Mifumo isiyoonekana inayojenga nchi

Mifumo isiyoonekana inayojenga nchi

Mgosi Mbena

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2023
Posts
544
Reaction score
664
Kwa kawaida Watu au waafrica tunapozungumzia maendeleo tunaongelea vitu kama Ajira,Miladi wawekezaji kutoka nje,mikubwa,Au kugundulika kwa rasilimali kama mafuta,dhahabu au gesi .

Lakini kamwe hatuangali mifumo na nguzo hizi zinazotengeneza na kukuza uchumi.

Nguzo ya kwanza : UAMINIFU
Uaminifu wa watu,taasisi na jamii huongeza na kukuza uchumi kwa kuchochea biashara na ujasiria mali,
Jamii ya watu wasio waaminifu ni ngumu sana kufanya nao biashara, kuagiza mizigo,kulipia bidhaa.

Kwa sababu hiyo mtu lazima awepo ana kwa ana ndio mfanye biashara kwa kuogopa kutapeliwa.
Kuna watu wengi sana nchini wanaogopa kufanya biashara ya kutoa bidhaa mahali ilipo kupeleka sehemu nyingine bila kuepo eneo la tukio.

Mfano: mwaka 2013 Nilimtumia mtu (Namfaham) shilingi 270000 anitumie Karoti kutoka mbeya hadi Dodoma. Jamaa alipotumiwa hela akatokomea.
Leo hii ukisahau simu au laptop mahali dk0 huioni.

Sehemu iliyojaaa :Wizi,Utapeli, uzurumishi hamna biashara au uwekezaji unaweza kukua hapo

Nguzo ya pili :MUDA
Muda ni kiungo kizuri sana kama nchi na jamii inataka kuendelea.Jamii ambayo haijali muda ni ngumu sana kuendelea kwani maendeleo hupimwa na muda pia!
Ukitazama vikao: watu hufika saa moja baada ya muda husika, Harusi au sherehe watu huja masaa3 baada ya muda tajwa. Kila mradi unaofanyika lazima upilize deadline..
Kifupi sehemu ambayo muda si kipaumbele hata Kusonga mbele( si kipaumbele pia)

Nguzo ya tatu : MTAZAMO WA UJASIRIA MALI
Kuwepo jamii zenye mtazamo huu huchochea ubunifu na biashara! Sehemu ambayo kila mtu anawaza kuajiriwa ni ngumu sana kuwa na jamii iliyoendelea kwani hamna nchi inajengwa na Ajira tu.

Ni wajasiriamali ndio huanzisha safari zinazozalisha ajira.Kama hakuna hawa basi kila mtu atakua analia na ajira

Nguzo ya Nne: Uwezo wa kutatua matatizo!
Badala ya kuajiri watu kuzingatia vyeti watu watazamwe kwa uwezo wa kutatua matatizo! Leo tuna watu kwene idara nyeti wasio na uwezo wa kutatua matatizo ya taasisi, jamii, badala yake wao ni sehemu ya matatizo!
Hii ndio msingi wa maendeleo wenyewe
 
Nguzo ya kwanza : UAMINIFU
Uaminifu wa watu,taasisi na jamii huongeza na kukuza uchumi kwa kuchochea biashara na ujasiria mali,
Jamii ya watu wasio waaminifu ni ngumu sana kufanya nao biashara, kuagiza mizigo,kulipia bidhaa.
Mzee umbumbumbu wetu ndio unafanya tuwaze uaminifu pekee. Nchi za wenzetu hazina watu waaminifu, zina strict legal systems tu! Ukizingua unafilisiwa na kufungwa fasta. Sisi tunataka kubembeleza watu wawe na hofu ya Mungu badala ya kuweka mifumo inayowabana wezi.
MTAZAMO WA UJASIRIA MALI
Kuwepo jamii zenye mtazamo huu huchochea ubunifu na biashara! Sehemu ambayo kila mtu anawaza kuajiriwa ni ngumu sana kuwa na jamii iliyoendelea kwani hamna nchi inajengwa na Ajira tu.
Kila mtu akiwa mjasiriamali nani atamfanyia kazi mwenzake? Hiyo entrepreneurship mindset inahubiriwa kwa sababu soko la ajira limefeli, hakuna nchi iliyoendelea kwa kila mtu kuuza nyanya au genge, tunachohitaji ni kuwa na viwanda vikubwa vinavyotoa ajira rasmi na za kueleweka.
 
Mzee umbumbumbu wetu ndio unafanya tuwaze uaminifu pekee. Nchi za wenzetu hazina watu waaminifu, zina strict legal systems tu! Ukizingua unafilisiwa na kufungwa fasta. Sisi tunataka kubembeleza watu wawe na hofu ya Mungu badala ya kuweka mifumo inayowabana wezi.

Kila mtu akiwa mjasiriamali nani atamfanyia kazi mwenzake? Hiyo entrepreneurship mindset inahubiriwa kwa sababu soko la ajira limefeli, hakuna nchi iliyoendelea kwa kila mtu kuuza nyanya au genge, tunachohitaji ni kuwa na viwanda vikubwa vinavyotoa ajira rasmi na za kueleweka.
Mkuu unaweza kuwa sahihiii kwa mifano unayolenga!
Lakini angalia inchi zote zilizofanikiwa zina
Kitu kimoja in common “UAMINIFU” hata mali ikipotea ni inapatikana
  1. 🇯🇵 Japan — exceptionally effective lost-and-found system; police receive and catalog millions of lost items.
  2. 🇸🇬 Singapore — organized public transport and police lost-property systems.
  3. 🇨🇭 Switzerland — strong lost-property systems, particularly on public transport.
  4. 🇩🇪 Germany — municipalities and transport companies operate formal Fundbüro (lost-and-found offices).
  5. 🇳🇱 Netherlands — well-organized systems for lost items, especially on trains and public transport.
  6. 🇬🇧 United Kingdom — transport operators, police, and private lost-property services handle lost items.
  7. 🇰🇷 South Korea — centraliz
 
Kuna ukweli mmoja mchungu inabidi tuukubali mkuu, binadamu wote duniani tabia zao zinafanana sana, kinachowatofautisha ni mazingira na mifumo inayowaongoza.

Chukua Mbongo mmoja mjanja mjanja kutoka Kariakoo, mpeleke hapo Singapore au Tokyo aishi huko kwa mwaka mmoja, unafikiri ataiba simu akizikuta zimesahaulika? Hawezi na atakuwa ni mtu mwaminifu sana pengine kuliko hata wao, kwa sababu anajua kule hakuna connection ya mjomba itakayomtoa korokoroni.

Sasa chukua huyo Mjapani unayemsifia, mtoe Tokyo mlete aishi mazingira yetu ya uswahilini ambapo umeme unakatika siku tatu, maji hakuna, na polisi ukiwafuata wanakuomba rushwa. Nakuhakikishia baada ya miaka miwili huyo Mjapani atajifunza michongo na atakuwa wa kwanza kukutapeli!

Uaminifu ni matokeo ya mazingira yanayomzunguka mwanadamu.
 
Ha ha una point mkuu
 
Back
Top Bottom