Bunge na wabunge 19 waliofukuzwa uanachama CHADEMA

Papa1

JF-Expert Member
Apr 21, 2012
1,943
2,000
Nimeona mwongozo wa spika kwa viongozi wa vyama vya siasa kuhusu kufukuza wanachama wabunge.

Naona huyu bwana anataka kuujulusha umma kuwa wabunge ni wanachama wa vyama wa daraja la kwanza ambapo wakifukuzwa sharti makosa yao, vikao vya kuwafukuza, wajumbe waliohudhuria, rufaa zao za mavazi zote ikiwa na maana ya kwamba kama wabunge hao wameenda mahakamani, basi hukumu ziambatanishwe kwenye barua ya kumtaarifu spika kuhusu jambo hilo.

Mimi naona ukakasi sana kukubaliana na jambo hilo kwa sababu zifuatazo:

1) Spika anataka kutueleza kuwa anajua kuzisoma katiba za vyama husika zaidi kuliko waliojiandalia katiba zao? Kama shida ni Katiba, basi utaratibu uwe kwamba kila chama chenye wawakilishi bungeni kupelekea nakala moja ya chama, basi! Sio kwamba jana nifukuze mwanachama nikupe katiba na mitahasari ya vikao, leo nifukuze mwingine, kesho na kesho kutwa naleta katiba, hilo kabati si litajaa makatiba?

2) Hivi Spika anaweza kukataa maamuzi ya vyama kwamba wameonewa hivyo wasifukuzwe na kwa hiyo waendelee kuwa wanachama ili waendelee na ubunge wao? Kwa hiyo Spika ni ngazi ya juu ya maamuzi ya vyama?

3) Hivi Spika anaposema mpaka ajiridhishe kwa muda autakao yeye, kwamba si lazima leo au kesho hivyo tumuache yeye ni mzoefu, ataamua muda atakaotaka, itakuwaje akikuta anaowatetea ni waharifu wa makosa ya jinai ya kughushi nyaraka na huku kesha wapa mikopo, mishahara na posho kibao kwa pesa za walipa kodi? Inatofauti gani na mkurugenzi anayelipa mishahara hewa au anayelipa waliofoji vyeti?

4). CHADEMA walipowafukuza wanachama wao na kutangaza hadharani walipaswa kwenda kila taasisi kupeleka tuhuma, mjadala wa makosa, vikao, rufaa na maamuzi ya mwisho ya rufaa zao na katiba ya chama? Kama wamechukua mikopo Benki wapewe nakala, kama wamepanga nyumba nakala, msajili wa vyama nakala, polisi nakala?!?! Iko hivyo kweli?

5) Hivi CHADEMA wakifukuza mwanachama wake aliyekuwa mbunge na kuutangazia umma, halafu taasisi yeyote huku ikijua kuwa huyo si mbunge tena ikaamua kumpa prevalage za kibunge mfano Diplomatic Passport au kumkopesha gari, ikitokea ndivyosivyo kwenye biashara hiyo CHADEMA itahusishwa kwa makosa yaliyofanywa na mwanachama huyo? Ikitokea tatizo la kinidhamu la wabunge hawa kwa Bunge au serikali, CHADEMA itahusishwa?

Hitimisho:
Mimi nadhani CHADEMA wajikite kwenye wanachama kufoji nyaraka kujipatia ubunge, wamefukuzwa uanachama, wameutangazia umma kuwa si wanachama wao. Sasa wakifanya lolote kwa utambulisho wa uanachama wa CHADEMA hiyo ni jinai. Wawashtaki kwa kughushi nakutumia uanachama kwa maslahi yao. Waachane na spika. Yeye akitaka kuendelea nao kwa njia haramu basi!

CHADEMA chagueni wabunge viti maalumu, peleka kwa tume ya uchaguzi na anzisha madai ya nafasi zenu bungeni.
 
Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,382

Ndugai huenda kuna kitu "alifanzwa" kwenye kichwa kule India wakati anatibiwa si kwa akili zile!!! Ameligeuza bunge kuwa MAHOKA!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom