crome20
JF-Expert Member
- Feb 5, 2010
- 1,247
- 888
Hebu tuwekane sawa. Uongo ni jambo baya na vitabu vitakatifu vimetuonya. Sasa fikiria ukimwambia mtoto kuwa usipokula ntamuita mbwa akung'ate masikio, hapo utakuwa umesema "Uongo" maana huwezi kufanya hivyo. Ukimwambia ingia ndani, nje kuna Simba watakumeza, umesema UONGO. Je tuseme huu kweli ni uongo? "Uongo" wenye tija ya kuokoa na kujenga huwezi ukauita uongo maana kazi ya uongo ni ya shetani na ni kwa ajili ya kuleta madhara kwa mtu mwingine ili mwingine afaidi. Kwa mantiki hiyo askari kuvujisha siri za kuwadhibiti CDM si usaliti bali uzalendo, maana kazi ya polisi si kuidhibiti CDM. Hiyo ni mikakati ya kiovu ya watawala na mawakala wa CCM. Kuvujisha siri hizo ni uzalendo kuhakikisha maisha na mali ya Watanzania wakiwemo wafuasi wa vyama vinalindwa. Hebu kuwa Great thinker bwana.
Mkuu, huo sio utiifu bali ni usaliti. Mtu wa namna hiyo ambae ana kiuka maadili ya kazi yake na kukiuka kiapo chake, kwa kuvujisha mambo ya jeshi ni MSALITI. Kwa sasa mnaweza kuwafurahia, ila kumbukeni dhambi ya usaili haipotei, itaendelea kuwatafuta tu.