Eee kweli Nchi hii imefikia pabaya sana...Watu mnaakili zenu wasomi na professions zao mnashabikia mambo ya kipumbavu! Lema kubweka kijinga bungeni mnaona kafanya la maana? CDM nawajua sana, Lema na Mbowe nawafahamu sana. Nimetoka jimbo la Hai...kampeni yake nilishiriki lakini wakati huo huo namfahamu Lema personaly. Lakini siungi mkono upupu huo wa Lema maana sio ya kiistaarabu. Tunahitaji mabadiliko ya kweli na hatukubaliani na upindishaji wa kanuni pindishi zinazofanywa na wana ccm lakini pia hatukubaliani na namna CDM inavyowasilisha mambo kwa nguvu badala ya nguvu ya hoja! Ninyi mnaoshabikia mambo haya ya kipuuzi ndio mtakaopelekea nchi yetu tukufu katika machafuko! Tupambane katika kutafuta haki na mabadiliko ya kweli lakini tuongozwe na ustaarabu, hekima na busara...Hakika tutafika na ushindi ni Hakika!