Burundi President says third term will be his last

Burundi President says third term will be his last

Huyo anapenda uchu wa uongozi,kwani angeacha kugombea angekufa au
 
Weeeee hivi unafkiri wao ni wajinga kuanza maandamano kabla ya uchaguzi??
Wanajua results zitakuwa twisted tuu.

Kwa hiyo hawakubali kushindwa. siasa gani hizi, inaonesha wameshindwa hata kabla ya uchaguzi, hawajiamini
 
Kwa hiyo hawakubali kushindwa. siasa gani hizi, inaonesha wameshindwa hata kabla ya uchaguzi, hawajiamini

Sio kutojiamini huyu mkuu kadhamiria kutaka kuendelea kuiongoza nchi so hata iweje anataka abaki so wananchi wakaona lilobaki nikuanza maandamano tuu yasiyo kuwa na kikomo.
 
Sio kutojiamini huyu mkuu kadhamiria kutaka kuendelea kuiongoza nchi so hata iweje anataka abaki so wananchi wakaona lilobaki nikuanza maandamano tuu yasiyo kuwa na kikomo.

Haina faida kuandamana namna hiyo. madhara ni mengi, tayari watu kadhaa wamepoteza maisha, wengine wamekimbia nchi yao. hasara tupu
 
Mbona naona kama hujamwelewa ana maanisha nini na wananchi wanataka nini????????????
 
Kama habari ulivyoiweka nguvu ya umma haijashinda kwani Nkurunzinza amesema anataka awamu hii ndo iwe ya mwisho wakati wananchi hawataki kuongozwau nae kwa awamu nyingine.
Inaelekea katiba yao imebakiza upenyo anaoutumia nkurunzinza kwa hivyo kwa faida ya amani warundi wasiwe kichwa cha mwendawazimu. La muhimu kwa warundi wadai jumuiya ya kimataifa kuwahakikishia uchaguzi huru haki na wa amani. Kama hawamtaki nkurunzinza watamtosa. Sio watu wachache kwa sababu za kikabila kutaka kuiletea nchi balaa.
 
Haina faida kuandamana namna hiyo. madhara ni mengi, tayari watu kadhaa wamepoteza maisha, wengine wamekimbia nchi yao. hasara tupu

Yaani hasara ni kubwa sana na ukichukulia nchi yenyewe ni miongoni mwa nchi maskini kabisa duniani kwa kiongozi anayejielewa asinge endelea kuendelea kukomalia madarakani hata kama kikatiba kweli unaruhusiwa ili kuinusuru nchi na hasara zaki uchumi na kijamii.
 
Sasa muda wowote alikuwa anasubiri nini kutoa hiyo kauli mpaka wananchi wake wameuwawa na kujeruhiwa .

Wanachokidai ni tofauti na kauli aliyoitoa, wao wanadai asigombee yeye anasema akichaguliwa safari hii hatogombea tena uchaguzi mwingne baada ya huu.
 
Hatimae nguvu ya uma imedhihiri nchini burundi baada ya kuushinda udhalimu.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amewaambia mawaziri wa Afrika Mashariki kwamba endapo atachaguliwa kuiongoza nchi hiyo mwezi June mwaka huu ,kwa muhula wa tatu basi itakuwa ni kipindi cha ukomo wa yeye kuendelea kusalia madarakani ,msemaji wa serikali ya Burundi Gervais Abayehorwa amesema hayo mapema Jumatano .

Rais Pierre Nkurunziza uamuzi wake wa kugombea kuiongoza nchi hiyo kwa muhula wa tatu uliibua hisia tofauti tofauti na kuzusha maandamano makubwa.

Waandamanaji wanadai kwamba kwa muujibu wa katiba ya nchi hiyo rais anapaswa kuiongoza nchi kwa mihula miwili tu.

Nayo mahakama ya katiba wameeleza kwamba hawahesabu muhula wa kwanza wa raisi huyo madarakani kwasababu aliteuliwa na wabunge na si kuchaguliwa kwa kupigiwa kura.

Regina Mziwanda kutoka mjini Dar-Es-Salaam amezungumza na msemaji huyo wa serikali ya Burundi ,kutaka kujua Nini ujumbe wa Rais Pirre Nkurunziza kwa taifa la Burundi pindi alipohutubia mapema Jumatano.?

Chanzo: BBC
Ili nguvu ya wananchi ishinde anatakiwa hasigombee kabisa. Lazima wafuate matakwa ya makubaliano ya Arudha yaliyoleta hiyo amani anaingia madarakani. Ameongoza vipindi viwili inatosha na hasianze kuitafasiri Katiba kwa matakwa yake. Isingekuwa hayo makubaliano kusingekuwa na kifungu hicho ndani ya Katiba. Hili siyo suala la kuchaguliwa na bunge au wananchi; ni suala la 'principle behind the requirement'. Bahati mbaya katika kundi la mawaziri wa Afrika Mashariki walioenda huko ni mawaziri wa Tanzania na Kenya tu wanaoweza kusimamia principle hii, wengine wako katika kundi la Madhambi yanayotendwa na Nkurunziza.
 
Kama habari ulivyoiweka nguvu ya umma haijashinda kwani Nkurunzinza amesema anataka awamu hii ndo iwe ya mwisho wakati wananchi hawataki kuongozwa nae kwa awamu nyingine.

Wanaotaka na wasiotaka aendelee kuongo wapi wengi? maana kama wasiotaka ni wengi kusingekuwa haja ya kuandamana bali watumie kura yao kama Jonathan walivyofanywa kule Nigeria
 
Title ni kitu chengine na ndani kuna kuna kitu chengine, sijuw hili ni tatizo la kutafsiri kiingereza! mana kuna ''Kill him Not,'' na ''Kill him, Not..''
 
Hatimae nguvu ya uma imedhihiri nchini burundi baada ya kuushinda udhalimu.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amewaambia mawaziri wa Afrika Mashariki kwamba endapo atachaguliwa kuiongoza nchi hiyo mwezi June mwaka huu ,kwa muhula wa tatu basi itakuwa ni kipindi cha ukomo wa yeye kuendelea kusalia madarakani ,msemaji wa serikali ya Burundi Gervais Abayehorwa amesema hayo mapema Jumatano .

Rais Pierre Nkurunziza uamuzi wake wa kugombea kuiongoza nchi hiyo kwa muhula wa tatu uliibua hisia tofauti tofauti na kuzusha maandamano makubwa.

Waandamanaji wanadai kwamba kwa muujibu wa katiba ya nchi hiyo rais anapaswa kuiongoza nchi kwa mihula miwili tu.

Nayo mahakama ya katiba wameeleza kwamba hawahesabu muhula wa kwanza wa raisi huyo madarakani kwasababu aliteuliwa na wabunge na si kuchaguliwa kwa kupigiwa kura.

Regina Mziwanda kutoka mjini Dar-Es-Salaam amezungumza na msemaji huyo wa serikali ya Burundi ,kutaka kujua Nini ujumbe wa Rais Pirre Nkurunziza kwa taifa la Burundi pindi alipohutubia mapema Jumatano.?

Chanzo: BBC

Mbona hueleweki? Unajuwa wananchi wa Burundi wanachopigania? Nguvu ya umma inataka hata hiyo June asigombee kwa sababu tayari ameshatawala vipindi viwili vinavyotamkwa katika katiba mpya ya sasa. Mahakama inakataa kipindi cha kwanza kuhesabiwa sababu kipindi hicho aliteuliwa, hakuwa amechaguliwa na wananchi. Demokrasia ya wananchi kuchagua rais imeanza ktk kipindi chake cha pili. Maana yake nguvu ya umma haijashinda sababu akichaguliwa June atakuwa anatawala kipindi cha tatu.
 
Back
Top Bottom