Buriani Sheikh Ali bin Mussa Maarufu Sheikh Rocket (1928 - 2026)

Buriani Sheikh Ali bin Mussa Maarufu Sheikh Rocket (1928 - 2026)

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
22,454
Reaction score
32,980
BURIANI SHEIKH ALI BIN MUSSA MAARUFU SHEIKH ROCKET

Naamini hakuna Muislam aliyezaliwa Dar es Salaam au kuishi tu ambae hakupata kumfahamu Sheikh Rocket au kumuona angalau kwa mara moja.

Mimi binafsi yangu nikimuona mara nyingi mitaani akipita amebeba bendera yake yenye maneno: ‘’Laillah Illallah’’ – ‘’Hapana Mola ila Allah’’ lakini mahali ambapo alikuwa hapungui kila anapokuwa Dar es Salaam ni Msikiti wa Mtoro na hapa ndipo nilipomuona mara nyingi akija kusali swala zake na wakati mwingine atasimama na kusisitiza kuhusu swala.

Hii ilikuwa katika miaka ya 1970.

Kitu muhimu ni kuwa Sheikh Rocket alikuwa maarufu misikiti yote ya Dar es Salaam na nilibahatika kwenda hija pamoja na yeye mwaka wa 1998 na hata huko Makka na Madina hakuwa mgeni, alikuwa mwenyeji sana na mahujaji wenzake kutoka Tanzania na wengine kutoka Kenya na Uganda wakimfahamu.

Kulikuwa na uvumi kuwa alikuwa rafiki mkubwa wa Rais Iddi Amin wa Uganda na wanasema watu kuwa alikuwa wakati mwingine akiwa safarini kwenda Hijja hupita Uganda kumsalimia.

Huu ulikuwa uvumi lakini imethibitika kuwa ni kweli Iddi Amin na Sheikh Rocket walikuwa marafiki wakubwa hata baadhi ya wanae walisoma Uganda kwa ajili ya urafiki huu wao.

Wasemaji wanasema Sheikh Rocket alikuwa akienda Hijja kila mwaka.

Mwaka mmoja siku zile watoaji kibali cha Hijja walikuwa BAKWATA peke yao walimnyima kibali cha kwenda Hijja.

Sheikh Rocket akaenda Uganda kwa rafiki yake Rais Iddi Amin akamweleza tatizo lake.

Iddi Amin akamwombea visa na Sheikh Rocket akaenda Hijja.

Sasa msafara wa BAKWATA ulipofika Makka wakamkuta Sheikh Rocket mwenyeji anawapokea na kuwakaribisha.

Ndipo ukatokea uvumi kuwa Sheikh Rocket amepaa na kuingia Makka.

Katika miaka 70 Sheikh Rocket amehiji mara 50 bila ya kukosa hata mwaka mmoja.

Taarifa imenifikia leo asubuhi kuwa Sheikh Rocket amefariki na ataswaliwa Msikiti wa Kitumbini baada ya swala ya Dhuhr kisha mwili utapelekwa Zawiyani, Qadiriyya Mtaa wa Mzizima na Mkunguni na baada ya hapo itaanza safari ya kwenda Mumburu, Mtwara kwa maziko na atazikwa kesho Jumatano.

Sheikh Rocket ana historia kubwa sana katika harakati zake za kuusukuma mbele Uislam na ni kitu ambacho amekifanya maisha yake yote hadi umauti ulipomfika.

Hii Zawiyya ya Kariakoo aliinzisha yeye kwa heshima ya Khalifa wake Sheikh Mohamed Nassoro.

Kila unapomuona Sheikh Rocket basi unauona Uislam.
Sheikh Rocket alikuwa mtu wa maskhara kidogo hasa kwa vijana.

Nakumbuka mwaka mmoja Mwezi wa Ramadhani mkesha wa Laylatul Qadr Msikiti wa Mtoro yeye alikuwa mbele basi akanyanyuka akaja mwisho wa msikiti ambako vijana tukipenda kukaa.

Akasimama mbele yetu anatuangalia kwa kama dakika moja, mbili hivi kisha akasema, ‘’Nyinyi mnaelekea hamswali lakini leo mmekuja hapa kula wali tu, basi muwe mnakuja na kuswali vilevile si mpunga tu.’’

Hapa Maktaba nina picha nilimpiga kwenye Khitma ya Saigon mwaka wa 2010.

Niliposikia kifo cha Sheikh Rocket haraka sana niliingia Maktaba kuzitafuta picha zile na ningependa kuziweka hapa.

Allah amfanyie wepesi safari yake.

1768928182638.png
 
Pole zao wanafamilia na waumini wote wa kiaslam.
Kwa hakika huyu hakuwa shekhe ubwabwa, mashekhe ubwabwa wote utawasikia kila mara katika kutetea uovu wa watawala na CCM.

Huyu, bila shaka sauti yake ilisikika zaidi msikitini alikoendesha ibada.

Basi Mungu wa rehema na huruma, akamjalie pumziko jema kutokana na yale mema na upendo alioutoa kwa wanadamu wenzake.
 
Inna lillahi wainaa lillahi raaajiun

Uislamu hautufundishi kuwa mchafu mchafu kutembea na mishanga shingoni kama mganga
Kutembea na mibendera ya utaifa Ni vitu uislamu umevikemea kabisa

Tunamuombea maghfirah kwa Allah alipokosea

Uislamu ni usafi
 
Back
Top Bottom