Bwana Kadogosa na Shirika la Reli mmejiandaa kujiendesha kisasa na kupambana na changamoto za uendeshaji TRC mpya ya SGR?

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
Juzi tumesikia garimoshi la kwenda Dodoma limedondoka na mabehewa kadhaa yameanguka.

Watu wengi wamejeruhiwa na wengine kufukiwa na vifusi vya michanga na udongo.

Hiyo ilikuwa ni baada ya mvua kubwa kunyesha eneo la Bahi na kusababisha njia ya reli kuzama hivyo kusababisha garimoshi kupita njia isiyo rasmi ya matope na kuangusha reli ambayo ilihamishwa na maji yalotokana na mvua ilonyesha.

Akihojiwa na vyombo vya habari bwana Kadogosa amesema TRC huwa wanafanya tathmini au Risk Assessment kubaini athari zinazoweza kutokea endapo njia madhubuti hazitachukuliwa kuzuia ajali kama hizo kwenye njia hizo za reli hiyo kongwe ya kati.

Lakini pia mmoja wa wananchi wa sehemu hiyo amedai kuwa kwa kipindi kirefu hakukuwa na mvua kubwa zilizonyesha katika eneo hilo hivyo kuja kwake mvua hizo ilikuwa ni jambo la kushitua na halikutarajiwa.

Habari nzuri ni kwamba reli ya kisasa ya SGR yaja na itaondoa kadhia ya reli hiyo ya kati katika kipande cha Morogoro na Dodoma.

Lakini jambo la msingi kwa TRC kwa sasa ni kujiandaa kujiendesha kisasa ili kuweza kukabiliana na matatizo kama hayo ya mvua katika maeneo ya bonde ambamo njia za reli zapitia.

Nikisema kisasa namaanisha kwamba mkandarasi wa sasa wa SGR atakuwa pia anafunga mitambo ya kisasa ya "real time systems" pamoja na mitambo ya kamera maalum za usalama za CCTV ambazo zinatatandazwa katika mfumo mzima wa reli hizo kuanzia Dar-es-Salaam hadi mwiho wa reli hiyo.

Hivyo basi vituo vyote vya polisi wa reli kuunganishwa na mifumo hiyo kwa ajili ya kutazama na kulinda miundo mbinu ya reli ambayo ni muhimu kwa uchumi wa nchi hii.

Naweza kulichukulia tukio la kuanguka kwa garimoshi hili eneo la Bahi kuwa ni la kizembe kwani lingeweza kabisa kuepukwa endapo hatua madhubuti bila mitambo ya kisasa wala mitambo ya kamera za CCTV kuwepo.

Pia naweza kulichukulia tukio la kuanguka kwa garimoshi sehemu ya bahi kuwa ni hujuma za makusudi ambazo zimefanywa na watu wanaoshirikiana na wapinga maendeleo yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano.

Sikatai hata katika nchi zinazoendelea kunakuwepo na ajali za garimoshi lakini mara nyingi chanzo cha ajali hizo na uzembe wa dereva wa garimoshi hizo kwa ama kulala njiani kutokana na kufanya sana kazi bila kupumzika au watu wanaoangalia njia za reli hizo kupitiwa kizembe na kushindwa kuona kwamba reli zimeathiriwa ama kwa mti kuanguka au hali ya hewa kama barafu jingi.

Lakini mazingira ni tofauti na ya kwetu na sisi pia twaweza kudhibiti ajali hizi kwa kuangalia alama za nyakati na kuwa macho na wahujumu.

Hii ni Tanzania mpya na hakuna kulala hadi kieleweke ili vizazi vyetu vya baadae vije kujivunia matunda ya kazi ngumu ya leo ya kuwaletea maendeleo Watanzania wote.

Hivyo kila mara kuwepo Risk Assessment katika maeneo yote hatarishi na hatua zichukuliwe ili kuzuia ajali na matukio kama hayo.

Hizi "Risk Assessment" hazifanywi baada ya matukio bali hufanywa kabla ya matukio ili kutengeneza vipambanishi au "Mitigations" ili kuzuia athari hizo.

Serikali kupitia TRC ianzishe kitengo maalum cha kipekee cha kuchunguza hizi ajali za reli ambazo hazieleweki barabara vyanzo vyake.

Kitengo hichi kisheria kitachunguza ajali za garimoshi, vifo na majeruhi wanaotokana na ajali hizo na uharibifu wa njia, vifaa vya reli na mali za wananchi wanaozunguka maeneo ya karibu zinamopita njia za reli.

Hivyo bwana Kadogosa na wenzio mjipange na msichukulie poa matukio hayo bali changamoto mpya ya wenye nia mbaya na wahujumu uchumi dhidi ya jitihada zako na za serikali katika kumkomboa Mtanzania wa kawaida ambae ataka kusafiri kwa raha kutoka Dar kwenda mikoani.

Au mwaonaje ndugu zanguni na Bwana Kadogosa?
 
Back
Top Bottom