CAG mstaafu Uttoh amesema si sawa mawaziri kujibu hoja za Ripoti ya ukaguzi wa CAG

Kulipa madeni ya halali siyo mbaya tofauti na awamu zilizopita walikuwa wanalipa madeni hewa!

CAG hajasema kwamba kulipa madeni ni makosa alichoshauri budget ifuatwe. Unalipa pesa yote madeni fungu la maendeleo litatoka wapi? Unalipa madeni kwa sifa halafu inabidi ukope tena kwa sana kwa kuwa kuna vitu lazima tu vifanye na ili vifanye inabidi ukope maana pesa yote umelipia madeni. Waziri wa pesa ninamheshimu sana ila nafasi aliyonayo inampwaya dalili ni mambo kama haya.
 
Hiyo sheria inayokataza Mawaziri kufanya hivyo ni yakipuuzi na inatakiwa irekebishwe haraka sana. Ripoti ya CAG inatakiwa iwe wazi kwa wananchi wote na Mawazi wanafanya vizuri kuwa wazi kwa wananchi wote. Wananchi ndio mabosi wa serikali na huyo CAG, hivyo wanayo haki ya kujua kinachofanywa na serikali na watumishi wao waliowapa kazi ya kuwatumikia. Ndio maana wengine twasema Rais JPM amekuja katika wakati muafaka kwa Taifa hili. Ile mentallity ya usiri ili watu wapige kwa staili hii itakufa kifo cha mende. "Usiri wa kuficha maovu"

Mawaziri wanapata ujasiri kuyasemea hayo yaliyotolewa na CAG kwa sababu serikali iliyafanya hayo kwa "Good Faith" hivyo hakuna kinachoisuta serikali.
Ripoti ya CAG siyo siri kwani kwa mujibu wa Public Audit Act (Sheria ya Ukaguzi wa Umma) ripoti hiyo mara baada ya kuiwasilisha bungeni huwa ni public document. Mtu yeyote aweza kuitolea maoni. Kwa upande wa serikali, ni accounting officers (maafisa masuhuli) yaani makatibu wakuu ndo wanapaswa kujibu hoja za ukaguzi mbele ya kamati za bunge yaweza kuwa PAC, nk. Hawa mawaziri hawana cha kujibu kwani wao wizarani ni wasimamizi wa sera kwa kiasi kikubwa.
Aidha majibu hayo ya makatibu wakuu hupelekwa kw CAG yakionyesha ni jinsi gani walivyoyafanyia kazi mapendekezo ya CAG.
Hawa mawaziri wasiwashwewashwe ku-attack ripoti hiyo bali yafaa waongee na makatibu wakuu wao kwa lengo hilo.
Kuhusu kile ulichokitaja 'nia njema' yaani matumizi ya fedha za umma kutumika nje ya mipaka ya kibajeti, serikali yapaswa kuomba ruhusa ya bunge, kinyume na hapo ni makosa. Mfano mdogo tu hata taifa kubwa kama US labda wanataka kutekeleza mission ya kivita na kiusalama nje ya mipaka yao hupeleka ombi hilo kwa seneti ili seneti iidhinishe matumizi hayo kufanya kinyume cha hapo ni kosa hata kama ni hatua ya nia njema. Kwenye dharura zipo taratibu zake kwa mujibu wa sheria.
Mwisho ripoti ya CAG ni kioo muhimu kwa serikali kujiangalia na kuona kama inatenda katika mipaka ya kibajeti na kisheria. Pia ni kioo muhimu kwa bunge kuona kama yale yote yanayopitishwa na hicho chombo cha wananchi serikali inayatekeleza kikamilifu.
Maoni yangu:
Ni wakati muafaka kwa Serikali kutambua mchango wa wananchi katika bajeti na itamke wazi ni kiasi gani kitakusanywa kama michango kugharamia bajeti ya serikali.
Ni hayo tu.
Usiku mwema Great Thinkers.
 
Hao Mawaziri wamewazuia hao Accounting Officers kujibu hizo hoja za CAG? Kuna sheria inayo wazuia Mawaziri kuzisemea hizo hoja za CAG, tena kama zina mapungufu yaliyomfanya CAG kuomba msamaha. Kule kukosewa kwa figure iliyotamkwa na CAG hakusababisha usumbufu wowote kwa Mawaziri, serikali na hata Rais? Kwa nini tusione ndio kichochoe cha kufanya serikali kwa kupitia Mawaziri izisemee hoja za CAG?

Haya mambo yana taratibu zake. Kama ni figure au vinginevyo hayo yote yapaswa kuwa katika majibu dhidi ya hoja za CAG. Ni takwa la kisheria siyo blablabla!
 
Haya mambo yana taratibu zake. Kama ni figure au vinginevyo hayo yote yapaswa kuwa katika majibu dhidi ya hoja za CAG. Ni takwa la kisheria siyo blablabla!

Jibu maswali, Mawaziri wamekiuka sheria gani kuongelea hoja za CAG kwenye vyombo vya habari? Accounting Officers wamezuiliwa kujibu hoja za CAG kwa mujibu wa sheria? Muko na agenda gani ya siri na huyu CAG maana mnamsemea sana? Blabla imeingia je hapa?
 
pata muda jielimishe juu ya katiba na sheria ya ukaguzi wa umma ( public audit) na kanuni zake. Fahamu pia kuwa NAO ni taasisi ya umma iliyo huru na inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa katiba na sheria zilizotungwa chini yake.
 
Mimi naona uttoh ana ropoka tuu...hakuna shida yeyote mawaziri kujibu hoja za CAG na kuzitolea majibu kama walivyo fanya..... sasa kama wasipo zijibu na kufanyia kazi wakae kimya ili iweje? hakuna sehemu mawaziri wamekataa report ya CAG bali wanacho fanya ni kutoa majibu na kueleza Umma jinsi ya kuzifanyia kazi hoja za CAG na kurekebisha matatizo yaliyo ainishwa.....
Sioni tatizo... sema tatizo la nchi hii huwa ni haki kwa upande mmoja kuongea na mwingine unyamaze...hahahaha
Hakikisha uwezo wako wa kufikiri unazidi rangi ya fulana yako
 
image.jpeg

CAG mstaafu Mzee Utouh naye ameeleza waziwazi msimamo wake kuwa kinachofanyika na mawaziri wa serikali ya awamu ya tano juu ya taarifa ya CAG ni kinyume cha utaratibu na sheria.

Utouh anasema kukagua mapato na matumizi ya serikali ni kazi ya CAG,na anapaswa kuwaeleza umma wa Watanzania aliyoyaona.Na pia ni wajibu wa CAG kutengeneza hoja za ukaguzi na kutoa hoja hizo.

CAG mstaafu Utouh anasema hoja ya ukaguzi haiwezi kutolewa na mkaguliwa(serikali/mawaziri),na hata hoja ikisha tolewa na CAG,si wajibu wala utaratibu wa mawaziri kujibu report ya CAG bila CAG kuhakiki kile wanachosema hao wakaguliwa kipo sawa na kimerekebishwa?

Kuipinga au kutolea hoja ya ufafanuzi si kazi ya mawaziri bali maafisa masuhuli wa serikali ambao si mawaziri.Na ufafanuzi huo ni lazima pia ukubalike na kuchunguzwa kitaalamu na CAG ili aweze kujiridhisha kuwa hao maafisa masuhuli(ambao si Mawaziri) hicho wanachokisema kina uhakiki wa CAG.

NB:Hili suala la mawaziri kuibuka na kujibujibu,ni dalili kuwa serikali hii haitaki kukosolewa mahali ilipokosea.Mawaziri wanadiriki kuita vyombo vya habari ili tu kujisafisha wakati kisheria ni makosa.

Asiyependa kukosolewa ili ajirekebishe,ni tishio kubwa sana kwa mustakhabali wa utawala bora.
 
Attachments

  • image.jpeg
    image.jpeg
    40.3 KB · Views: 18
mimi nimepigwa na butwaa na mambo wanayofanya hawa mawaziri awamu hii
halafu kinatokea kikaragosi chenye njaa kinachoitwa kafulila(we miss you fisadi werema) kinatetea huu uhuni
 
Back
Top Bottom