CAG: Serikali Yashusha Deni la Taifa

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
13,497
29,833
Anyway, hapo juu nimeongeza chumvi, ndimu, pilipili, kachumbari na mbilimbi kwa mbaaaaali manake nimesikia Dar kuna bonge la pupwe!!

CAG hajasema serikali imedanganya deni la taifa bali Serikali Yashusha Deni la Taifa!!

Hivi si ndo kudanganya kwenyewe huko; au?! Hebu msomeni CAG kwenye ripoti yake kisha ndipo nihukumiwe:
Kushushwa Kiwango Deni la Taifa kwa kiasi cha Shilingi bilioni 4,588.39

Mapitio yangu ya mchanganuo wa Deni la Taifa yalibaini kwamba, kiwango cha deni la taifa kilifikia Shilingi billion 46, 081.43 kufikia tarehe 30 Juni, 2017. Kiwango hiki hakijumuishi madeni ya Shilingi bilioni 4,588.39 ikiwa ni madeni ya mifuko ya pensheni kiasi cha Shilingi bilioni 4,421.75 na dhamana zilizokiukwa masharti kiasi cha Shilingi bilioni 166.64 chini ya Idara ya Msajili wa Hazina.

Hapo juu ni Ripoti Kuu (Serikali Kuu) ya CAG
inayopatikana Ukurasa wa 104 - 105.

Hapo utaona CAG anataja kiwango cha deni la taifa ambacho ni takribani Shilingi trilioni 4.6 ambacho serikali imekwepa ku-declare.

Mbaya zaidi, kati ya hizo, takribani Shilingi Trilioni 4.4 ni pesa za wavuja jasho... pesa za wafanyakazi! Pesa za wale wale wanaoamka alfajiri na kwenda kugombea madaladala ili wawahi kazini lakini serikali ni kama inasema "pesa zenu tumechukua na kuzitumia tumezitumia; lakini hamtudai!" Kisa?

CAG anaendelea:
Mapitio yangu zaidi kuhusu msingi wa kukataliwa yalibaini kwamba, baadhi ya madeni hayo, kimsingi, hayakukataliwa; bali kulikosekana nyaraka za kuthibitisha wakati wa uhakiki; na baadhi yamekataliwa kutokana na makosa ya kiufundi. Kwa mfano, nimeona mfano ambao mkopo ulikataliwa kwa sababu tu mkopeshaji (NSSF) alielekeza fedha kwenye akaunti ya benki aliyoelekezwa na wizara mama, ambayo kimsingi ni akaunti ya MkopajI (serikali) badala ya ile aliyoelekezwa na Mlipaji Mkuu wa Serikali awali.

Sasa kama huko sio KUDANGANYA kiwango halisi cha Deni la Taifa kumbe tuite nini?!

Yaani, nimekukopesha 1M na umezitumia lakini unaenda kwa demu wako unasema unadaiwa Laki 7 eti kisa tu, baada ya kukupa laki 3, nikasaini lakini chini ya sahihi yangu sikupiga mstari na kwahiyo hilo deni la laki 3 hulitambui... ebo!!

Wakati unazitumia hukuona mapungufu lakini katika kumwambia demu wako kwamba unadaiwa ndo unaona mapungufu!!

That said, kwa kutumia ripoti hiyo hiyo ya CAG kwamba:
Mapitio yangu ya mchanganuo wa Deni la Taifa yalibaini kwamba, kiwango cha deni la taifa kilifikia Shilingi billion 46, 081.43 kufikia tarehe 30 Juni, 2017.

Na kujumuisha taarifa kwamba:
Kushushwa Kiwango Deni la Taifa kwa kiasi cha Sh. Bilioni 4,588.39

Kwa taarifa hizo mbili, utaona kiwango SAHIHI cha Deni la Taifa ni Shilingi bilioni (46, 081.43 + 4, 588.39) = 50,669.82 ambalo ni takribani Shilingi Trilioni 51 na sio Shilingi Trilioni 46.

Aidha, ripoti hiyo hiyo ya CAG inasema GDP yetu ni Shilingi bilioni 106,867 na kwahiyo Deni la Taifa ni 47.4% ya Pato la Taifa na sio 41% kama tulivyokuwa tumeambiwa hapo awali!

Aidha, ikumbukwe kwamba, deni hilo ni hadi June 2017. Kwa maana nyingine, kuna uwezekano mkubwa sana kwamba hivi sasa kiwango cha deni halisi la taifa kimezidi nusu ya pato la taifa!
 
Subiri waje ndio utajua Tanzania tuna vilaza wengi Kama kina JINGALAO na washirika wake. Ila nina imani itafika time watakosa Cha kutetea na watapanda na ID mpya humu. Kwani kina LIZABONI yuko wapi siku hizi? Kaona Mambo si Mambo
 
mtoto akililia wembe mpe ,lakini kwa watoto wa siku hizi hata wembe ukimkata atasema hujamkata huku akificha vidole na machoni ukimuangalia utaona anatamani kulia lakini kajikaza
 
Subiri waje ndio utajua Tanzania tuna vilaza wengi Kama kina JINGALAO na washirika wake. Ila nina imani itafika time watakosa Cha kutetea na watapanda na ID mpya humu. Kwani kina LIZABONI yuko wapi siku hizi? Kaona Mambo si Mambo
CKU JIZI ANAJIITA NIBOZALI
 
Subiri waje ndio utajua Tanzania tuna vilaza wengi Kama kina JINGALAO na washirika wake. Ila nina imani itafika time watakosa Cha kutetea na watapanda na ID mpya humu. Kwani kina LIZABONI yuko wapi siku hizi? Kaona Mambo si Mambo
CKU HIZI ANAJIITA NIBOZALI
 
Subiri waje ndio utajua Tanzania tuna vilaza wengi Kama kina JINGALAO na washirika wake. Ila nina imani itafika time watakosa Cha kutetea na watapanda na ID mpya humu. Kwani kina LIZABONI yuko wapi siku hizi? Kaona Mambo si Mambo
Po pote ulipo Lizaboni njoo pande hizi utoe utetezi kwa serikali!!
 
Anyway, hapo juu nimeongeza chumvi, ndimu, pilipili, kachumbari na mbilimbi kwa mbaaaaali manake nimesikia Dar kuna bonge la pupwe!!

CAG hajasema serikali imedanganya deni la taifa bali Serikali Yashusha Deni la Taifa!!

Hivi si ndo kudanganya kwenyewe huko; au?! Hebu msomeni CAG kwenye ripoti yake kisha ndipo nihukumiwe:

Hapo juu ni Ripoti Kuu (Serikali Kuu) ya CAG
inayopatikana Ukurasa wa 104 - 105.

Hapo utaona CAG anataja kiwango cha deni la taifa ambacho ni takribani Shilingi trilioni 4.6 ambacho serikali imekwepa ku-declare.

Mbaya zaidi, kati ya hizo, takribani Shilingi Trilioni 4.4 ni pesa za wavuja jasho... pesa za wafanyakazi! Pesa za wale wale wanaoamka alfajiri na kwenda kugombea madaladala ili wawahi kazini lakini serikali ni kama inasema "pesa zenu tumechukua na kuzitumia tumezitumia; lakini hamtudai!" Kisa?

CAG anaendelea:

Sasa kama huko sio KUDANGANYA kiwango halisi cha Deni la Taifa kumbe tuite nini?!

Yaani, nimekukopesha 1M na umezitumia lakini unaenda kwa demu wako unasema unadaiwa Laki 7 eti kisa tu, baada ya kukupa laki 3, nikasaini lakini chini ya sahihi yangu sikupiga mstari na kwahiyo hilo deni la laki 3 hulitambui... ebo!!

Wakati unazitumia hukuona mapungufu lakini katika kumwambia demu wako kwamba unadaiwa ndo unaona mapungufu!!

That said, kwa kutumia ripoti hiyo hiyo ya CAG kwamba:

Na kujumuisha taarifa kwamba:

Kwa taarifa hizo mbili, utaona kiwango SAHIHI cha Deni la Taifa ni Shilingi bilioni (46, 081.43 + 4, 588.39) = 50,669.82 ambalo ni takribani Shilingi Trilioni 51 na sio Shilingi Trilioni 46.

Aidha, ripoti hiyo hiyo ya CAG inasema GDP yetu ni Shilingi bilioni 106,867 na kwahiyo Deni la Taifa ni 47.4% ya Pato la Taifa na sio 41% kama tulivyokuwa tumeambiwa hapo awali!

Aidha, ikumbukwe kwamba, deni hilo ni hadi June 2017. Kwa maana nyingine, kuna uwezekano mkubwa sana kwamba hivi sasa kiwango cha deni halisi la taifa kimezidi nusu ya pato la taifa!
Nchi yangu...............
Mimi...................
Ndio maneno ya siku hizi hayo.
 
Arekebishe Katiba , liwe jeshi LA mtu mmoja . Kwa katiba hii anatuchanganya sana. Naumbumbuka Dictator Amini Uganda aliwahi muua kwa bastola waziri wake wa fedha baada ya kusema ukweli hali ya hazina sio nzuri.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
"ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu yafutwa, shughuli zake kuhamishiwa hazina"
"kuanzia mwaka wa fedha 2017/2018 report itakuwa inakabidhiwa kwa Rais na kujadiliwa ndani ya vikao vya baraza la Mawaziri"
 
Back
Top Bottom