Busara ya Nchi ilipotelea kwenye vyeti feki

Busara ya Nchi ilipotelea kwenye vyeti feki

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
12,280
Reaction score
23,439
Hakika Busara ni neno zito,
Busara ya Taifa ilipotelea kwenye vyeti, hapo ndipo jahazi lilipoanza kuyumba, nahodha akaanza kuwatosa watu kwenye Maji ili jahazi lisizame, nahodha aliamini chanzo cha jahazi kuyumba ni watu aliowabeba, kumfukuza mtu aliyebakiza mwezi mmoja astafu Kwa kosa la vyeti feki ni jambo linalogusa "BUSARA" , Kama ingetumika busara kungewekwa mstari mwekundu, kwamba kuanzia sasa, waajiliwa wapya watahakikiwa vyeti vyao, !!!
BAADA YA HAPO UBUNIFU UMEPOTEA KABISA KWA WATENDAJI, KINACHOENDELEA SAHIVI NI KUSIKILIZA MAAGIZO.
…...........................................
Wakati hayo yakiendelea tujikumbushe historia ya haya matukio je nani mkweli? Tumwamini yupi?
  • Waliotaja Mhongo ni muongo walipuuzwa Lakini leo imethibitika kumbe kweli alikuwa muongo.
  • Kuna watu walisema ndege Mpya mbovu, kundi jingine likakanusha vikali lakini baadae ukweli ukatajwa kuwa ile ndege ilikuwa na matatizo.
  • Clouds TV ilipovamiwa wakapinga vikali kwamba si kweli lakini footage ya video ilipotoka baadae wakakubali lakini Kwa kisingizio cha ulinzi.
  • Watu mwanzo walipouawa MKIRU propaganda nyingi sana zilisemwa lakini baadae ikathibitika.
  • Tundu alitahadhalisha utekaji Wa makinikia uzingatie sheria akaitwa mnafiki
  • Fedha za escrow zilisemwa si za Umma lakini baadae zimekuja julikana ni za Umma badala wazipeleke Bank, wakaanza rejesha TRA
  • Waliosema Bombardier Q400 imekamatwa Canada walipingwa lakini baadae imethibitika ni kweli imeshikiliwa.
  • Wasanii kina roma walitekwa na watu wasiojulikana hadi Leo? Hata mgambo asingeshindwa chunguza hilo!
  • Waliomtolea bastora nape wakatajwa hawakuwa Askari na hawajulikani walipo hadi Leo
  • Wenye vyeti feki walikuwa raia tu, askari hawawezi gushi vyeti.
  • Ben saa nane alitekwa na watu wasiojulikana hadi Leo.....
  • Mwangosi alipigwa na kitu chenye incha Kali ....uchunguzi unaendelea
  • Alphonce Mawazo alipigwa na kitu kizito.....uchunguzi unaendelea
  • Imma Advocate ilivamiwa na wahuni wasiojulikana... Uchunguzi unaendelea.
  • Tundu lisu kapigwa risasi na watu wasiojulikana.... Uchunguzi unaendelea.
***HIVI HUWA HAMUANGALII HATA MOVIE ZA ULAYA WANAVYOCHUNGUZA?.....naomba nijibiwe na nyinyi watu msiojulikana ***

(Hakuna rafiki au adui Wa kudumu; waliomlinda Lowassa enzi hizo, Leo wanamshambulia, aliyekuwa waziri Wa polic enzi hizo Leo anashitakiwa na polic Kwa uchochezi,....UNAPOFIKILIA KUMUUA MPINZANI LEO, NI KUFIKILIA KUMUUA NDUGU YAKO WA KESHO!..UNAPOWAZA KUUA LISSU, UNAWAZA KUUA WATANZANIA!
[HASHTAG]#kama[/HASHTAG] polepole angeuawa kipindi kile, Leo hii asingekuwa katibu Wa CCM#
"shindaneni Kwa hoja"
 
Hili ni sahihi kuchunguzwa
Kwamba kuna watu wanaitwa wa chama tawala na wengine wapinzani naona kuna taabu hapo
Police anaamini mpinzani hawiki afu mtu wa chama tawala kuchukuliwa hatua ni haramu hadi pale maagizo yawepo .
Na hii ni dhambi kubwa sana leo kwangu kesho kwako watch out

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kawaida tu..mbona Mzee Karume aliuawa na maisha yanaendelea..mbona John F Kennedy aliuawa na maisha yakaendelea..Sokoine aliuawa maisha yakaendelea..
Kuna wakati lazima mtu/watu afe/wafe ili maisha yaendelee
Hata Chacha Wangwe aliuawawa makusudi ili maisha yaendelee..pengine angekuwepo leo usingemsikia Mbowe.
Hata zitto amepotezewa timing ya kisiasa ili maisha yaendelee
 
Siyo wa kwanza huyo ni mengi sana yalishatokea na maisha yanasonga alikufa baba mzazi maisha yakasonga eti kushambuliwa kwa Lissu tuone ajabu angekuwa ni wa kwanza kushambuliwa hapa nchini tungeshituka ila ni muendelezo wa yale ya nyuma hakuna jipya chini ya jua
 
Kawaida tu..mbona Mzee Karume aliuawa na maisha yanaendelea..mbona John F Kennedy aliuawa na maisha yakaendelea..Sokoine aliuawa maisha yakaendelea..
Kuna wakati lazima mtu/watu afe/wafe ili maisha yaendelee
Hata Chacha Wangwe aliuawawa makusudi ili maisha yaendelee..pengine angekuwepo leo usingemsikia Mbowe.
Hata zitto amepotezewa timing ya kisiasa ili maisha yaendelee
ujue unaakiri sana wewe:
1.umenena ukweli
2.umewakumbusha watu ukweli
3.umecelewa kuchangia ili watu watoe mapovu wakidhani wanaweza kuuficha ukweli.

ninahofu watakapoumbuka watachafua hali ya hewa. Mungu wa kweli atatushindia
 
Kawaida tu..mbona Mzee Karume aliuawa na maisha yanaendelea..mbona John F Kennedy aliuawa na maisha yakaendelea..Sokoine aliuawa maisha yakaendelea..
Kuna wakati lazima mtu/watu afe/wafe ili maisha yaendelee
Hata Chacha Wangwe aliuawawa makusudi ili maisha yaendelee..pengine angekuwepo leo usingemsikia Mbowe.
Hata zitto amepotezewa timing ya kisiasa ili maisha yaendelee
Kazi kweli
 
Karume aliuwawa baada ya yeye kuua wenzake. Kisasi cha baba wa muuaji kuuliwa baba yake hakikuisha. Kwa hiyo usishangae...

JFK aliuwawa baada ya nchi yake kuua viongozi wa nchi nyingine. TAFAKARI
 
Back
Top Bottom