Business parter kanikimbia/kayeyuka

ya mufindi

JF-Expert Member
Dec 23, 2014
508
738
Wasalaam wana jukwaa hope mko poa na majukumu ya kulijenga taifa.

Katika pita pita hapa JamiiForums kuna jamaa wa Zanzibar akani PM ni akanielezea anapenda sana kilimo anataka awekeze shambani akaniulizia abc's nikamwelekeza vizuri tu,huyu jama yaani akawa anapiga simu hadi nakereka kila muda simu afu anataka muongee zaidi ya dakika20 anauliza mambo yaleyale aliyouliza jana hadi kuna muda sipokei simu zake maana kwangu dk20 ni upotevu mkubwa wa muda wangu so nikawa napokea nikiwa na muda tu jamaa nikipokea lawama kibao duuh.

Sasa mwezi wa tano akaja huku akayaona mashamba na mishe kibao za mbao,milunda,mabanzi,miti nk jamaa akachanganyikiwa kuwa anakaa tu mjini wakati fursa ziko vijijini,mwezi wa sita akatoa proposal kuwa tulime mahindi ya gobo/ya kuchoma huku akiahidi kuwa mimi nitajitolea nguvu kazi yaani kuandaa bustani,kulima,kupalilia maana palizi ndio dawa ya mahindi kustawi,kumwagilia nk kwakuwa vitendea kazi vilikuwepo kama pump na zana za kilimo nikasema poa.

Kwa upande wake yeye alisema atatoa pesa ya kukodia bustani jirani na mto ruaha,pesa ya mbegu,hela ya mbolea na madawa, tulipanga tupande mahindi tarehe 30 ya mwezi wa saba ili tuvune tar30 wakumi soko litakuwa zuri sana kwani mida hiyo mahindi ya kuchoma huwa adimu sana.

Mipango ikaanza kuwa vitendo muda wakukodi bustani nzuri ukafika jamaa maneno kibao mara nasubiri hela za urithi mara nasubiri kamisheni,kwa maneno anaonekana anatamani sasa hela hana anapiga simu hadi analia akasema kopa sehemu me nitakupa usijali, basi nikajipinda nikalipia ekari tatu sehemu jirani na mto na rutuba nzuri kwa 80,000×3=240,000 jamaa nikamwambia basi atume hela kidogo kwaajili ya dawa ya kuua magugu ili tuchome tulime ile hela tsh50,000 nayo alitoa kwa mbinde wiki nzima anapiga kiswahili tu. nikakopa sehemu alivotuma nikairejesha, ikaja kwenye kulima kila ekari elfu 50 nayo kiswahili ikabidi nilime kwa ng'ombe badala ya trekta jamaa maneno tu vitendo sifuri.

Ikaja kwenye hatua ya tuanze kupanda jamaa anasisitiza kuwa hela bado kidogo itatoka ikabidi ninunue mbegu kilo 15@15,000 nikaziweka nikamwambia mambo tayari sasa tuanze kazi jamaa kimya sasa hiv ni tarehe tano na hapokei cm,sasa sijui alikuwa tapeli au anapenda ila hela hana anashindwa kufunguka,kaniingizia hasara kubwa kwa maisha haya ya kuungaunga ningefanyia mambo mengine tu.

Japo sijakata tamaa nimeamua nilime ekari moja tu ambapo nita chimba mashimo 14,800 wastani wa chini kwa kupishanisha cm20 kwa cm70 then nitavuna hayo mahindi 14,800×200=2,960,000 kwa kima chani ndani ya siku 90 kwa gharama roughly jumlisha nilizopoteza kama laki8 hivi.

Nawashauri humu ndani wote sio wema tuwe makini kuanzisha ushirikiano nao.
 
Siku nyingine unishirikishe tupige hizo kazi Mimi nipo mufindi ndugu yangu
Hao wazanzibar wamezoea urojo tu

Kama jamaa kapotea ghafla jiridhishe kwanza ujue kama yupo, usikute Mwenyezi kampenda zaidi wewe huku unalaumu.
😃😃😀hili nalo neno kuna jamaa alikufa kwenye ajali ya meli ya nizigo nadhani MV skagit sisi huku tunamlaumu hatumi hela ukapita mwezi ndo tunaambiwa alifariki na mahindi yaliishia baharini ilituuma sana daah
 
Spacing ya mahindi ya gobo weka 30cm kwa 80cm (30*80) ili kupata mahindi makubwa kwenye heka ya mita 70*70 utapata jumla ya mahind 21,000

21,000*200tsh=4,200,000/=

Kila la heri.
 
Haya jamani wawekezaji mjitokeze, kuna eka 2 hapo, kwa hesabu za haraka haraka, mil6, haikosekani...Angalizo tuwe makini na kilimo cha nyuma ya keyboard..

Everyday is Saturday............................. :cool:
 
Biashara za partnership huwa zina changamoto sana, ni heri ufanye pekeyako
 
Spacing ya mahindi ya gobo weka 30cm kwa 80cm (30*80) ili kupata mahindi makubwa kwenye heka ya mita 70*70 utapata jumla ya mahind 21,000

21,000*200tsh=4,200,000/=

Kila la heri.
Binafsi mi changamoto yangu tuliyekubaliana ahudumie shamba ndie alitoweka bila kunipa taarifa, kwahiyo akaacha mazao na shamba peke yake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom