Burundi: Watoto waliokamatwa kwa kuchora vibaya picha ya Rais Nkurunziza waachiwa huru

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Burundi imewaachilia huru wanafunzi watatu wa kike ambao walikamatwa wakishutumiwa kuichafua kwa kuichorachora picha ya rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza kwenye vitabu vyao vya shule.Waziri wa sheria Aimée Laurentine Kanyana ameeleza.

Kushikiliwa kwa wasichana hao takribani majuma mawili yaliyopita kwa shutuma za kumtusi rais kulizusha kampeni mitandaoni za kutaka wasichana hao waachiliwe kampeni iliyokua na jina #FreeOurGirls, watu wakituma picha kwenye mitandao ya Twitter.

Waziri amesema wasichana hao wenye miaka 15,16 na 17 wameachiwa huru kwa muda.

''Tunawataka wazazi kuboreha elimu ya watoto wao .Tunawakubusha watoto kuwa wanapaswa kuheshimu mamlaka,na kuwa umri wa kuwajibishwa ni miaka 15

Walikamatwa walipokuwa katika shule ya ECOFO iliyopo katika mkoa wa kaskazini wa Burundi wa Kirundo tarehe 12 mwezi Machi ,2019

Awali walishitakiwa wakiwa wanafunzi saba, lakini wanne wakaachiliwa huru.

Watatu hao walikua wanashikiliwa kwenye gereza la wanawake la mkoa wa Ngozi.

Mnamo mwaka 2016 shule mbali mbali mjini Bujumbura na mikoani watoto kadhaa walitiwa mbaroni wakihusishwa na matukio ya aina hiyo.

Shirika la kutetea watoto FENADEB lilikua msitari wa mbele kuwatetea watoto hao.

Mashirika ya kutetea haki za watoto nchini Burundi yameshauri uchunguzi wa kina ufanyikekabla ya kuwatia watoto hao hatiani ili kubaini ni kwa nini matukio kama hayo yanajitokeza.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari bila picha huwa ahinogi, weka picha ya muheshimiwa ile iliyochorwa
 
Kama mimi mzazi wa mtoto kati ya hao wala simwambii chochote mwanangu, nitampa tu moyo asome kwa bidii ili baadae aje kupinga vizuri tawala mbovu za kiafrika. Ukiona hadi unafikia kuchukiwa watoto wa miaka 16 ujue umeshindikana and you need to step down.
 
Matukio haya yanajirudia kwa sababu "Effect of dictatorship has no age boundary".
 
Walichora wakiwa shuleni je waalimu ndo waliripoti michoro hiyo ?
Je ni wanafunzi wenzao walioripoti ?
Vitu vingine ni kilujichafulia tuu Rais unashataki wanafunzi miaka 15 huku unaacha mambo yanayoamua mustakbali wa Taifa
 
Habari bila picha huwa ahinogi, weka picha ya muheshimiwa ile iliyochorwa

1553701945834.png
 
Nkurunzinza ni mpumbavu sana. Kwa umri ule bado hajui kuenenda na mtoto mtundu wala jambazi sugu. Adhabu ya jambazi sugu anampa mtoto mdogo aliyejamba kwa kula biskuti nyingi. 😂😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom