CAG: Sh. Bilioni 20.9 za chanjo zafujwa na kuliwa.

shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
8,106
3,967
Ripoti ya Mkaguzi mkuu wa fedha za serikali ametoa ripoti yake kuhusu matumizi katika Wizara ya Afya ya mwaka fedha wa 2015/16 ambapo billioni 20.9 zilitolewa.
Katika ripoti yake amebaini ufisadi mkubwa wa MABILIONI ya fedha ambazo zilikuwa zitumiwe katika CHANJO za SURUA- RUBELLA.

CAG Ameshauri kufanyika uchunguzi wa KIJINAI kwa wote waliohusika ili WAREJESHE fedha hizo serikalini.
Halmashauri za wilaya na za Waganga wakuu wa Mikoa walihusika pakubwa ikiwa ni pamoja na watu wengine WIZARANI.

My take: TAKUKURU/DPP/JUDICIARY-Mahakama. Jamani lisaidieni Taifa hili.

Hawa watu waliokula fedha hii bila kujali maisha ya WATOTO ni WAUWAJI wasijali taif na ni WEZI.

Watanzania wanangoja kuona the WHEEL of Justice likianza KUZUNGUKA pasipo kujali cheo cha mtu.
Hapo ndo tutakuwa na imani katika vyombo vya kupambana na rushwa.
 
Kipindi cha uchaguzi kile Chama hulazimisha kipewe hela,na sehemu nyingi ambazo waligoma kutoa,walifyekwa,wakuu wake wote wako benchi au wametimuliwa

Ogopa sana kukaa karibu na tajiri anayekaribia kufilisika,ni rahisi mno kukutoa kafara ili aendelee kuwa na mali
 
Eh Mwenyezi Mungu tusaidie
Mauaji kwa watoto hayo, wizi bila kujali utu halafu wachome watoto kwa chanjo feki
 
Haya mapigo yatakoma siku CCM ikitoka madarakani......huu upigaji ni balsa, nilisoma hiyo habari Mwananchi nikabaki sina la kusema.
 
DMOs,maafisa Afya wanapiga sana hela hizi!Tena wangeenda nyuma kidogo kuna pesa za ujenzi wa zahanati na ununuzi wa vifaa vyake zilipigwa na ma dmo na wafamasia kwa wakisaidiwa na wahasibu.Ulikuwa unakuta mfamasia ana miaka miwili tu kazini lakini ameshafungua famasi zaidi ya moja zenye milioni zaidi ya 80 kila moja,ana nyumba,gari na matanuzi kwenye hotel za maana.Ila Mara nyingi ukiona mbwa anabweka sana,ujue ni mwoga!
 
Chain iko hivii...
1.Waratibu wa chanjo taifa
2.RMOs
3.Makatibu wa afya mikoa
4.Maafisa Afya mikoa
5.MDOs
6.Makatibu wa Afya wiliya
7.Maafisa Afya wa wilaya

Hayo ndio mafisadi yaliyosababisha watoto kufa kwa sababu ya kukisa chanjo, wakamatwe wafunge tu.
 
Hii ripoti ipo kwenye tovuti ya NAO, naona wengine wanaisoma wakikutana na kitu kikawakuna wanaanzisha uzi kwenye hili jukwaa. Sijui hii trend itaendelea hadi lini.
 
Hii nchi kumbe sio masikini kumbe kuna kundi la watu walikuwa wanaitafuna nchi ndio maana wanahaha sana kwa utawala wa huyu jamaa
 
Mpwa hatuna haja ya kutahamaki, iwapo POMBE ni ile ile kilichobadilishwa ni kifungushio, I mean KIROBA.

Na katika hawamu zote, hawamu hii ndio itapigwa hela ya wavuja jasho, kuliko hawamu zote zilizopita, maana hakuna vyombo vya habari tena, vyenye uwezo wa kutangaza tukio kama hilo (rajea kasheria ketu kale)

Yani sasa hivi CAG ndio atabaki kama mkombozi wetu katika kutupasha habari za pesa zetu, zinavyofisadiwa.
 
Ni kweli kabisa Mkuu, CAG anajitahidi sana kuweka hadhatani madudu ya kutisha kuhusu ufisadi mbali mbali Serikalini na taasisi zake lakini anadharauliwa na kupigwa vita kwa kumpa bajeti kiduchu sana hivyo kushindwa kutimiza majukumu yake na pia kupoteza wafanyakazi mahiri katika sekta ya ukaguzi wa mahesabu ambao huamua kuhamia kwa waajiri wengine.

Mpwa hatuna haja ya kutahamaki, iwapo POMBE ni ile ile kilichobadilishwa ni kifungushio, I mean KIROBA.

Na katika hawamu zote, hawamu hii ndio itapigwa hela ya wavuja jasho, kuliko hawamu zote zilizopita, maana hakuna vyombo vya habari tena, vyenye uwezo wa kutangaza tukio kama hilo (rajea kasheria ketu kale)

Yani sasa hivi CAG ndio atabaki kama mkombozi wetu katika kutupasha habari za pesa zetu, zinavyofisadiwa.
 
Hivi huyu Dereva wa Lori hajaisoma hii ripoti? Kumbe nae ni wale wale mdebwedo
 
Kipindi cha uchaguzi kile Chama hulazimisha kipewe hela,na sehemu nyingi ambazo waligoma kutoa,walifyekwa,wakuu wake wote wako benchi au wametimuliwa

Ogopa sana kukaa karibu na tajiri anayekaribia kufilisika,ni rahisi mno kukutoa kafara ili aendelee kuwa na mali

Hizo Fedha haiwezekani zote zilitoka kwny Quarter ya Kwanza ya Mwaka wa Fedha. Kiasi kikubwa kilitoka baada ya Magu kuwa Rais sio kila kitu kusingizia Uchaguzi
 
Back
Top Bottom