CAF Champions League: Simba yatinga hatua ya makundi

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Sep 11, 2020
69
104
20210106_190720.jpg

Mchezo wa michuano ya Klabu bingwa barani Afrika umepigwa hii leo katika Dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam ambapo Wekundu wa Msimbazi Simba alikua nyumbani akiikaribisha FC Platinum ya Zimbabwe ikiwa ni mchezo wa pili kati ya michezo miwili ya hatua ya mtoano.

Mechi hiyo ambayo ilipewa jina la kingereza ‘’WAR IN DAR’’ na wenyeji Simba imetoa maamuzi ya klabu ya Simba kuendelea kusonga mbele kwenye hatua ya makundi baada ya kuitandika Platinum bao 4 - 0.

Goli la kwanza la Simba limefungwa na E. Nyoni kunako dakika ya 39' kwa mkwaju wa penati na goli la pili likifungwa na S .Kapombe dakika ya 62' na goli la tatu likifungwa na J .Bocco dakika ya 90+1' na goli la kutamatisha likifungwa na C.Chama dk ya 90+5'.

Wachimba Platinum wa Zimbabwe waliingia katika mchezo huo wakiwa na faida ya goli 1-0 walilolipata katika mchezo wa kwanza uliopigwa katika Dimba la Taifa huko Zimbabwe majuma mawili yaliyopita.
 
Hongereni Mikia, Refa kawabeba. Kitu kimoja team zetu za East Africa tulikuwa tunafail ni mikakati nje ya uwanja Kama hiyo ya refa.. Hongereni kwa kulijua hilo
Refa kawabeba wapi? kama penati ya Nyoni ilikuwa halali, kwanini beki amshike Kapombe mkono ndani ya penati box? kama ile faulu ingekuwa katikati ya uwanja msingelalamika, ila kwasababu imesababisha penati ndio mnapiga kelele.

Mjifunze kupongeza panapostahili muache majungu yenu ya kibongo.
 
Back
Top Bottom