CAG Vs SPIKA

Ngamanya Kitangalala

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
501
1,214
Binafsi pamoja na uelewa wangu mdogo katika sheria, ili niweze kulielewa vema sakata hili ninesoma vitu vifuatavyo, (nitaambatanisha humu na wenzangu mpitie)

1.katiba ya jamhuri wa muungano wa Tanzania ya mwaka 1977( The constitution of United Republic of Tanzania of 1977)

2.Sheria ya ukaguzi wa mahesabu ya umma ya mwaka 2008( The Public Audit Act 2008)

3.Sheria ya Haki, Kinga na madaraka ya bunge ya mwaka 1988 na marekebisho yake ya 2004( The parlimentary Immunities, powers and privileges act of 1988)

Sasa naomba turudi kwenye sakata letu

Ofisi ya Mdhibiti na mkaguzi wa hesabu wa serikali imeanzishwa kikatiba kwenye sura ya saba, ibara ya 143, na katika ibara hiyo kwa pamoja na sheria ya ukaguzi wa hesabu za umma kifungu cha 9,10,11,12,13 &14 vimeeleza kwa ufasaha kabisa, kazi, majukumu, madaraka, mamlaka na kinga za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serkali( Controller and auditor General)

Naomba kunukuu katiba, sura ya saba, ibara ya 143 inasema " katika kutekeleza madaraka yake,kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya 2,3, na 4 ya ibara hii, mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali,hatarazimika kufuata amri au maagizo ya mtu yeyoteau idara yeyote ya serikali lakini maelezo hayo ya ibara hii, hayatazuia mahakama nayo kutumia madaraka yake katika kuchunguza kama mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali, amekeleza masharti ya katiba hii katika kutekeleza madaraka yake"

Maana yake nini?

Katka kutekeleza majukumu na madaraka yake kama mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, hakuna chombo chochote chenye mamlaka ya kuingilia, kutoa maagizo au kuchunguza isipokuwa mahakama tu

Kwa mantiki hiyo, CAG ana kinga(immunity) ya kutokuingiliwa na mamlaka nyingine, isipokuwa mahakama pale tu anapotekeleza madaraka na mamlaka yake ya kikatiba na sheria

Kwa maana hiyo anapokuwa nje ya utekelezaji wa mamlaka na madaraka yake, hana kinga hiyo, mfano anapofanya kosa la jinai, anapotoa maneno ya kashfa au dharau juu ya taasisi nyingine au anapokataa kutii wito kutoka katika mamlaka nyingine hana kinga hiyo

Sasa swali la msingi hapa la kujiuliza, CAG alipokuwa anatoa maoni yake juu ya utekelezaji wa mapendekezo yake, alikuwa anatekeleza mamlaka na madaraka yake ya kikatiba na sheria????

Jibu, hapana,

Kwa nini?
Someni sheia ya Ukaguzi wa hesabu za umma ya mwaka 2008, kifungu cha 9,10,11,12, & 13 kimeeleza fika kazi, mamlaka na madaraka ya CAG, hakuna mahala CAG amepewa kufanya tathmini ya namna gani mapendekezo yake yanatekelezwa na serikali

Tuje kwenye issue ya Spika kuagiza CAG aletwe mbele ya kamati Haki, kinga na maadili ya bunge

Swali tunalopaswa kujiuliza hapa? Je Spika anayo mamlaka hayo???

Jibu, ndiyo, Spika anayo mamlaka ya kumuita mtu yeyote mbele ya kamati zake, lakini sio kama mtuhumiwa bali kama shahidi, someni sheria ya Haki, kinga na madaraka ya bunge ya mwaka 1988 kifungu cha 13, na nukuu"The assembly, any standing committee or any sessional committee, may subject to provisions of section 18 and section 20 of this act, order any person to attend before the assembly or before such committee, and to give evidence or to produce any documents in the possession or under control of such person"

Swali lingine linakuja hapa

Je Spika amemuita CAG kama mtuhumiwa au kama shahidi???

Jibu, Spika amemuita CAG kuja mbele ya kamati ya maadili ya bunge, kama shahidi wa kuja kutoa ushahidi wake, ni namna gani anaona bunge ni dhaifu na si kama mtuhumiwa, lakini akaenda mbele zaidi, kwa kusema, kama CAG hatotii wito wake(Bunge) atapelekwa mbele ya kamati kwa pingu

Swali lingine linakuja hapa

Je Spika anayo madaraka ya kuamuru mtu apelekwe kwa nguvu mbele ya kamati?

Jibu, ndiyo, Spika anayo mamlaka ya kuamuru mtu aletwe mbele ya kamati kwa nguvu endapo atotii wito wa kamati, Someni tena sheria ya Haki, Kinga na madaraka ya bunge ya mwaka 1988 kifungu cha 15

Kwa hiyo kwa ufafanuzi wangu huo, binafsi mimi kama Ngamanya Kitangalala, naamini hatua aliyochukua Spika ya kumwita CAG aje mbele ya kamati na kutoa ushahidi wake ni kwa namna gani bunge letu ni dhaifu yuko sahihi kabisa

Kitu ambacho sina uhakika nacho, na hatua zipi Spika, kwa maana ya Bunge litachukua dhidi ya CAG ikibainika alikiuka maadili ya kazi zake

Naomba kuishia hapo, nakaribisha mjadala wa hoja na si kejeli na matusi
Asanteh

Ngamanya Kitangalala
 
Back
Top Bottom