Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,390
- 2,851
Google imeanza mchakato wa kuondoa Mfumo wa kutumia Qr Code kuweza kuunganisha simu na kompyuta kwenye Google Messages for Web .
Zamani ukienda kwenye Messages for Web, ulipata QR Code kwenye kompyuta: Simu → Messages → Device Pairing → Scan QR Code → Scan QR kwenye PC sasa mambo yamebadilika bhana.
Badala yake, Google inaelekeza watu Kuanza kutumia Google Account kufanya pairing ya Messages kati ya simu na kompyuta. 💻📲
Mabadiliko haya yanaanza kusambazwa hatua kwa hatua—kwa hiyo usishangae kama QR Code bado ipo kwenye simu yako. 👀
Unaionaje mabadiliko haya tuachie maoni yako 👋
#bongotech255