Bungeni Kuna Nini

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
219
Nimekuwa nikijiuliza kuwa huko bungeni huwa kuna nini kinachowafutia wa watanzania wengi wapende kuwa wawakilishi wa wananchi/wabunge??????Unakuta mtu alikuwa Mkurugenzi wa shirika kubwa,au mwalimu wa chuo kikuu kama mwaliosi,mwandosia ,mlingwa,mwakiembe , au padri kanisani kama Silaa,au mfanyabiashara mkubwa kama dialo na karamagi au hata waliofeli na kupata division zero kama sendeka Moringe sec wanakuwa wabunge. Hivi kweli wote hawa lengo lao ni kuhudumia wananchi au ni njia za kuboresha maslahi yao binafsi kupitia tiketi ya ubunge.Kuna wakati nilikuwa katika eneo la chuo kikuu nikasikia wahudumu katika idara moja wakiongea kwenye corrido kwamba malechara wengi wanakimbilia bungeni kwa matumaini kwamba watapata uwaziri na ikishindikana watapata japo unaibu.bora hawa wenye vyeti vyao lakini ni kweli kuwa hizo wizara zitatosha!!! wakikosa nasikia ni vifitina mtindo mmoja Hili kundi jingine la waliopata zero ni wizara gani unadhani wangeweza kuongoza!!!zamani sana niliwahi kuishi Arusha,miaka hiyo ndio Mrema na Elisa molel waalikuwa kama na miaaka mitatu katika ubunge wao arusha, ,hadi leo ni zaidi ya mika 10 wapo madarakani,ila wananchi wanawalaini ila dua la kuku halimkuti mwewe,hawajafanya jambo lolote katika majimbo yao wao huwa wanasubiri bunge wakachukue hela wakati wakipiga ndogo ndogo kusaka uwaziri au unaibu waziri. Sasa tujiulize je nchi hii ina hitaji mawazi wa ngapi?na je kama jimbo limekushinda ukipewa wizara utaweza au ni ili mradi tu uwe umeboresha maslahi binafisi?Hawa ni watu ambao ni wa binafsi tena huwa wanatumia rushwa kubwa sana kushinda uchaguzi.Mfano Elisa mollel uchaguzi ukifika huwa ananunua katiba za jamuhuri ya muungano nyingi kwa ajili ya wajumbe halafu kabla hajawagawia anaweka hela za kuwaonga ndani ndio anawapa.Bila aibu aliwahi kusema kwenye kampeni kuwa yeye huwa anachaguliwa na hela zake na sio wananchi kwa hiyo wewe kama hutanipa kura yao nitashinda tu?Je kweli tutafika? Sasa tujiulize huu mgawanyiko uliopo ndani ya CCM chanzo chake ni nini kama sio hizo fitina za kwa nini sijapewa uwaziri,na hata wale waliopewa uwaziri bado wanaandamwa na waliokosa.Hii hii ni maskini sana na sio rahisi kila mbunge awe wazari,mimi nawashauri CCM wakae chini wa shikamane wateleze ilani ya uchaguzi kama walivyotuhaidi tukawapigia kura ili waweze kuinua maisha ya mwananchi wa chini Wakiendelea na haya majungu na malumbano tunakosa imani na chama na nibora wawape upinzani nchi mapema,malechara warudi vyuoni kufundisha na wasio kuwa na vyeti wakaresiti mitiahani halafu wajipange umpya kuomba tena kura.
 
SHY,
Nimekuwa hata mie nawaza as you did here. Ninadhani iwe specific ktk katiba aina ya wizara tunazohitaji na idadi yake, ila kama kuna mabadiliko ni kuunda idara au kuhamisha idara na siyo wizara. Hii inachanganya sana ktk utendaji maana utakuta sekta zinapigwa danadana kila baraza jipya linapoapishwa.

Kuhusu Bungeni, Nadhani kuna tatizo somewhere ambapo sasa matajiri ndio wanaopata nafasi, Hata chama Changu (CCM) kimekiri kuwa matajiri wananyemelea kukitamalaki kabisa, Naunga mkono kauli ya Muungwana kuwa siasa na biashara si vyema vikawa ktk bakuli moja.

Yote tisa, kumi ni kumpunguzia madaraka Rais na pia baadhi ya kinga zake kuziangalia ili kwa kuwa yeye anahimiza maadili basi awe namba moja ktk maadili na si madili. Na Bunge lipewe uwezo wake sasa wa kutunga sheria na si kupitisha sheria.
 
Back
Top Bottom