Bwana Afya Kukingia kifua wachafuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bwana Afya Kukingia kifua wachafuzi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by lumange, Aug 5, 2011.

 1. l

  lumange Member

  #1
  Aug 5, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna Bwana afya Kata ya Kariakoo kwenye Manispaa ya Ilala anatishia usalama wa kazi za kiafya, yeye yuko na maafisa afya wenzie wawili yaani jumla ni watatu kwenye Kata hiyo isipokuwa yeye ni mwenyeji kuliko wote, Kwa kutumia kigezo cha kukaa sana amejijengea mazingira ya kuwalinda wafanya biashara wa migahawa, baa, maduka na ma hotel kiasi kwamba wenzie wakienda kukagua na kukuta uchafu wakitaka kuchukua hatua za kisheria yeye anawaambia watuhumiwa kuwa hakuna atakayewafanya chochote nyie lete pesa nimpelekee Bwana Afya wa Manispaa ambaye ndio bosi wao wote.

  Kwa hiyo ndugu zangu mnaokula kwenye migahawa na kununua bidhaa kwenye min super marketi za Kariakoo kuweni macho, kabla ya kuagiza chakula nenda uani angalia hali ya vyoo na ikiwezekana penyeza macho jikoni na sehemu za kupakulia vyakula mtajionea maajabu ya chakula kinavyoandaliwa kwenye mazingira hatarishi kiafya.

  Kwenye min super markets kuna vyakula vilivyopitwa na muda wa kutumika vingine vikikamatwa vikaletwa ofisi ya kata iliyopo kwenye jengo la DDC Kariakoo ghorofa ya tatu, Bwana Afya huyu mkongwe katika kata hii anawaita wakachukue vitu vyao waendelee kuviuza!

  Alipotafutwa Afisa mtendaji wa kata hiyo kuthibitisha tuhuma hizo hakuweza kupatikana kwa kile kinachosemekana yuko likizo, Maafisa afya wenzie hawakuwa tayari kuzungumzia tuhuma hizi kwa kuhofia kupikiwa majungu kwa Afisa Afya wa Manispaa ambapo wanadai adhabu yake ni kuhamishiwa kata za nje ya mji kama Kinyerezi au kazimzumbwe hata kama unaishi Bunju na kuwa utachelewa kufika kituo cha kazi na kushindwa kuleta ufanisi.
   
 2. Mulama

  Mulama JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Jamani hawa watu wapo kweli hapa mjini? na wanafanya kazi gani na wapi? hata hivyo kama mambo yenyewe ndio haya ya kulindana si tutakufa kwa kipindupindu?!
  Mkurugenzi na Meya wa Manispaa ya Ilala inabidi wachukue hatua za haraka Vinginevyo watu wengi wanakuja kariakoo kununua bidhaa mbali mbali hivyo suala la usafi ni muhimu tafadhari.
   
 3. Mulama

  Mulama JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Hii topic haina wachangiaji!! kuna hatari tukafa kwa magonjwa kwakuwa inaonekana hatujui hata umuhimu wa hawa wataalamu wetu!, kfiupi ni kwamba mtu huyu anachofanya ni sawa na traffic kuruhusu gari mbovu kubeba abiria, mpaka ipate ajari ndio watu tunaanza kuuliza chanzo.
  Kwenye jf hakuna mtu anayejua kariakoo atujuze ukweli wa kitu hiki?
   
Loading...