Bungeni: Msigwa aongea 'point'

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2011
Posts
7,146
Reaction score
3,829
Kwa mara ya kwanza tangu nimfahamu mhe Msigwa, leo nimeona ameongea kwa staha na utulivu wa hali ya juu alipokuwa akiuliza swali kwa waziri wa mambo ya ndani kuhusiana na kujenga na kuboresha makazi ya jeshi la polisi nchini.

My take;

Leo nimeamini kuwa ile chuki kwa jeshi la polisi inayo aminiwa kutawala kwa wapinzani ni geresha tu, ukweli ni huo alioutoa Msigwa kuwa ana wajali na kuwathamini polisi wetu, iweje mashabiki wa CHADEMA mjenge chuki na jeshi la polisi?
 

Hakuna anaye wachukia polisi, Tunawachukia wanaowatuma na kuwashikiza poilisi kuuwa raia wema!
 
Kwani POLISI ni wabaya, ni hao wakuu wao wanaopokea maelekezo ya kijingo toka kwa watawala na kuwapa amri polisi kutekeleza uvunjifu wa sheria na amani. Usituletee maneno ya Mh. Lukuvi wakati mnajua Jeshi la polisi hivisasa linaongozwa na IGP Mwigulu Nchemba.
 
Hata wewe polisi unayetumwa kuua hivi huwezi kutumia akili zako kidogo kufikiri??
 
Msigwa siku zote anaongea point tupu. Ni mtu anayesema Facts zaidi na sio myths.

Kumuita Kinana jangili nayo point? kushika biblia bungeni huku akishusha matusi kwa watawala nayo point? kwa hili la leo nimempa viji-credit kidogo na ningependa wapinzani wengine wafuate mwenendo huo wa Msigwa!!
 

Acha kumvunjia heshima IGP Mwema, hakuna mtu asiye jua kuwa Mwema ni jembe, makosa ya kiufundi yanayo endelea kwa sasa ni mapungufu tu ya kiutendaji. Ifike wakati tujifunze ku-appreciate.
 
Acha uzushi wewe gamba,sio polisi wote ni mandondocha ya magamba wapo waadilifu!!Tuna ugomvi na watu kama akina kamhanda na vibaraka wenzao wanajijua....

Kwa kuongezea ni kwamba vita iliyopo ni ya mfumo wa jeshi la polisi ambao kama utawekwa vizuri mambo yatakuwa shwari kwani polisi kama individual ni vijana wetu na ni ndugu zetu ila wanafanya mambo hayo kutokana na mfumo wenyewe mbovu, hii inanikumbusha story ya Malcom X alivyokuwa anawachukia wazungu kwa rangi yao akiamini kama ni wabaguzi though kulikuwa kuna ambao hawana chembe ya ubaguzi but alipoenda Mecca kuhiji akakutana na watu wa mataifa mbalimbali weusi kwa weupe na wote wanajichanganya kwa pamoja, na alipotoka huko akabadilisha approach kwa kutambua kwamba kumbe tatizo ni mfumo na si individuals. Back to the point, issue hapa ni kuboresha mfumo wa jeshi ili utekeleze majukumu yake pasipo matakwa ya kiasa mwisho wa siku haki itendeke kulingana na sheria zilizopo na si kwamba kama mnapigania mabadiliko katika jeshi la polisi basi askari wasitetewe kisa jeshi halikubaliwi.
 
Kumuita Kinana jangili nayo point? kushika biblia bungeni huku akishusha matusi kwa watawala nayo point? kwa hili la leo nimempa viji-credit kidogo na ningependa wapinzani wengine wafuate mwenendo huo wa Msigwa!!

Kwani bungeni ni nyumba ya mungu?mbona watu wameshika biblia mara kibao bungeni wa kiapa karibu kila awamu lakini mwisho wa siku wanasafirisha mpaka wanyama hai alafu wanatuzuga hawafahamu hao wanyama wamekwenda kwa nani mpaka wanaomba msaada kwa serikali huko uarabuni wakati airport msafiri wa kaaida tu akibeba lotion inatolewa sembuse wanyawa. Biblia na misahafu inayoshikwa pale ni utamaduni tu kwani wengi pale katika maisha yao mtaani kabla ya kuingia bungeni walikuwa hawashiki wala kuwa karibu na vitabu hivyo vitakatifu.
 
alishughulikiwa vizuri siku ile alipofanya vurugu iringa ndio mana amepata adabu
 
Kumuita Kinana jangili nayo point? kushika biblia bungeni huku akishusha matusi kwa watawala nayo point? kwa hili la leo nimempa viji-credit kidogo na ningependa wapinzani wengine wafuate mwenendo huo wa Msigwa!!

Kwa hivo Kinana sio jangili?
 
We hukijui kilichomkuta msigwa alipokuwa lockup, kachezea kichapo na kapigwa mkwara mkali sana, tokea siku ile ana adabu.
 
The only thing you dont know, ni ukweli kwamba baadhi ya hao polisi ndiyo wanatupatia siri za ndani kabisa za jeshi la polisi. Wewe unafikiri huwa tunajuaje mipango yenu ya kuihujumu chadema? Kuna polisi ambao ni watiifu kwa CHADEMA na hao ndiyo tunaowahurumia.
 

Mkuu, huo sio utiifu bali ni usaliti. Mtu wa namna hiyo ambae ana kiuka maadili ya kazi yake na kukiuka kiapo chake, kwa kuvujisha mambo ya jeshi ni MSALITI. Kwa sasa mnaweza kuwafurahia, ila kumbukeni dhambi ya usaili haipotei, itaendelea kuwatafuta tu.
 
Mashabiki wa CHADEMA wala hawana chuki na polisi isipokuwa ni pale wanapo jua kuwa wana haki ya jambo Fulani lakini polosi hawataki haki hiyo itimizwe, kila mtu anajua umuhimu wa polisi lakini polisi wanapoamua kuwa vibaraka wa CCM hapo ndipo fujo huzuka
 

Mkuu, nakubaliana na wewe kuwa wengi wa wabunge huko walikotoka hawakuwa kwenye misingi hiyo ya imani, hivyo kuwapa vitabu vitakatifu inaweza isiwe na tija. Ila nadhani una mfahamu Msigwa, huyu ni mchungaji, ana ongoza wana kondoo wa bwana, iweje yeye awe kinara wa matusi awapo bungeni? au akiingia bungeni ndio kuna ukomo wa uchungaji wake?
 
Siyo usaliti bali wamechoka kutumiwa na CCM kwa mambo ya kisiasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…