BUNGENI: Muswada wa mabadiliko ya katiba

BUNGENI: Muswada wa mabadiliko ya katiba

Mmh nimechoka. Km mswada wa marekebisho ya katiba ndo vile. Na km utasomwa kwa mara ya 2, then waupitishe na rais auridhie. Unadhani hyo katiba itakuwa na tija yoyote kwa wananchi hyo kabla ya 2015?
Mungu ibariki Tanzania.
 
Tunakutegemea Mkuu! Tujuze yanayojiri. Updates Pls!

Kinachoendelea ni utumbo mkuu, tusubiri mchana kwenye mjadala wa mswaada wa katiba tutajuzana kila hatua. Ila kwasasa nitakuwa na weka maji kwenye gunia kama alivyosema member mmoja hapo juu kuwa maswali ni yale yale na majibu yale yale.
 
Nakubaliana na hoja ya Dr Kitila Mkumbo kwamba ama ccm na serikalia yake wafanye kama wananchi wanavyotaka au wanaharakati watuongoze sisi wananchi kuandaa mchakato na hatimaye katiba mpya. Hii inawezekana kabisa na nina hakika hata kama ni suala la gharama wananchi wengi watakuwa tayari kuchangia ili mradi wanajua ni kwa ajili ya katiba wanayoitaka.

CCM wameamua kujitenga na wananchi hivyo hakuna haja ya kuwabembeleza. Kama kweli hawa ccm walitaka maoni ya kitaalam kwa nini wasimuite Prof Shivji badala ya huyo kilaza ambae wamekuwa wanamtumia kila mara. Huyo Prof Kabudi ana tofauti gani na yule Dr Conrard Murray aliyempa Michael Jackson madawa kinyume na taratibu na maadili ya taaluma yake? Ni aibu huyu Prof kulamba miguu ya ccm inakufa.
 
Wanabodi wenye access na TBC, angalieni TBC Live kipindi cha Jambo Tanzania. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Warema na Waziri Stephen Wasira, wanahojiwa live kuhusu kuwasilishwa Muswada wa Sheria wa Kuundwa Tume ya Kukusanya Maoni ya Kubadilisha Katiba.
Werema na Wasira ni vilaza.
 
Kinachoendelea ni utumbo mkuu, tusubiri mchana kwenye mjadala wa mswaada wa katiba tutajuzana kila hatua. Ila kwasasa nitakuwa na weka maji kwenye gunia kama alivyosema member mmoja hapo juu kuwa maswali ni yale yale na majibu yale yale.

Hata fedha ikipatikana watu hawatengenezi au hawaifanyi miradi inavyotakiwa sababu ya kutaka cha juu kila kona, matokeo yake ndo kurudia rudia kufanya vitu vile vile kwa kutumia watu wale wale. Hapo ndo nachoka na viongozi wetu, sijui huwa hawajionei wanapofanya safari za nje tena mara kwa mara. Wanadhani walifika hapo wenzao kwa porojo na kutegemea misaada bila mikakati ya maana.
 
Huyu ni Mwanasheria Mkuu wa ajabu sana. Yaani hawa wote wanaopinga ni wajinga isipokuwa wao tu ndio wapo sahihi? Shivji, Kanywanyi, TLS, Jukwaa la Katiba, na wananchi wengine wote hawajui wanachokipinga?

Mimi nafikiri hatua iliyobaki ni moja, nayo ni wanaharakati wote na vyama vya upinzani kuibuka na mchakato sambamba na ule wa serikali ambao hawa bwana wamekamia kuupitisha wiki hii. Kisha kukusanya maoni sambamba na hiyo tume ya kwao na kuibuka na rasimu ya katiba mbadala. Itakapofika wakati wa kura ya maoni, ifanyike kampeni ya kura ya 'HAPANA' dhidi ya kura ya 'NDIYO' ya serikali.

Dr. hili naliunga mkono. ukisikiliza mijadala mbalimbali utagundua wengi wanapinga tu bila kutoa mawazo mbadala yanayotekelezeka. ni vyema wanaharakati watoe mchakato mbadala nao ujadiliwe kama inawezekana. unaweza kuwa unatoa options ambazo hazipo. lazima pia watu wajue kwamba Tanzania ipo na serikali ipo na hata tume itakayoteuliwa na yoyote bado italipwa na serikali (CCM) pia bunge (75% CCM) lililopo litahusishwa. Hivyo influence ya CCM ni vigumu kuepukika.
MKJJ anasema itakuwa ya CCM well, namna gani litaepukwa hilo labda ni kuwaacha wafanye wamalize then katiba za vyama vingine zitakuja kuundwa hapo watakaposhika madaraka
 
Tatizo la 'watawala' wa Tanzania hujidanganya kuwa wao wana akili kuliko 'watawaliwa' na hivyo hupuuza matakwa halisi ya 'watawaliwa'. Matokeo yake 'watawaliwa' wakichukua hatua utasikia visingizio visivyo na maana kutoka kwa 'watawala'. Hii ilitokea Mbeya ambako Kandoro"mtawala" haamini wamachinga wangeweza kugoma na kukataa ukandamizaji dhidi yao bila kuchochewa! Vichwa maji kama Werema na Tysoni wanataka kutuletea balaa ktk nchi hii na baadae waanze kutafuta mchawi!
 
nenda sikiliza bunge live kupitia TBC Taifa kwenye internet live bila chenga
 
Hivi kweli Prof. Shivji na Kanywanyi hawajui muswada huu unahusu nini? au Werema na huyo Tayson wameamua kuwaponda hadharani wanataaluma hao?
Mkuu Avatar yako nimeipenda. Huenda.
 
Mtujuze wengine hatuna access na tv...decoder imecorrupt huku
 
Hadi sasa huu muswada ni wa kurekebisha katiba na sio kwa kutunga katiba mpya. Kwa Werema kuutetea ni sawa kabisa maana tangu hapo awali alisema waziwazi kuwa katiba ya sasa haina shida kama kuna jambo la kurekebisha basi watu waseme na litarekebishwa. Maneno haya ya Werema pia yalisemwa na Celina Kombani.

Kwa hiyo Serikali ya ccm haina nia ya kuandika katiba mpya - that's very obvious. Kama walikuwa na nia ya kuandika katiba mpya kwa nini hawataki kusikiliza maoni ya wananchi? Ni kitu gani kinawafanya watake kusoma huu muswada kwa mara ya pili? Ni ni lini muswada wa KUTUNGA katiba mpya uliwahi kupelekwa bungeni? Ule mwingine ulipelekwa tena kwa lugha ya kiingereza ulikuwa wa KUREKEBISHA katiba.

Naye Steven Wasira na utaalam gani kwenye mambo ya katiba kiasi kwamba ccm wanamtumia kuhubiri huu muswada uliojaa matatizo? Kwa nini watu kama Wasira na Werema wanajiona wanajua mambo ya katiba kuliko Prof Shivji? Shida kubwa ninayoona ni kwamba kuna gap kubwa sana kati ya ccm na wananchi. Wakishapata Ubunge hawa ccm ni kama wanajigeuza baraza la mawaziri tena mawaziri wasiosikiliza wale wanaowaongoza. Huu muswada unaweza kuipeleka kuzima ccm mapema kuliko ilivyokuwa iwe.

Ningeomba kuuliza, Spika wa bunge ana uwezo/nguvu gani katika hali kama hii ambapo serikali inaonekana waziwazi kwenda kinyume na public interest?

Mkuu umeshamaliza kuwa CCM haina sababu na nia ya kubadili katiba kwa sababu katiba ya sasa unawanufaisha sana. Kuhusu uwezo wa Spika kuithibiti serikali juu ya mwenendo wake juu ya katiba mpya ni kwamba hana sababu, nia, wala uwezo wa kufanya hivyo. Ni usanii mtupu.
 
Jamani naomba mnisaidie, mswada ukisomwa kwa mara ya kwanza au ya pili, what are the effects
 
Huyu ni Mwanasheria Mkuu wa ajabu sana. Yaani hawa wote wanaopinga ni wajinga isipokuwa wao tu ndio wapo sahihi? Shivji, Kanywanyi, TLS, Jukwaa la Katiba, na wananchi wengine wote hawajui wanachokipinga?

Mimi nafikiri hatua iliyobaki ni moja, nayo ni wanaharakati wote na vyama vya upinzani kuibuka na mchakato sambamba na ule wa serikali ambao hawa bwana wamekamia kuupitisha wiki hii. Kisha kukusanya maoni sambamba na hiyo tume ya kwao na kuibuka na rasimu ya katiba mbadala. Itakapofika wakati wa kura ya maoni, ifanyike kampeni ya kura ya 'HAPANA' dhidi ya kura ya 'NDIYO' ya serikali.

Hapo umenena. Hatuwezi kupata katiba yenye kuashiria matarajio ya Watanzania wa leo na vizazi vijavyo kwa kutumia serikali hii na bunge la sasa.
 
Kwani katiba ya CCM iliindwa kwa mamlaka ya Mwenyekiti wao? Kwani katiba ya CDM imeundwa na Mwenyekiti wao? Siku katiba hizo zikibadilishwa zitakuwa zimebadilishwa na wenyeviti wao? Vipi TAnzania? Mwenye mamlaka ya kubadilisha katiba ni nani? Ni rais au Wananchi?. Vipi RAis atuundie hata utaratibu wa kukusanya maoni? Vipi aweke mipaka hata ya kupinga watakachofanya wakusanya maoni hata kama ni kibaya kwenye katiba hiyo? Vipi tutumie pesa nyingi kupata katiba ambayo nayo haikidhi matakwa tegemeo la wananchi wenye mamlaka nayo? KAtiba kama Job description kati ya Mwajiri na mwajiriwa; RAis na Wananchi nani mwajiri na ninani mwajiriwa? Vipi Mwajiriwa aamue job description yake juu ya mwajiri?
 
Jamani naomba mnisaidie, mswada ukisomwa kwa mara ya kwanza au ya pili, what are the effects

Kwa mara ya kwanza ukisomwa maana yake utarudi kwa wananchi waujadili, waanalyse mapungufu nk. Then ndo urudi bungeni kusomwa kwa mara ya pili ukiwa umerekebishwa kwa kuzingatia maoni yote yaliyotolewa.
Kwa mara ya pili, maana yake utasomwa, utajadiliwa na wabunge tu, then wataupitisha then rais atauridhia kwa kuusaini kuwa sheria. Or wabunge wanaweza kuukataa, lakini si kwa bunge letu.
Nielewavyo mimi.
 
Jamani naomba mnisaidie, mswada ukisomwa kwa mara ya kwanza au ya pili, what are the effects

kwa namna ninavyojua mimi' inabidi usomwe mara tatu' baada ya hapo unajadiliwa na kupitishwa kuwa sheria.Kumbuka kila unaposomwa lazima ujadiliwe,swali linakuja je ulivyosomwa mara ya kwa ulijadiliwa? Kilichofanyika,mswaada haukujadiliwa ila iliamriwa urudishwe uandaliwe uwe wa kiswahili kitendo cha kung'ang'ania ujadiliwe kwa mara ya pili wakati haukujadiliwa kwa mara ya kwanza unapunguza nafasi ya kupata maoni na mapendekezo toka kwa wabunge na wananchi!
 
WEREMA AMEFIKIA HATUA YA KUMTUKANA MWALIMU WAKE ILI AMTETEE JK NA MAFISADI WENZAKE ??KWELI MTU HUYU NI HATARI ANAWEZA KUFANYA JAMBO LOLOTE ILIMRADI UBINAFSI WAKE NA MARAFIKI ZAKE UFANIKIWE,HANA AIBU NA WALA STAHA HANA NI MTU HOVYO NA HUONGEA HOVYO KWA UDANGANYIFU WA HALI YA JUU,GEORGE NI JINGA KABISA HATA UKIANGALIA SURA YAKE NI ABNORMAL KWA HIYO SIWEZI MLAUMU SANA ILA WEREMA NI MUONGO NA HANA AIBU ANAWEZAJE KUMTUKANA MWALIMU WAKE KWELIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII MWALIMU ANADHALILISHWA KWA AJILI YA NJAAA ILHALI UKWELI UNAUJUA

ndugu yangu rudi nyuma na ukumbuke ulipokuwa unavaa malapa yaliyotoboka pale mlimani
 
Kwa sasa Werema, akili na busara zake kaweka pembeni kabisa na anachofanya sasa ni kutumia kwa kutumia tumbo lake, haiwezekani watz wengi wanaowakilishwa na wanaharakati, na wasomi anaowaponda wasiwe na uwezo wa kujua na kutofautisha masuala.

Kuanza kushambulia watu kwa mtu mwenye elimu kubwa kama Werema ni sababu ya kuishiwa hoja na ukweli uwa sasa wananchi wakishirikiana na wanaharakati wenye mapenzi mema ya nchi hii wanawapiga kina werema&co chini ya mkanda
 
inasikitisha sana mtu kuwa mwanasiasa anajifanya yeye ni kila kitu, mbona tunao wabunge waganga wa kienyeji, darasa la saba kama kile kibajaji na vikaragosi kama wasira. wanasiasa acheni ujinga wa kujifanya mnajua kila kitu. Kwa taarifa wassira hupaswi kujilinganisha na prof SHIVJI kwa jinsi jamii inavyomuheshimu. unatia kichefuchefu
 
Back
Top Bottom