Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 104
Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF limefuta mashindano ya fainali za Afcon kwa vijana chini ya umri wa miaka 17
Mashindano hayo ambayo yalikuwa yafanyikie Morocco yalitarajiwa kuanza Machi 13
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania vijana chini ya miaka 17 tayari kipo Morocco na mchezo wao wa kwanza ulipangwa kuchezwa Machi 14 dhidi ya Nigeria
Kamati ya Dharura ya CAF ilikutana Jumatatu, Machi 08, 2021 huko Rabat, Morocco ili kuamua juu ya kufanyika kwa michuano ya Afcon U-17 2021
Kamati ilifahamishwa juu ya vizuizi vinavyokabiliwa na baadhi ya washiriki pamoja na nchi mwenyeji wa michuano hiyo ikiwa ni pamoja na uwepo wa janga la Korona .
Aidha kwa kuzingatia kuwa FIFA ilifuta Kombe la Dunia la Vijana chini ya miaka 17 kwahiyo hata Afcon U-17 ingeendelea wasingeweza kufuzu kombe la dunia
Kuibuka tena kwa janga la Covid19 na kuongezeka kwa vizuizi katika safari za kimataifa na kutokuwa na uhakika juu ya mabadiliko ya hali hiyo Kwa sababu hizi zote, Kamati iliamua kughairisha mashindano hayo