Baada ya CAG kuachia ripoti yake, kwa kiasi kikubwa imeitikisa serikali na kwa mara ya kwanza kulazimisha mawaziri kadhaa wakijipanga zamu kujibu hoja, huku baadhi ya wanachama wa chama tawala wakionyesha kukerwa na watu wanaoichambua ripoti hiyo hasa kipengere maarufu cha 1.5T
Kutokana na tafsiri ya haraka haraka kwamba huenda hii ripoti ikatumiwa na watu wanaopenda kuchokonoa mwenendo wa serikali kutumia muda mwingi kuikosoa (serikali) badala ya kuchapa kazi ili kuendana na mfumuko wa viwanda, je, kuna umuhimu wa kuzuia utoaji wa ripoti hizi zinazokula muda wa kuzichambua, pengine hadi mwaka wa uchaguzi 2020?
Nauliza tu kama umuhimu upo, maana umuhimu wa muda katika kuutumia kuchapa kazi huo upo dhahiri