Mbunge wa zamani wa Kilwa Kusini, Suleman Bungara, 'Bwege', ametoa wito kwa Watanzania kutoaingia kwenye mgogoro wa dini aliodai kuwa umeanzishwa na watu waliojawa na uroho wa madaraka ambao wamebuni silaha ya kufarakanisha wananchi kwa misingi ya dini ili kuendelea kulinda maslahi yao.
Akizungumza na MwanaHALISI DIGITAL 'Bwege', amesema kuwa silaha ya udini mbaya inaweza kuufarakanisha umma hivyo amesema kuwa Watanzania ni vema wakajiweka kando na mchezo huo.
"Kuna watu wanatengeneza makusudi mgawanyiko kwa maslahi binafsi, tusikubali kugawanyika kwa kuwa sisi sote ni watoto wa Adam na Hawa., tusigawanywe na hawa wataka madaraka na wanaotaka matajiri kwa njia za haramu, kuna kikundi kina madaraka na utajiri ndio wanaotugambanisha.
View: https://www.instagram.com/reel/DTNTcp8AkpO/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
Hawa watu wapo tayari kuua kwa ajili ya madaraka yao ili kutugawa sisi, naomba Watanzania, tusikubali," Suleman Bungara 'Bwege'.
Hata hivyo .
Bwege amesema kuwa yanayoendelea nchini, ni mpango mahsusi wenye lengo la kuwagawa Watanzania, kwa misingi ya kidini ili waendelee kutalawa katika mfumo usiokuwa wa haki.
“Ninawaomba tusikubali kugawanyika katika dini zetu, sote ni wamoja,” amefafanua.