Royals
JF-Expert Member
- Nov 19, 2011
- 1,476
- 389
Wana jamii forum, sioni kama mkubwa wa bwana James Mbatia ataafiki kufukuzwa kwa mbunge huyu kwa sababu zifuatazo;
1. C.C.M. wanajua fika kuwa jimbo la Kigoma kusini si lao ni la Upinzani.
2. C.C.M. wanajua kuwa jimbo hilo si la NCCR bali ni la Kafulilia, wapiga kura walimpenda Mgombea na wala si chama.
3. C.C.M. wanajua kuwa kama Kafulila atagombea kwa tiketi ya Chadema ni hakika kuwa mshindani wao mkubwa ataongeza kifaa kingine ambacho ikitokea hivi ni mbaya kwao na hivo ni heri kufanya juu chini ili Kafulila abaki Nccr kuliko kwenda CDM.
4. Jimbo la Igunga lilikula sana mtaji wa nchi kiasi ambacho hakuna anayeomba jambo hili litokee tena. Kwa hali ilivo kwa sasa hata mbunge akishikwa na Maralia tu atakimbizwa India ili asije akafa na kusababisha kurudiwa kwa uchaguzi. Uchaguzi kama wa Igunga ukitokea mara mbili tu basa msishangae kuja kwa kodi ya kichwa.