CAG Profesa Assad asema moto ni uleule

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,366
2,000

Rais Jakaya Kikwete akibadilishana mawazo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Musa Assad (kulia) baada ya kumwapisha Ikulu Dar es Salaam jana. Katikati ni Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal.

Dar es Salaam. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mpya, Profesa Mussa Assad amesema ataanza kazi kwa moto uleule ulioachwa na mtangulizi wake, Ludovick Utouh aliyestaafu.

Akizungumza jana mara baada ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu, Profesa Assad aliyeteuliwa Novemba 5 kushika wadhifa huo alisema: "Ninasubiri niingie ofisini nianze kazi… nitaendeleza yote yaliyoachwa na mwenzangu, sitatoka nje ya mstari."

Profesa Assad alisema yuko tayari kusimamia utendaji kazi wa kisasa kwa kusimamia misingi ya ofisi yake, ili kulinda hadhi na heshima aliyopewa na Rais katika uteuzi huo.

Kuhusu Ripoti ya Akaunti ya Escrow, Profesa Asaad alisema anasubiri kukabidhiwa rasmi taarifa hiyo na maagizo yote yaliyotolewa na Bunge kwa ajili ya kutekeleza yale yaliyopo chini ya ofisi yake na kuendeleza yale ambayo yalishaanza kutekelezwa.

Alisema moja ya mambo ambayo atayafanyia tathmini na kupatia majibu ni kutotajwa moja kwa moja katika Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kama fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa kwa pamoja na Tanesco na IPTL ni za umma au vinginevyo.

Utoh anena

Akizungumza katika hafla hiyo, Utouh alisema kuwa amemkabidhi Profesa Asaad ofisi yenye watendaji wanaofanya kazi kwa ari na ufanisi katika kutekeleza majukumu yao.Alisema amefurahishwa na uteuzi wake na kusema anaamini ataendeleza uwajibikaji na umadhubuti wa ofisi hiyo kwa manufaa ya Taifa.

Utouh alimkabidhi Profesa Asaad mwongozo maalumu wenye kurasa 78 na kueleza kwamba utampa mwelekeo wa namna ofisi hiyo ilivyo na iwapo kuna upungufu yuko tayari kutoa ushirikiano.

Spika Makinda

Akimzungumzia Profesa Asaad, Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema mtikisiko uliolikumba Taifa kutokana na Kashfa ya Escrow umelifanya lijenge misingi mizuri zaidi ya kiutendaji na uwajibikaji katika kuhakikisha matumizi mazuri ya fedha za umma.

Alisema anaamini CAG mpya ataingia na mfumo wa kisasa zaidi na kusaidia kuweka miundo bora zaidi ya kuhakikisha kunakuwa na nidhamu ya hali ya juu katika kusimamia mapato na matumizi ya Serikali.

Chanzo: Mwananchi
 
Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,649
2,000
huyu kaja kuficha uvundo,hatamfikia UTUOH
Tamko lake la kwanza litamjenga au kumbomoa. Fedha ni za umma au si za umma. Kazi anayo.
Bila kufanya ukokotoaji kujua Iptl wali overcharge kiasi gani,fedha ni za TANESCO ni za umma.
 
MARKYAO

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
673
1,000

Rais Jakaya Kikwete akibadilishana mawazo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Musa Assad (kulia) baada ya kumwapisha Ikulu Dar es Salaam jana. Katikati ni Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal.

Dar es Salaam. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mpya, Profesa Mussa Assad amesema ataanza kazi kwa moto uleule ulioachwa na mtangulizi wake, Ludovick Utouh aliyestaafu.

Akizungumza jana mara baada ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu, Profesa Assad aliyeteuliwa Novemba 5 kushika wadhifa huo alisema: “Ninasubiri niingie ofisini nianze kazi… nitaendeleza yote yaliyoachwa na mwenzangu, sitatoka nje ya mstari.”

Profesa Assad alisema yuko tayari kusimamia utendaji kazi wa kisasa kwa kusimamia misingi ya ofisi yake, ili kulinda hadhi na heshima aliyopewa na Rais katika uteuzi huo.

Kuhusu Ripoti ya Akaunti ya Escrow, Profesa Asaad alisema anasubiri kukabidhiwa rasmi taarifa hiyo na maagizo yote yaliyotolewa na Bunge kwa ajili ya kutekeleza yale yaliyopo chini ya ofisi yake na kuendeleza yale ambayo yalishaanza kutekelezwa.

Alisema moja ya mambo ambayo atayafanyia tathmini na kupatia majibu ni kutotajwa moja kwa moja katika Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kama fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa kwa pamoja na Tanesco na IPTL ni za umma au vinginevyo.

Utoh anena

Akizungumza katika hafla hiyo, Utouh alisema kuwa amemkabidhi Profesa Asaad ofisi yenye watendaji wanaofanya kazi kwa ari na ufanisi katika kutekeleza majukumu yao.Alisema amefurahishwa na uteuzi wake na kusema anaamini ataendeleza uwajibikaji na umadhubuti wa ofisi hiyo kwa manufaa ya Taifa.

Utouh alimkabidhi Profesa Asaad mwongozo maalumu wenye kurasa 78 na kueleza kwamba utampa mwelekeo wa namna ofisi hiyo ilivyo na iwapo kuna upungufu yuko tayari kutoa ushirikiano.

Spika Makinda

Akimzungumzia Profesa Asaad, Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema mtikisiko uliolikumba Taifa kutokana na Kashfa ya Escrow umelifanya lijenge misingi mizuri zaidi ya kiutendaji na uwajibikaji katika kuhakikisha matumizi mazuri ya fedha za umma.

Alisema anaamini CAG mpya ataingia na mfumo wa kisasa zaidi na kusaidia kuweka miundo bora zaidi ya kuhakikisha kunakuwa na nidhamu ya hali ya juu katika kusimamia mapato na matumizi ya Serikali.

Chanzo: Mwananchi

Hapa hamna kitu ni mambo yale yale tu. Bora hata Uhouh alikuwa kwa kiasi kurevieal mambo akijiamini na akafanikiwa.

Hamna Professor aliyefanya vyema katika nafasi hizi za kuteuliwa a chilia mbali za kuchagua. wote wameprove failure, wachumia tumbo waoga, wasio na maamuzi, wasio na maono na wavivu kiutendaji. Mifano michache ni hii

1. Professor Jumanne Maghembe na domo lake la kusema by anavyochemsha wizara ya maji! Mnbali na misaada na mikopo serikali imepata kwa sector ya maji bado mchwa wa CCM wako wanatafura professor anapiga domo tu bila kuleta mipango sanisfu ya kumaliza tatizo la maji mijini na vijijini. uwezo mdogo wa kushauri serikali na kusimamia funds za maji zifanye kaze husika.

2. Professor Benno Ndulu! Mipango mibovu ya kifedha kwa Tanzania, mfumuko wa bay, High interest rates kwa mabank , fedha haram na utatishaji wake e.g. FBME. Matumizi ya US dolla Tanzania kwa huduma zinazotolewa Tanzania. Fedha nyingi feki kwenye mzunguko, Noti dhaifu sana za bongo, cash kuhamishwiwa nje kupitia bank zetu nas mengineyo mengi.

3. Professor Mark mwandosya nadani mnafahamu na mnamuona wenyewe utumbo anaooungea publically. Kama vile hakwenda shule. Anabaki tu akitetea mabo ya kijinga mpaka inakuwa kero kwa jamii.

4. Professor Muhongo nadhanai mmemsikia wenyewe na dahrau zake na kijeli kwa Tanzania. Nakumbuka alivyotaka kujilinda wakati wa bunge la budget kwa kutumia gossips kumnyamazisha Ole sendeka baada ya kusema itabidi tuite CV za wabunge wengine kwani kuna waliopata zero form six akimmaanisha O..S. kama professor haya manaeneo sio!!

5. Professor Shivji alivyoanza kutetea Katiba ya CCM na serikali mbili na kusahao aliyokwisha kuyaandika ni dhihaka ya maprof wetu.

6. Professor Mkulo alivyockemsha wizara ya Fedha

7. Professor Anna tibaijuka na failure kwenye ardhi na makazi

8. Professor Mosolla ndio kabisaa mpaka anafika mahali akabaki na kaubunge tu.

9. Na kwa sasa Professor JK wa Kichina kwenye kilimo!!

Hawa ni baadhi tu muone jinsi maprofessor walivyo na utendaji mbovu. waachwe kwenye taasisi za elimu na sio kwenye huduma muhimu zinazohitaji wawajibikaji.

'Nawasilisha
 
Songoro

JF-Expert Member
May 27, 2009
4,126
0
let us wait and see
Sio tu CAG mpya bali hata PAC mpya haitokuwa na makali kwa kuwa hatutakuwa tena na Prof Kikwete aliewapa sio tu uhuru bali pia uthubutu! Kamati ya PAC na CAG zilikuwepo hata kabla ya 2005 lakini hazikuonesha makali yake kwa kuwa hapakuwa na utayari wa dola, kabla ya Prof kuwa Rais nani angethubutu kuleta ripoti ya CAG Bungeni? Bunge halikuwa na historia ya kuagiza uchunguzi, for that case utendaji na uwajibikaji wa Prof Sssad utategemea uungaji na utayari wa Head of State kama akiwa kama Prof JK basi nae anaweza kuwa mzuri otherwise ofisi yaCAG itakuwa dormant kama ilivokiwa kabla ya Kutawazwa Ndugu Kikwete.
 
Kitaja

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
2,818
2,000
Mkulo naye profesa? Hapana nakataa labda uprofeseri wa kichina kama mkulu
 
Ivonya-Ngia

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
703
195
6. Professor Mkulo alivyockemsha wizara ya Fedha
Huyo bwana hajawahi kuwa professor wa kitaaluma labda kama alijitunuku like yule mbunge mganga wa kienyeji.
 
Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
25,515
2,000
Hapa hamna kitu ni mambo yale yale tu. Bora hata Uhouh alikuwa kwa kiasi kurevieal mambo akijiamini na akafanikiwa.

Hamna Professor aliyefanya vyema katika nafasi hizi za kuteuliwa a chilia mbali za kuchagua. wote wameprove failure, wachumia tumbo waoga, wasio na maamuzi, wasio na maono na wavivu kiutendaji. Mifano michache ni hii

1. Professor Jumanne Maghembe na domo lake la kusema by anavyochemsha wizara ya maji! Mnbali na misaada na mikopo serikali imepata kwa sector ya maji bado mchwa wa CCM wako wanatafura professor anapiga domo tu bila kuleta mipango sanisfu ya kumaliza tatizo la maji mijini na vijijini. uwezo mdogo wa kushauri serikali na kusimamia funds za maji zifanye kaze husika.

2. Professor Benno Ndulu! Mipango mibovu ya kifedha kwa Tanzania, mfumuko wa bay, High interest rates kwa mabank , fedha haram na utatishaji wake e.g. FBME. Matumizi ya US dolla Tanzania kwa huduma zinazotolewa Tanzania. Fedha nyingi feki kwenye mzunguko, Noti dhaifu sana za bongo, cash kuhamishwiwa nje kupitia bank zetu nas mengineyo mengi.

3. Professor Mark mwandosya nadani mnafahamu na mnamuona wenyewe utumbo anaooungea publically. Kama vile hakwenda shule. Anabaki tu akitetea mabo ya kijinga mpaka inakuwa kero kwa jamii.

4. Professor Muhongo nadhanai mmemsikia wenyewe na dahrau zake na kijeli kwa Tanzania. Nakumbuka alivyotaka kujilinda wakati wa bunge la budget kwa kutumia gossips kumnyamazisha Ole sendeka baada ya kusema itabidi tuite CV za wabunge wengine kwani kuna waliopata zero form six akimmaanisha O..S. kama professor haya manaeneo sio!!

5. Professor Shivji alivyoanza kutetea Katiba ya CCM na serikali mbili na kusahao aliyokwisha kuyaandika ni dhihaka ya maprof wetu.

6. Professor Mkulo alivyockemsha wizara ya Fedha

7. Professor Anna tibaijuka na failure kwenye ardhi na makazi

8. Professor Mosolla ndio kabisaa mpaka anafika mahali akabaki na kaubunge tu.

9. Na kwa sasa Professor JK wa Kichina kwenye kilimo!!

Hawa ni baadhi tu muone jinsi maprofessor walivyo na utendaji mbovu. waachwe kwenye taasisi za elimu na sio kwenye huduma muhimu zinazohitaji wawajibikaji.

'Nawasilisha
Kielimu Mimi basi, sisomi tena
 
jzm-teak

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
1,628
1,195
Mteule mpya wa HESABU ZA SERIKALI(CAG) Prof Assaad kasema lazima siasa itenganishwe na biashara, ili watu waweze kufanya maamuzi bila kuangalia 'INTEREST' zao wenyewe!, hii itasaidia kuondoa mgongano wa kimslahi 'conflict of interest' kwenye mambo ya kitaifa. hapa alimaanisha kuwa wanasiasa wetu wasiwe wachoyo wa kutanguliza ubinafsi wanapofanya maamuzi kwenye mambo ya wananchi, kwahiyo hapatakuwepo na taarifa chafu kama za ESCROW kama watu hawatakuwa na tamaa za kiwiziwizi na kibinafsibinafsi!
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
52,913

CAG anateuliwa na rais halafu anaenda kukagua mahesabu ya ma Escrow ambayo yamepitishwa na rais.

Halafu anatuzuga na habari za "conflict of interest".

Hivi huyu CAG akienda sehemu kukagua na kukuta Kikwete kachota hela anaweza kumtoa nishai Kikwete? Mtu aliyemteua?

Conflict of interest my foot.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom