TAECOLTD
JF-Expert Member
- Mar 2, 2013
- 1,051
- 1,845
Habari za siku ya leo ndugu zangu, bwana harusi si neno geni lakini napenda nilitumie neno hili kufikisha ujumbe niliouandaa kwa siku ya leo.
Bwana harusi ni mtu yule ambaye amekwisha hakikisha taratibu zote zimefuatwa ikiwa ni pamoja na kujitambulisha ukweni, kupeleka posa pamoja na kulipa mahari kama ilivyo desturi kisha kupanga tarehe ya kufunga ndoa hiyo na hatimaye kamati kuanza na taratibu za ndoa kuanza rasmi. Je unadhani bwana harusi huruka hatua zote hizo hadi kufika kanisani au msikitini kufunga ndoa? Unafahamu kuwa wale walioruka hatua zote na kujiamulia kuishi pamoja pasi kupita hatua yoyote hapo hukumbana na matatizo makubwa makubwa sana sababu hawakujiandaa au hawakuandaliwa vizuri kisaikolojia?
Sasa basi mafanikio yoyote ya mwanadamu yanahitaji maandalizi mazuri ikiwa ni pamoja na kuwa na wazo na si ilimradi wazo tu bali wazo imara na lililoshiba, kuliainisha wazo hilo katika karatasi au computer, kujipatia elimu zaidi kuhusu wazo hilo, kulifanyia kazi, kuwa na msimamo kwa wazo hilo na hatimaye kungojea mafanikio.
Kamwe hakuna mafanikio yanayokuja kwa bahati mbaya pasi kuwapo kwa maandalizi, vivyo hivyo hakuna bwana harusi bila kuwapo kwa maandalizi stahiki. Wakati ni wako sasa na utumie vizuri hatimaye uwe bwana harusi au bibi harusi mwenye mafanikio
Nikutakie siku njema na yenye mafanikio tele
Mkurugenzi Mtendaji
TAECO LTD
www.facebook.com/TAECO2012
www.taecoltd.webs.com
Sent using Jamii Forums mobile app