CAG mstaafu Uttoh amesema si sawa mawaziri kujibu hoja za Ripoti ya ukaguzi wa CAG

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
47,553
2,000
Akizungumza na wajumbe wa kamati za fedha, CAG mstaafu ndugu Uttoh amesema si sawa mawaziri kujibu hoja za ukaguzi wa CAG hadharani bali wawaache watendaji wafanyie kazi ripoti hiyo.

Uttoh amesema kama Waziri ana jambo lililomgusa anaweza kumuandikia CAG na si kuitisha vikao na waandishi wa habari, kwanza ripoti yenyewe bado haijafanyiwa kazi na bunge na kamati zake aliongeza Uttoh.

Chanzo: ITV habari!

Habari zaidi...

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Naghenjwa Kaboyoka amekosoa utaratibu unaoendelea wa mawaziri walioguswa katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka unaoishia Juni 30, 2016 kuwa si sahihi kujibu hoja zake nje ya Bunge.

Mara baada ya uwasilishaji wa ripoti hiyo wiki hii, mawaziri mbalimbali wakiwamo Dk Phillip Mpango wa Fedha na Mipango, Selemani Jafo (Tamisemi), Dk Harrison Mwakyembe (Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo) na Charles Mwijage wa Viwanda, Biashara na Uwezeshaji, walianza kujibu hoja hizo kupitia mikutano na wanahabari.

Hata hivyo, Dk Mpango juzi alieleza sababu za wao kutoa maelezo kupitia mikutano ya waandishi wa habari akisema kisheria hawabanwi licha ya kuwa kipindi cha nyuma hawakufanya hivyo.

Dk Mpango alisema kuwa majibu hayo ni kwa mujibu wa Sheria ya Ukaguzi wa Umma, kifungu cha 418 (38) (3) inayowapa mamlaka ya kujibu hoja hizo licha ya kuwa zamani walitumia njia hiyo lakini iliishia bungeni.

“Awali Serikali ilikuwa ikijibu kwa kuweka hoja zote bungeni, mwenzetu CAG alikuwa anawasilisha bungeni kisha anawaita waandishi wa habari na kuzungumza nao, sasa Serikali imeamua kufuata njia anazotumia ili kuwapa ukweli Watanzania, tutafanya hivyo kila wakati na mawaziri wote watakuja,” alisema Dk Mpango.

Alisema majibu ya kimyakimya ambayo yalikuwa yanatolewa na Serikali yameonekana kutokuwa na tija kwa kuwa wanapomuacha CAG kuwaambia Watanzania na waandishi kutumia zaidi ya mwezi wakichambua hoja hizo, Serikali inashindwa kupeleka ukweli hata kama upo.

Akizungumza jana baada ya semina iliyotolewa na Taasisi ya Uwajibikaji ya Wajibu kwa kamati tatu za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na ile ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Kaboyoka alisema utaratibu huo wa Serikali kujibu ripoti ya CAG si sahihi na watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kesho kuelezea kwa nini hawakubaliani nao.

“Nafikiri hili tulizungumzie Jumatatu, tutalitolea maelezo maana sio sahihi kabisa. Maana nani ame-verify (amethibitisha) ndio useme hivyo. Ile ripoti ni ya kibunge na ina taratibu zake za kupokewa na kufanyiwa kazi, kwa hiyo haiwezi kujibiwa tu hivihivi,” alisema.

Awali, CAG mstaafu, Ludovick Utouh alisema mafunzo waliyoyatoa kwa wajumbe wa kamati hizo yalilenga kuwajengea uwezo wajumbe wa kuhoji juu ya ripoti za CAG.

“Tunajua ili kamati hizi zifanye kazi zake za usimamizi ipasavyo kwa niaba ya Bunge, zina umuhimu wa kuelewa fika ripoti zenyewe na ni kitu gani kinazungumzwa,” alisema.

Aprili 11, CAG Profesa Mussa Assad aliwasilisha bungeni ripoti yake inayoonekana kuwagusa kwa karibu mawaziri watano baada ya wizara zao kutajwa katika taarifa hiyo ikionyesha upungufu katika baadhi ya maeneo, aliyosema yanajenga shaka.

Maeneo mengine yaliyoonyesha shaka katika taarifa hiyo ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Taifa (NSSF), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Bandari (TPA) na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida).

Profesa Assad alisema taasisi hizo zimetumia fedha nyingi kufanya ununuzi ambao hauna viambatanisho, hivyo kutia hofu kubwa

Chanzo: Mwananchi
 
Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,571
2,000
Akizungumza na wajumbe wa kamati za fedha, CAG mstaafu ndugu Uttoh amesema si sawa mawaziri kujibu hoja za ukaguzi wa CAG hadharani bali wawaache watendaji wafanyie kazi ripoti hiyo. Uttoh amesema kama Waziri ana jambo lililomgusa anaweza kumuandikia CAG na si kuitisha vikao na waandishi wa habari, kwanza ripoti yenyewe bado haijafanyiwa kazi na bunge na kamati zake aliongeza Uttoh. Source ITV habari!
Elimu elimu elimu ni shida
 
mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,237
2,000
Akizungumza na wajumbe wa kamati za fedha, CAG mstaafu ndugu Uttoh amesema si sawa mawaziri kujibu hoja za ukaguzi wa CAG hadharani bali wawaache watendaji wafanyie kazi ripoti hiyo. Uttoh amesema kama Waziri ana jambo lililomgusa anaweza kumuandikia CAG na si kuitisha vikao na waandishi wa habari, kwanza ripoti yenyewe bado haijafanyiwa kazi na bunge na kamati zake aliongeza Uttoh. Source ITV habari!
Kwani lini ukaguzi wa CAG uliwahi kufanyiwa kazi? Mwambie afunge mdomo wake.
 
Double Elephants

JF-Expert Member
Mar 25, 2013
517
500
Akizungumza na wajumbe wa kamati za fedha, CAG mstaafu ndugu Uttoh amesema si sawa mawaziri kujibu hoja za ukaguzi wa CAG hadharani bali wawaache watendaji wafanyie kazi ripoti hiyo. Uttoh amesema kama Waziri ana jambo lililomgusa anaweza kumuandikia CAG na si kuitisha vikao na waandishi wa habari, kwanza ripoti yenyewe bado haijafanyiwa kazi na bunge na kamati zake aliongeza Uttoh. Source ITV habari!
Wao (mawaziri) wanadhani wanajibu wapinzani (wanasiasa wenzao)
 
M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,232
2,000
Akizungumza na wajumbe wa kamati za fedha, CAG mstaafu ndugu Uttoh amesema si sawa mawaziri kujibu hoja za ukaguzi wa CAG hadharani bali wawaache watendaji wafanyie kazi ripoti hiyo. Uttoh amesema kama Waziri ana jambo lililomgusa anaweza kumuandikia CAG na si kuitisha vikao na waandishi wa habari, kwanza ripoti yenyewe bado haijafanyiwa kazi na bunge na kamati zake aliongeza Uttoh. Source ITV habari!
safi.

ticha angu prof Assad amewashika watu kunako!!
 
LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
7,147
2,000
Akizungumza na wajumbe wa kamati za fedha, CAG mstaafu ndugu Uttoh amesema si sawa mawaziri kujibu hoja za ukaguzi wa CAG hadharani bali wawaache watendaji wafanyie kazi ripoti hiyo. Uttoh amesema kama Waziri ana jambo lililomgusa anaweza kumuandikia CAG na si kuitisha vikao na waandishi wa habari, kwanza ripoti yenyewe bado haijafanyiwa kazi na bunge na kamati zake aliongeza Uttoh. Source ITV habari!
Labda boss kawaambia wajibu kama anavyo fanya yeye
 
Mnyanyembe wa Mboka

JF-Expert Member
Feb 10, 2017
2,072
2,000
Utto waache hao wana weweseka usiku ... kwa dhambi walizotenda mchana ...

Watoto wa kileo wanaita kujistukia ...

Sisi kule kwetu Unyanyembe tunaita Kuyabhula!!

Yaani "kuyabhula" maana yake ni pale mchawi anapo mroga mtu akafa au akaugua, halafu siku ya msiba au wakati wa tiba mchawi anaanza kujiongelesha mwenyewe jinsi alivyofanya hilo rogo lake ...

Amini nawaambia CCM Wanayabhula!!! Mchana kweupeee sasa ivi wataanza kutajana kuhusu yule mgonjwa wetu wa Ubelgiji ...
 
CCM inaingiaje hapa?........haya ni mambo ya kitaaluma!
 
Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
48,699
2,000
Mimi naona uttoh ana ropoka tuu...hakuna shida yeyote mawaziri kujibu hoja za CAG na kuzitolea majibu kama walivyo fanya..... sasa kama wasipo zijibu na kufanyia kazi wakae kimya ili iweje? hakuna sehemu mawaziri wamekataa report ya CAG bali wanacho fanya ni kutoa majibu na kueleza Umma jinsi ya kuzifanyia kazi hoja za CAG na kurekebisha matatizo yaliyo ainishwa.....
Sioni tatizo... sema tatizo la nchi hii huwa ni haki kwa upande mmoja kuongea na mwingine unyamaze...hahahaha
 
chanaga

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
344
250
M
Utto waache hao wana weweseka usiku ... kwa dhambi walizotenda mchana ...

Watoto wa kileo wanaita kujistukia ...

Sisi kule kwetu Unyanyembe tunaita Kuyabhula!!

Yaani "kuyabhula" maana yake ni pale mchawi anapo mroga mtu akafa au akaugua, halafu siku ya msiba au wakati wa tiba mchawi anaanza kujiongelesha mwenyewe jinsi alivyofanya hilo rogo lake ...

Amini nawaambia CCM Wanayabhula!!! Mchana kweupeee sasa ivi wataanza kutajana kuhusu yule mgonjwa wetu wa Ubelgiji ...
Mimi kwetu kijijini Machame tunasema kuroroma.
 
Lusungo

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
22,490
2,000
Mimi naona uttoh ana ropoka tuu...hakuna shida yeyote mawaziri kujibu hoja za CAG na kuzitolea majibu kama walivyo fanya..... sasa kama wasipo zijibu na kufanyia kazi wakae kimya ili iweje? hakuna sehemu mawaziri wamekataa report ya CAG bali wanacho fanya ni kutoa majibu na kueleza Umma jinsi ya kuzifanyia kazi hoja za CAG na kurekebisha matatizo yaliyo ainishwa.....
Sioni tatizo... sema tatizo la nchi hii huwa ni haki kwa upande mmoja kuongea na mwingine unyamaze...hahahaha
Nani kakuleta huku? Rudi kule mkawajadili akina Nandy na vyupi vyao
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom