CAG mstaafu Uttoh amesema si sawa mawaziri kujibu hoja za Ripoti ya ukaguzi wa CAG

Kusema ukweli hii serikali imeoza na inadharau sana haki ya ofisi zingine na kujiona wao ndio wenye haki za nchi hii kufanya lolote watakalo na hakuja wa kuwaadhibu.

Wanachokifanya mawaziri ni kumjibu CAG kwa madudu waliyoyaganya kwa serikali hii iliyodanganya umma kuwa inapambana na ufisadi kumbe ndio mafisadi makubwa.

Imekuwa sio serikali ya wanyonge bali serikali ya kumuuwa kabisa anayeitwa mnyonge. Maana hawa jamaa ni zaidi ya panya na mchwa.

Mbona serikali zilizopita sikuwai kusikia majibu baada ya ripoti ya cag? Wanachokipinga ni ni hasa? Hizo press kwenda kujibu kwenye media maana yake ni kumchamba cag na sio vinginevyo.

Lakini hakuna hata mmoja aliyetolea ufafanuzi pesa ya watanzania kwanini imetumika nje ya iliyo idhinishwa na bunge hakuna hata mmoja, hakuna aliyesema tril 1.5 imeenda wapi hakuna, kodi ya tra tulipigwa changa hakuna. Zaidi ya umbea tu.

Watanzania hivi hata kuibiwa tril 1.5 tupo tupo tuuuuu sie ni zaidi ya maiti.
 
nimeshangaa sana Naibu spika anasema ni hoja binafsi

Kwan kituko kama hiki kilishawahi kufanyika kwenye awamu zilizopita?
 
Nyie mnaohororoja kwamba Sheria inavunjwa ni bora mngekuwa mnatuambia kwamba ni sheria ipi inavunjwa .
 
Baada ya CAG kuachia ripoti yake, kwa kiasi kikubwa imeitikisa serikali na kwa mara ya kwanza kulazimisha mawaziri kadhaa wakijipanga zamu kujibu hoja, huku baadhi ya wanachama wa chama tawala wakionyesha kukerwa na watu wanaoichambua ripoti hiyo hasa kipengere maarufu cha 1.5T

Kutokana na tafsiri ya haraka haraka kwamba huenda hii ripoti ikatumiwa na watu wanaopenda kuchokonoa mwenendo wa serikali kutumia muda mwingi kuikosoa (serikali) badala ya kuchapa kazi ili kuendana na mfumuko wa viwanda, je, kuna umuhimu wa kuzuia utoaji wa ripoti hizi zinazokula muda wa kuzichambua, pengine hadi mwaka wa uchaguzi 2020?

Nauliza tu kama umuhimu upo, maana umuhimu wa muda katika kuutumia kuchapa kazi huo upo dhahiri
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom