meno wala kucha.....
 
Ethics za kazi ya ukaguzi inazuia matamko ya kisiasa kama alivyofanya huyu jamaa. Mbona wataalamu wetu wanakosa mwelekeo jamani????????
 
Kengemanyoya anaongea kamakakalia kigogo bana
 
Back
Top Bottom