Bunju, Boko Traffic wapo, Tegeta kibaoni wapo, Makonde wapo, Mwenge wapo. Kama nchi imefilisika tuambieni

Fedha hizi siku hizi ni sehemu ya 'income' au? kwa kuwa hakuna elimu, hakuna ushauri, hakuna kuonywa! Nahisi siku hizi ni sehemu ya mapato kama yalivyo mapato mengine.
 
Trafiki wapo kwa ajili ya usalama wako, ongezeko lao linamaanisha serikali inajali zaidi usalama wako na ina uwezo mkubwa wa kuajiri vijana wachapakazi.
Tii sheria bila shurti.
Inawezekana huna gari,nakuombea upate hata la mjombaako ndo utawaelewa wanaolalamika,au we ndio hao hao.
 
Sheria zipi kama hata elimu juu ya usalama barabarani siku hizi haitolewi zaidi ya kushika EFD mashine
Yaani wewe una leseni halafu unadai huna elimu ya usalama barabarani? Ulipataje leseni yako? Au wewe ni mmoja wa wale walioletewa leseni nyumbani bila kwenda darasani?
 
Askari kuwepo barabarani ni wajibu wao sasa munataka wakae wapi saazingine tunalalama vitu tusiovijua au tunapenda kulalama
Mkuu una gari?

Baba kuwepo nyumbani ni wajibu na lazima. Lakini usipotimiza majukumu ipasavyo na kwa kadri baba anavyotakiwa kufanya na upuuzi. Ndicho tunacholalama hapa mkuu. Tatizo ni kero tunayopata. Jiulize unasafairi kwenda Tanga umepiga hesabu zako kwa mwendo 100 speed pamoja na vibao vya 50 speed umekadiria kutumia masaa 4. Sasa hawa jamaa wanakusimamisha dakika 30 hadi saa 1. Unategemea nini.
 
Yani hata mimi wananiudhi sana hawa trafic. Kibaya zaidi ukiwa unaenda unasimamishwa wanaomba leseni na ukiwa unarudi hata baada ya dakika 5 watakusimamisha tena wanaomba leseni. Imagine vituo vyote hivyo unasimamishwa. Hasa wale wa bunju B pale wanaboa sana.
 
Back
Top Bottom