Mwana CCM.
Member
- Jan 4, 2011
- 83
- 10
Mimi ni mwanachama wa C.C.M, na kiongozi ndani ya Chama katika ngazi ya Wilaya lakini kwa mara ya kwanza nalazimika kusema ukweli, Malalamiko ya viongozi wetu ngazi ya Taifa kuhusiana na maandamano ya CHDEMA yalenge katika ukweli, tujiulize hawa watu wanalaumu nini? na wanawaambia nini wananchi? kuna ukweli ndani yake? kama hakuna ukweli kwa yale wanayoyasema tuwashitaki haraka iwezekanavyo, nahisi kama hatuwatendei haki kusema wana dhamira ya kumwaga damu, so far sijaona kosa walilofanya na ndo maana hawajapelekwa mahakamani na wakapatikana na hatia hizo, unajua kwa haya malalamiko yetu inaonyesha hatutaki changamoto za kweli na hatupendi vyama vya upinzani viwe strong. Nadhani sisi kama chama tuwe wa kweli wananchi wamechoka na maisha duni yanayozidi kuwa makali kila kukicha nadhani umefika wakati sasa viongozi wetu kutekeleza ilani zetu kwa vitendo na tusifanye siasa katika hili, tukiri katika utawala huu mambo yamekuwa tofauti sana ukilinganisha na vipindi vilivyopita kwa mfano itakuwa ni busara sana tukitumia muda mwingi kujibu maswali yanayoulizwa kwa mifano hai ya utekelezaji wa tuliyo waahidi kuliko kulaumu tu na umefika wakati sasa tuwe na ahadi chache na zinazotekelezeka ni hatari kuahidi maisha bora kwa kila mtu ilihari hata nchi tajiri zinapata changamoto kubwa sana kufikia hiyo hatua, tunatakiwa tujipange vinginevyo watatushinda kwa hoja mbele ya wananchi.
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.