CAG Profesa Assad asema moto ni uleule

CAG Profesa Assad asema moto ni uleule

Kama akiweza kulizuia hili atakuwa katusaidia sana make wanasiasa wetu wanafanya mambo ya ajabu sana wanaonea watu kwa chuki zao kisa tu biashara zao zimebanwa kwenye wizara au idara fulani.
 
CAG anateuliwa na rais halafu anaenda kukagua mahesabu ya ma Escrow ambayo yamepitishwa na rais.

Halafu anatuzuga na habari za "conflict of interest".

Hivi huyu CAG akienda sehemu kukagua na kukuta Kikwete kachota hela anaweza kumtoa nishai Kikwete? Mtu aliyemteua?

Conflict of interest my foot.
Kinachozingatiwa ni taluma siyo undugu wala kujuana ukifuata hayo unamkagua mtu yeyote.
 
Kinachozingatiwa ni taluma siyo undugu wala kujuana ukifuata hayo unamkagua mtu yeyote.

Kaongelea suala la conflict of interest na kufuata taaluma, si siasa.

Alivyoteuliwa yeye tu ni kisiasa. He is a presidential appointee. Tayari kama kuna zali linalomhusu rais, tushaanza kumuondolea uhuru wa kumnanga rais ipasavyo, kwa sababu kama a presidential appointee atamuonea haya.

Katika katiba mpya moja ya vitu vinavyotakiwa kufanywa ni kupunguza madaraka ya rais, ikiwa ni pamoja ya kupunguza hawa presidential appointees.

Hivi hamna namna nyingine ya kumpata CAG mpaka awe presidential appointee?

Na kama CAG ni presidential appointee, ana moral authority gani ya kukemea kuchanganya siasa na taaluma wakati uteuzi wake yeye mwenyewe ni wa kisiasa?
 
Huyo CAG anaweza kuwa mtu mzuri tu. Tena mwenye mapenzi sana na nchi yake. Lakni kwa kawaida mtu mwadilifu akianza kuishi na wachafu atachafuka tu. Biblia inasema na hata Quarun inasema kaa mbali na wasio amini au wapagani. Huwezi kuendelea na kile unachoamini tena. Huyu mzee uislam wake safi ndio ushaakimbia kwa kukubali ofa y kikwete.
System nzima ni hovyo. Hatuwezi kumlaumu raisi moja kwa moja laknj hataki kuboresha hilo hitilafu na migongano ya katiba yetu. Lazima professionalism iwe mbali na siasa. Period. Hatutaki mawaziri wawe wabunge. Tulisema hilo. Jingwa kubwa Pinda akasema hapana haiwezekani. Je tutabaki kusema rais ana nia njema na nchi? Lah!
 
Moto ni ule ule
images(159).jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
assad+px.jpg

Rais Jakaya Kikwete akibadilishana mawazo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Musa Assad (kulia) baada ya kumwapisha Ikulu Dar es Salaam jana. Katikati ni Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal.

Dar es Salaam. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mpya, Profesa Mussa Assad amesema ataanza kazi kwa moto uleule ulioachwa na mtangulizi wake, Ludovick Utouh aliyestaafu.

Akizungumza jana mara baada ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu, Profesa Assad aliyeteuliwa Novemba 5 kushika wadhifa huo alisema: "Ninasubiri niingie ofisini nianze kazi… nitaendeleza yote yaliyoachwa na mwenzangu, sitatoka nje ya mstari."

Profesa Assad alisema yuko tayari kusimamia utendaji kazi wa kisasa kwa kusimamia misingi ya ofisi yake, ili kulinda hadhi na heshima aliyopewa na Rais katika uteuzi huo.

Kuhusu Ripoti ya Akaunti ya Escrow, Profesa Asaad alisema anasubiri kukabidhiwa rasmi taarifa hiyo na maagizo yote yaliyotolewa na Bunge kwa ajili ya kutekeleza yale yaliyopo chini ya ofisi yake na kuendeleza yale ambayo yalishaanza kutekelezwa.

Alisema moja ya mambo ambayo atayafanyia tathmini na kupatia majibu ni kutotajwa moja kwa moja katika Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kama fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa kwa pamoja na Tanesco na IPTL ni za umma au vinginevyo.

Utoh anena

Akizungumza katika hafla hiyo, Utouh alisema kuwa amemkabidhi Profesa Asaad ofisi yenye watendaji wanaofanya kazi kwa ari na ufanisi katika kutekeleza majukumu yao.Alisema amefurahishwa na uteuzi wake na kusema anaamini ataendeleza uwajibikaji na umadhubuti wa ofisi hiyo kwa manufaa ya Taifa.

Utouh alimkabidhi Profesa Asaad mwongozo maalumu wenye kurasa 78 na kueleza kwamba utampa mwelekeo wa namna ofisi hiyo ilivyo na iwapo kuna upungufu yuko tayari kutoa ushirikiano.

Spika Makinda

Akimzungumzia Profesa Asaad, Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema mtikisiko uliolikumba Taifa kutokana na Kashfa ya Escrow umelifanya lijenge misingi mizuri zaidi ya kiutendaji na uwajibikaji katika kuhakikisha matumizi mazuri ya fedha za umma.

Alisema anaamini CAG mpya ataingia na mfumo wa kisasa zaidi na kusaidia kuweka miundo bora zaidi ya kuhakikisha kunakuwa na nidhamu ya hali ya juu katika kusimamia mapato na matumizi ya Serikali.

Chanzo: Mwananchi
Mengi yapo nyuma
 
Back
Top Bottom