Bungeni, Dodoma: Kikao cha kwanza Bunge la 13 mwaka 2018

Bungeni, Dodoma: Kikao cha kwanza Bunge la 13 mwaka 2018

hugochavez

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2013
Posts
1,907
Reaction score
1,009
Analiongoza spika mwenyewe Job Ndugai na katika shughuli muhimu za leo ni viapo vya wabunge waliochaguliwa hivi karibuni.fuatilia

=====

Wabunge wa CCM Themotheo Mzava wa Korogwe Vijijini, Mwita Waitara wa Ukonga, Julius Kalanga wa Monduli na Zuberi Kuchauka wa Liwale wamekula kiapo cha Uaminifu mbele ya Spika Ndugai

Wabunge wa upinzani isipokuwa baadhi ya wa Chama Cha Wananchi (CUF) kambi ya Ibrahim Lipumba wamesusia zoezi la kuapishwa wabunge wanne wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliochaguliwa hivi karibuni.

----
Anthony Mavunde
Serikali inaona umuhimu wa kuendelea na utaratibu wa kuukimbiza Mwenge wa Uhuru nchi nzima kila mwaka ili uendelee kufanya kazi ya kuimarisha misingi ya taifa letu na kuhamasisha maendeleo ya wananchi

Kandege
Serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 4.2 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vituo 9 vya afya katika mkoa wa kigoma

Hatua za awali za kuanza ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Kakonko zimeanza ambapo eneo la hekari 32 limetengwa kwa ajili ya ujenzi huo

Dr. Faustine Ndugulile
Kwa sasa Serikali inaendelea kuifanyia maboresho Hospitali ya Kibena kwa kufanya upanuzi wa jengo la radiolojia ili kusimika mashine mpya,ujenzi huo utagharimu shilingi 39,750,000

Katika Mwaka wa Fedha 2018/19, Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 7 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe kwa kujenga jengo la X-ray, jengo la upasuaji, jengo la uchunguzi wa maabara na la kuchomea taka hatarishi

Merry Mwanjelwa
Serikali imedhamiria kuvikarabati vyuo vya kilimo kupitia Programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) ili viweze kutoa mafunzo ya kilimo kwa ufanisi, Mwaka 2018/19, jumla ya sh. Bil.4 zimetengwa kwa ajili ya ukarabati huo

Mgumba
Serikali kupitia vituo vyake vya utafiti inaendelea kufanya utafiti wa mbegu bora za alizeti ambapo tayari aina tano za mbegu zimesajiliwa

Subira Mgalu
Serikali inatekeleza ujenzi wa mradi wa kusafirisha umeme wa North West Grid kV 400 kutoka mkoani Mbeya hadi Kigoma wenye urefu wa KM 1,372,mradi huo utagharimu Dola milioni 455

Serikali imeanza utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme wa MV 45 kwa kutumia maporomoko ya maji ya mto Malagarasi unaotarajiwa kujengwa katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2019/20 na kukamilika 2020/21 .

---
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amewasilisha Bungeni Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/20.

Mpango huo umewasilishwa Bungeni ili uweze kupokelewa,kujadiliwa na kutolewa maoni na ushauri kwa ajili ya kuandaa Mpango wa Maendeleo wa Taifa na kuboresha Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali ya mwaka 2019/20.

​
 
Wabunge wanne wameshaapishwa. Waitara, kalanga , wa korogwe na kuchauka
 
Asubuhi hii katika kipindi cha maswali na majibu Mtulia alikuwa akiuliza swali la nyongeza kuhusu mwenge wa uhuru!
Alianza kwa kueleza kuwa "kwakuwa serikali imekiri kuwa mwenge ulikuwa na umuhimu kati ya mwaka 64 na 92,na kwakuwa Mwenge umepoteza mvuto na kuhudhuriwa na wanafunzi na watumishi wa serikali,kwakuwa watumishi wamekuwa wakilazimishwa kukesha kwenye mwenge hivyo kuhatarisha ndoa zao,na kwakuwa kwenye Mwenge kumekuwa sehemu inachochea kushamiri kwa ngono na kuongezeka maambukizi ya VVU,naomba kuuliza swal................!"

Spika amkatisha:Hakuna swali,tuendelee na mheshimiwa.........!

UPDATE:Ni "Mtolea" na si "Mtulia"!
 
Hii sharia mpya ya pension inayotaka kupitishwa na bunge ikoje!?
 
Wameanza kuogopa mapema tu hivi. 😁😁😁
Huu mchezo wa nunua nunua wapunzani kuna siri nzito nyuna ya vyama Hivi vya upinzani..
 
alijisahau kuwa saizi anatakiwa kuunga mkono juhudi
 
Asubuhi hii katika kipindi cha maswali na majibu Mtulia alikuwa akiuliza swali la nyongeza kuhusu mwenge wa uhuru!
Alianza kwa kueleza kuwa "kwakuwa serikali imekiri kuwa mwenge ulikuwa na umuhimu kati ya mwaka 64 na 92,na kwakuwa Mwenge umepoteza mvuto na kuhudhuriwa na wanafunzi na watumishi wa serikali,kwakuwa watumishi wamekuwa wakilazimishwa kukesha kwenye mwenge hivyo kuhatarisha ndoa zao,na kwakuwa kwenye Mwenge kumekuwa sehemu inachochea kushamiri kwa ngono na kuongezeka maambukizi ya VVU,naomba kuuliza swal................!"

Spika amkatisha:Hakuna swali,tuendelee na mheshimiwa.........!
Ukikubali kuolewa sharti ulale bila chupi
 
Suala la mwenge ni mambo ya deep sio la mzaha ndio maana magu hajataka kuzuia harakati hizo
 
Ni baada ya kupewa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza, Mtulia alianza kwa kuelezea jinsi ambavyo mwenge huo umepoteza mvuto kwa wananchi na wahudhuriaji wengi wamekua ni wanafunzi, wafanyakazi wa serikali na madiwani, pia akawa anaelezea athari za mikesha ya mwenge na alikua anaelekea kuelezea zaidi athari zake lakini kabla hajaenda kwenye lengo (swali lake) Spika akaamulu akae na kwamba hilo sio swali. [emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom