Kama unaelewa kuhusu hicho nilichokiandika juu hapo .Naitaji kujua tofauti ya cache memory na cache yenyewe maana kuna lecture ananichanganya hapa?!
Umesema kama data itakuwa mbali kutoka kwenye cache process itakuwa slow vipi kama cache size itakuwa kubwa nini kitatokeaAngalia kwenye hii graph ya memory hierarchy
Tukiongelea cache mara nyingi tunaanzia kwenye memory kweda chini, memory ni RAM, kuaccess RAM ni faster sana kuliko kuaccess harddrive, ndio maana tunapoweka data kwenye RAM tunasema tuna~cache the data ili baadaye tuziaccess faster bila kusearch kwenye harddrive.
Kwenye hiyo graph kuanzia kwenye memory kwenda chini zote ni cache, kuanzia L3 hadi L1 cache, hizo zote ziko karibu na CPU, kwa kawaida hua zina size ndogo sana kwa kua ni very expensive lakini ni very fast kuaccess data kutoka kwenye hizo cache kuliko kwenye RAM.
Unavodeclare variable kwenye program yako na kuomba data flani, CPU inaanza kutafuta hiyo data kama ipo kwenye cache ya karibu kabisa, kama ipo inaitumia hiyo data process inaitwa "cache hit", kama hamna inatokea process inaitwa "cache miss", data inaenda kutafutwa kwenye cache inayofuata, hivohivo hadi mwisho kwenye hard drive ambayo ndo slowest, data itavutwa itawekwa kwenye RAM, then cache zote as you progress kwenda chini, kuna Algorithms kama LRU, MRU na nyingine nyingi za kuhakikisha data ipi inakua cached unaweza google kuzisoma kwa undani.
Nimekupa summary, tafuta kitabu ujaribu kuelewa zaidi.
Umesema kama data itakuwa mbali kutoka kwenye cache process itakuwa slow vipi kama cache size itakuwa kubwa nini kitatokea
processor nyingi mpya za intel zinakuja na edram ambayo ni faster kuliko dram (inayotumika kwenye ram) ambayo hutumika kama vram kwa ajili ya gpu lakini pia hushare na processor kama L4 cache. ukubwa wa hii edram ni mb 128 kwa desktop na 64mb kwa laptopCache size kua kubwa vipi?
Processor nyingi za siku hizi L caches ni 2MB, hiyo ni ndogo sana kutunza program nzima, na computer nyingi za consumer RAM ni 4-8GB. Ila hard disk zinaenda hadi Terabytes, hakuna processor yenye L cache inayokaribia harddisk, wala hakuna RAM kubwa inayokaribia harddisk, zipo sababu nyingi mojawapo ni cost, kutengeneza RAM ya TB itacost pesa nyingi sana, na bado kuna technical limits.
Data kua mbali namaanisha ipo kwenye Harddrive, maana nimesema processor inavokua inatafuta data flani kuprocess inaanzia kwenye cache zilizopo karibu ambazo ndo hizo L caches, zipo ndani ya processor. Ikikosa ndipo inaenda kutafuta data kwenye RAM, ikikosa kabisa ndio inaenda kutafuta kwenye hard disk, kusoma hard disk ni very slow, yaani kuaccess RAM ni faster mara 100,000 kuliko harddisk.
ipo hivi,Kuna watu wanasema cache ni cache ni data zinazotokea WAKATI unaporun program na hizi cache zikiwa nyingu ndo kuna ccleaner inaziondoa ili program irun fastor je hii ni sawa cache memory? Na vipi kuhuusu cookies
Kuna watu wanasema cache ni cache ni data zinazotokea WAKATI unaporun program na hizi cache zikiwa nyingu ndo kuna ccleaner inaziondoa ili program irun fastor je hii ni sawa cache memory? Na vipi kuhuusu cookies