Bwawa la Stiegler likijengwa, basi Rais wetu aendelee kama bonus!

Ni wajibu wake kama Rais, hamna haja ya kumpa bonus,hutakiwi kushangaa na kutoa povu kwa kufurahishwa na hayo, yampasa afanye kwa ajili ya Taifa lake.
We ulitegemea akanyoe kiduku pale, hilo ni jukumu lakeeee !
Shabaashi.
 
Akimaliza kujenga mastiglaz pale singida kuna umeme wa upepo ukivunwa vizuri tunasambaza umeme afrika nzima, yani wenzetu wafikiria umeme wa gigawatts(GB) kwenda tetrawatts sisi bado tunajisifu na kuanza kuzalisha vimegawat(MB)
 
Kama Rais wetu pamoja na Serikali yake wakifanikisha kutuingizia zaidi ya 2000 MW za Umeme kwenye Gridi yetu ya Taifa

Inawezekana kujengwa, Data zote wanazo Norplan toka miaka zaidi ya 20 iliyopita. Baada ya Norplan kuondoka Idara ya Haidrolojia Wizara ya Maji iliendelea kukusanya takwimu za mto rufiji. Hawa wanatakwimu za kidatu pia na mito husika. Tatizo mpaka leo wanapewa hela ndogo sana ya kufanyia kazi.
 
Kama Rais wetu pamoja na Serikali yake wakifanikisha kutuingizia zaidi ya 2000 MW za Umeme kwenye Gridi yetu ya Taifa, basi kama wakipenda na kukubali kuendelea kuongoza baada ya 2025 na iwe hivyo, lkn kama wakipenda wenyewe kwani hiyo siyo kazi ya kitoto kwa nchi ya Kiafrika, Ethiopia wameweza lkn kwa ungangari haswa, hivyo kwangu mimi hiyo ni litmus test , kama kweli tukijenga na kuzalisha umeme wa MW 2000 basi najua tumeshatoka na tutaitafuta double digit economic growth.
nchi ngapi zina double digt ec, growth? acha mihemko
 
Kama Serikali hii ikifanikiwa kutuingiza 2000 MW za Umeme kwenye gridi ya Taifa basi wanastahili kuongezewa muda kama wakipenda kufanya hivyo!

2000 MW, that is a lot of power man, we going to become super power country in Africa. I concur.
 
2000MW kwa kutumia water turbines ni jambo jema lakini ni vyema pia tukajifunza kuwa na vipaumbele ili tuache kutapanya pesa, 2000MW ikiingia kwenye grid jumlisha tulizonazo ni kama tutakuwa tumemaliza tatizo la umeme wa kutosha ila changamoto itabaki kwenye miundombinu ya umeme na Tanesco kujiendesha kibiashara.. Taifa lingekuwa na vipaumbele na policy basi leo hii tungeweza kuwa na hiyo 2000MW maana tayari gas ilishakuwepo na miundombinu tayari ipo kilichotakiwa ni uwekezaji wa either Gas turbines au Gas engines ambapo cost isingekuwa kubwa kama kuanza upya na Water turbines.. Awamu ya nne kama nchi ingekuwa na policy na vipaumbele basi inawezekana huo mradi ungekuwa tayari, lakini baadala yake tunaishi kama tumbili shika pale acha shika pale acha basi full vurugu, maana either awamu ya nne ingeanza na huu mradi nakuachana na Gas au ingeanza na Gas na awamu ya tano ikamlizia katika kipindi cha miaka miwili kwa maana ya 2015 - 2017 tayari tungekuwa na hizo 2000MW.

Suala la kuendelea kuongoza huo ni ujinga maana kazi ya serikali yeyote duniani ni kutimiza majukumu yaliyombele yake, Serikali kuhakikisha mifumo iko imara na vizuri ni majukumu yake na sio msaada kwa wananchi, Suala la msingi kama utawala huu unajiamini uko smart ni kuhakikisha unatengeneza mazingira ya watanzania wote kuwa smart kiasi cha taifa kuwa na watu wengi walio tayari na smart kiasi cha kuweza kuongoza nchi kizalendo na tija na faida ikaonekana kwa jamii yoote ya kitanzania. CCM bado ina deni kubwa kwa wananchi wa Tanzania baada ya kushindwa kufanya mambo mengi ya msingi toka 1961 kwa uzembe wao wenyewe hivyo kwa sasa hawana budi kulipa deni tena kwa speed na faida.
 
2000 MW, that is a lot of power man, we going to become super power country in Africa. I concur.

Kwa hiyo 2000MW tu uwe superpower,?? Bado tuna deni kubwa sana kuufikia huo usuper power wa Africa..
Maana hata sasa bila hiyo 2000MW mbona tungeweza tu kuwa superpower Africa kama akili na bongo zetu zingefanya kazi vizuri maana tuna kila kitu Mungu ametujalia ambacho kingeweza kutufanya kuwa super power Africa na Dunia
 
Mkuu hakuna haja ya kumwongezea mtu muda wa kutwawala isipokuwa anatakiwa aandaliwe mtu anayeweza kusimamia maendeleo yaliyopatikana ili tuweze kusonga mbele. Hebu fikiria ikiwa Nyerere angebaki madarakani hadi akafariki nchi ingekuwa katika taharuki gani?

Suala la umeme wa Stiegler 2000MW hilo tayari ni suala la kusubiri kuanza kazi tu. Magufuli akishasema Pesa Ipo anamaanisha.
Kama nilivyoandika mbele inawezekana kujenga sababu Norplan wanazo data toka 1980s Hydrology Department pale Ubungo waliendelea kukusanya takwimu za mto rufiji. Lakini OC ya kuwawezesha ufuatiliaji ni kiduchu kwa hiyo kazi haifanyiki. Na mkuu wa idara ataesema OC haitoshi nadhani. tamko. uliliskia. Umeme hauji kwa matamko Mkuu. Hiyo Mungu peke yake ndio alisema na iwe Nuru ikawepo.
 
Kwa hiyo 2000MW tu uwe superpower,?? Bado tuna deni kubwa sana kuufikia huo usuper power wa Africa..
Maana hata sasa bila hiyo 2000MW mbona tungeweza tu kuwa superpower Africa kama akili na bongo zetu zingefanya kazi vizuri maana tuna kila kitu Mungu ametujalia ambacho kingeweza kutufanya kuwa super power Africa na Dunia

2000mw + how much we using now since independence? Less than 2000. Now think, 2000mw in less than ten years, isn't that super power.
 
2000mw + how much we using now since independence? Less than 2000. Now think, 2000mw in less than ten years, isn't that super power.

Hiko sio kigezo cha kujiita SUPER POWER, bali ni moja ya msingi kuelekea maendeleo kama tutaweza kupambana na kuweka mambo mengine sawa, "Tembea uone" kwanza hapo tumechelewa sana maana ilitakiwa tuwe na uwezo huo toka 1980 huko.

Bado kuna mambo mengi sana hayako sawa na tunahitaji nguvu ya ziada kuyaweka sawa ili kuyafikia maendeleo ya kweli.
 
Back
Top Bottom