C.C.M tukiri udhaifu!!

WW Mwana CCM, jina lako ndio hapa jamvini ni moja ya kileo kinacho walevya hao mafisadi. Wakiona jina lako wanajipa moyo kuwa pamoja na upuuzi wao bado kuna watu wajiita mwana CCM. Ruzuku imepungua sijui kama mwezi ulipita kuna senti ilikuja kwako. Soma alama, achana nao changia mabadiriko.
 
Mimi ni mwanachama wa C.C.M, na kiongozi ndani ya Chama katika ngazi ya Wilaya lakini kwa mara ya kwanza nalazimika kusema ukweli, Malalamiko ya viongozi wetu ngazi ya Taifa kuhusiana na maandamano ya CHDEMA yalenge katika ukweli, tujiulize hawa watu wanalaumu nini? na wanawaambia nini wananchi? kuna ukweli ndani yake? kama hakuna ukweli kwa yale wanayoyasema tuwashitaki haraka iwezekanavyo, nahisi kama hatuwatendei haki kusema wana dhamira ya kumwaga damu, so far sijaona kosa walilofanya na ndo maana hawajapelekwa mahakamani na wakapatikana na hatia hizo, unajua kwa haya malalamiko yetu inaonyesha hatutaki changamoto za kweli na hatupendi vyama vya upinzani viwe strong. Nadhani sisi kama chama tuwe wa kweli wananchi wamechoka na maisha duni yanayozidi kuwa makali kila kukicha nadhani umefika wakati sasa viongozi wetu kutekeleza ilani zetu kwa vitendo na tusifanye siasa katika hili, tukiri katika utawala huu mambo yamekuwa tofauti sana ukilinganisha na vipindi vilivyopita kwa mfano itakuwa ni busara sana tukitumia muda mwingi kujibu maswali yanayoulizwa kwa mifano hai ya utekelezaji wa tuliyo waahidi kuliko kulaumu tu na umefika wakati sasa tuwe na ahadi chache na zinazotekelezeka ni hatari kuahidi maisha bora kwa kila mtu ilihari hata nchi tajiri zinapata changamoto kubwa sana kufikia hiyo hatua, tunatakiwa tujipange vinginevyo watatushinda kwa hoja mbele ya wananchi.

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.

Huyu hajajua ofisi za CHADEMA zilipo. Kichwa kama hiki hakifai ndani ya CCM.
 
msimlaumu...wako wengi wanaoteseka sana na hakuna wa kuwasikiliza hasa baada ya kuuza chama kwa matajiri.....

cha msingi, kama uko kwa kuwahudumia umma, hama chama...chama cha sisiemu si mama yako wala baba yako...alisema nyerere itakuwa wewe?

karibu sana chadema!
 
CCM bajaji zetu vp? wake zetu wanahangaika kwenda kujifungua. Sisi na bajaji, wabunge na milioni 90. CCM Oyeeeeeeee!!!
 
Ndugu mwana ccm inaonyesha ni jinsi gani ulivyo mdogo kimaadili kama kweli uko chamani. Tunatarajia kiongozi wa chama tumjue kwa matunda yake na si vingine. Hiyo avatar yako ni disqualification tosha! We utakuwa mpiga debe tu huko. Tutake radhi kwa kupoteza muda wetu
 
Ndugu mwana ccm inaonyesha ni jinsi gani ulivyo mdogo kimaadili kama kweli uko chamani. Tunatarajia kiongozi wa chama tumjue kwa matunda yake na si vingine. Hiyo avatar yako ni disqualification tosha! We utakuwa mpiga debe tu huko. Tutake radhi kwa kupoteza muda wetu

Mimi ni mpenzi wa Manchester, ninge mjibia hivyo
 
Jamani haya maandamano ya CDM na maneno yanayotolewa kwenye mikutano ni uchochezi ili wananchi waichukie Serikali. Uchaguzi umefanyika miezi mitatu tu iliyopita. Si msubiri basi kidogo muone kasi zaidi na ari zaidi itatoa matunda gani? Viongozi ndio kwanza wamechaguliwa (Mawaziri, wabunge n.k.). Si muwape muda basi muone watafanya nini? Kama kuna makosa ndani ya Chama na Serikali ni dhahiri yameshaonekana, kwani wao wajinga kuendelea na makosa hayo? Naamini wako katika harakati za kuyarekebisha makosa na kutafuta ufumbuzi wa kuleta mabadiliko na maendeleo kwa wananchi na kuondoa kero. Hii mikutano sioni kama inalenga kuleta maendeleo, ni kuleta uvunjaji wa amani tu. Mimi sio mwanasiasa na siko upande wowote, lakini naipenda nchi yangu na napenda Amani. Tusimuandame Rais wetu na Serikali yetu kwa mambo ambayo yako katika mchakato wa kutekelezwa. Mabomu, umeme, ukali wa maisha n.k. vinatakiwa kutafutiwa ufumbuzi, sio kuandamana na kutoa lawama tu.
Unajua wanatii maneno ambayo rais alikuwa akinena kuwa hivi vyama vya msimu, tumpongeze JK kwa kupata chama cha upnzani cha kudumu kisicho cha msimu, nae asiwe na presha maana kapata alichokuwa akiota siku za nyuma sasa hatasema tena kuwa achaneni na vyama vya musimu
 
mimi ni mwanachama wa c.c.m, na kiongozi ndani ya chama katika ngazi ya wilaya lakini kwa mara ya kwanza nalazimika kusema ukweli, malalamiko ya viongozi wetu ngazi ya taifa kuhusiana na maandamano ya chdema yalenge katika ukweli, tujiulize hawa watu wanalaumu nini? Na wanawaambia nini wananchi? Kuna ukweli ndani yake? Kama hakuna ukweli kwa yale wanayoyasema tuwashitaki haraka iwezekanavyo, nahisi kama hatuwatendei haki kusema wana dhamira ya kumwaga damu, so far sijaona kosa walilofanya na ndo maana hawajapelekwa mahakamani na wakapatikana na hatia hizo, unajua kwa haya malalamiko yetu inaonyesha hatutaki changamoto za kweli na hatupendi vyama vya upinzani viwe strong. Nadhani sisi kama chama tuwe wa kweli wananchi wamechoka na maisha duni yanayozidi kuwa makali kila kukicha nadhani umefika wakati sasa viongozi wetu kutekeleza ilani zetu kwa vitendo na tusifanye siasa katika hili, tukiri katika utawala huu mambo yamekuwa tofauti sana ukilinganisha na vipindi vilivyopita kwa mfano itakuwa ni busara sana tukitumia muda mwingi kujibu maswali yanayoulizwa kwa mifano hai ya utekelezaji wa tuliyo waahidi kuliko kulaumu tu na umefika wakati sasa tuwe na ahadi chache na zinazotekelezeka ni hatari kuahidi maisha bora kwa kila mtu ilihari hata nchi tajiri zinapata changamoto kubwa sana kufikia hiyo hatua, tunatakiwa tujipange vinginevyo watatushinda kwa hoja mbele ya wananchi.

msema kweli ni mpenzi wa mungu.
sauti pweke nyikani
 
Back
Top Bottom