Hakika Busara ni neno zito,
Busara ya Taifa ilipotelea kwenye vyeti, hapo ndipo jahazi lilipoanza kuyumba, nahodha akaanza kuwatosa watu kwenye Maji ili jahazi lisizame, nahodha aliamini chanzo cha jahazi kuyumba ni watu aliowabeba, kumfukuza mtu aliyebakiza mwezi mmoja astafu Kwa kosa la vyeti feki ni jambo linalogusa "BUSARA" , Kama ingetumika busara kungewekwa mstari mwekundu, kwamba kuanzia sasa, waajiliwa wapya watahakikiwa vyeti vyao, !!!
BAADA YA HAPO UBUNIFU UMEPOTEA KABISA KWA WATENDAJI, KINACHOENDELEA SAHIVI NI KUSIKILIZA MAAGIZO.
…...........................................
Wakati hayo yakiendelea tujikumbushe historia ya haya matukio je nani mkweli? Tumwamini yupi?
- Waliotaja Mhongo ni muongo walipuuzwa Lakini leo imethibitika kumbe kweli alikuwa muongo.
- Kuna watu walisema ndege Mpya mbovu, kundi jingine likakanusha vikali lakini baadae ukweli ukatajwa kuwa ile ndege ilikuwa na matatizo.
- Clouds TV ilipovamiwa wakapinga vikali kwamba si kweli lakini footage ya video ilipotoka baadae wakakubali lakini Kwa kisingizio cha ulinzi.
- Watu mwanzo walipouawa MKIRU propaganda nyingi sana zilisemwa lakini baadae ikathibitika.
- Tundu alitahadhalisha utekaji Wa makinikia uzingatie sheria akaitwa mnafiki
- Fedha za escrow zilisemwa si za Umma lakini baadae zimekuja julikana ni za Umma badala wazipeleke Bank, wakaanza rejesha TRA
- Waliosema Bombardier Q400 imekamatwa Canada walipingwa lakini baadae imethibitika ni kweli imeshikiliwa.
- Wasanii kina roma walitekwa na watu wasiojulikana hadi Leo? Hata mgambo asingeshindwa chunguza hilo!
- Waliomtolea bastora nape wakatajwa hawakuwa Askari na hawajulikani walipo hadi Leo
- Wenye vyeti feki walikuwa raia tu, askari hawawezi gushi vyeti.
- Ben saa nane alitekwa na watu wasiojulikana hadi Leo.....
- Mwangosi alipigwa na kitu chenye incha Kali ....uchunguzi unaendelea
- Alphonce Mawazo alipigwa na kitu kizito.....uchunguzi unaendelea
- Imma Advocate ilivamiwa na wahuni wasiojulikana... Uchunguzi unaendelea.
- Tundu lisu kapigwa risasi na watu wasiojulikana.... Uchunguzi unaendelea.
***HIVI HUWA HAMUANGALII HATA MOVIE ZA ULAYA WANAVYOCHUNGUZA?.....naomba nijibiwe na nyinyi watu msiojulikana ***
(Hakuna rafiki au adui Wa kudumu; waliomlinda Lowassa enzi hizo, Leo wanamshambulia, aliyekuwa waziri Wa polic enzi hizo Leo anashitakiwa na polic Kwa uchochezi,....UNAPOFIKILIA KUMUUA MPINZANI LEO, NI KUFIKILIA KUMUUA NDUGU YAKO WA KESHO!..UNAPOWAZA KUUA LISSU, UNAWAZA KUUA WATANZANIA!
[HASHTAG]#kama[/HASHTAG] polepole angeuawa kipindi kile, Leo hii asingekuwa katibu Wa CCM#
"shindaneni Kwa hoja"