Tetesi: Burundi is another Rwanda.

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,113
27,099
Watutsi walivyo fika Rwanda walikaribishwa na wahutu na watwaa na wote kwa pamoja waliishi kwa upendo mkubwa sana.

Wahutu waliwakaribisha watutsi kwa sababu watutsi walisifika kwa kuwa na uwezo mkubwa sana kivita kwa hiyo wahutu waliwatumia watutsi pia kama ngao yao dhidi ya makabila jirani. Waliamini kwa Ku assimilate na watutsi basi hakuna kabila jirani lingeweza kuwasumbua kivita.

Watutsi waliipenda sana jiografia ya Rwanda kwa sababu ilishabihiana sana na jiografia ya mahali walipotoka (Ethiopia/Somalia/Israel?) hususani uwepo wa milima mingi ambayo pamoja na mambo mengine kwao ilikiwa ni nyenzo muhimu sana ya kivita ( Remember our secondary school history famous question why Ethiopia was not colonised and how mountains played a very vital role when they defeated the Italians ?..This is what am talking about here)

So watutsi wakan assimilate na wahutu waka adopt lugha yao kibantu", wakaoleana etc.

Kwa kuwa watutsi walikuwa wamestaarabika zaidi ya wahutu na walikuwa wana mfumo wao wa kiutawala ambao ni utawala wa kifalme , walianzisha utawala wa kifalme na kuishi kwa upendo na umoja na wahutu.

Kama mnavyo jua watutsi ni wafugaji.Kuongezeka kwa idadi ya watu na mifugo kulileta hitaji la ardhi kubwa zaidi kwa ajili ya kuwa accommodate wafugaji na mifugo yao.

Mfalme akatuma ujumbe wa watu kwenda katika maeneo jirani ili kuona kama wanaweza kupata ardhi zaidi .

Safari ya mamesenja hao iliwafikisha hadi katika eneo ambalo ni Burundi ya Leo.

Eneo lilikuwa zuri sana.Inasemekana kulikuwa na watu wa kabila la watwaa..Mfalme alivyo pewa taarifa kuhusu kupatikana kwa eneo hilo alienda kujionea yeye mwenyewe.

Mfalme alivyo fika Burundi alishangaa kuona eneo hilo linafanana kijio grafia kwa kila kitu na Rwanda . So akaliita eneo hilo URUNDI RWANDA yani Another Rwanda au Rwanda Nyingine.

Baada ya hapo sasa watutsi na wahutu kutoka Rwanda wakaanza kuhamia Burundi kwa ajili ya more Green Pastures.

Source: Oral Tradition
 
Back
Top Bottom