Bunge na muonekano wa rangi nyekundu

ubuntuX

JF-Expert Member
Aug 18, 2014
1,977
2,200
wakuu

Bunge ni chombo kikubwa sana katika nchi hii pia kinaitambulisha taifa kwa muonekano wake tu

nimekuwa nikijiuliza sipati jibu huku tu muhimili ulioenda chini katika serkali hii ukiongozwa na rais unabendera yenye rangi zinazoelekea sawa na zile za taifa

Muonekano wa bunge la Tanzania ukiingia ndani limetawaliwa na rangi nyekundu, viti na zuria lilotawala bunge linarangi nyekundu!

hii rangi imepoteza kabisa rangi za taifa bungeni, ingefana zaidi tungewekewa miongoni mwa rangi zetu pendwa ndio zitawale ambazo ni Nyeusi, njano, bluu na kijani

Nyekundu inawakilisha nini bungeni katika taifa hili lenye rangi zake?

ni nani aliyesanifu na kupendekeza rangi nyekundu isiyo na picha nzuri, mvuto na maana yoyote kwa taifa hili
 
Wazo Lako Linaweza Kuwa Zuri Kutegemea Na Mtazamo Wako, Hatujui Unawaza Nin. Km Ungelipeleka Kwenye Jukwaa La Mitindo Na Urembo Au Jukwaa La Engineering Tech Kule Labda Watu Wangehc Unazungumzia Rangi Kwa Design2 Ya Ndani Ya Jengo. Tatizo Wazo Lako Umeliweka Jukwaa La Siasa, So Watu Wanaamini Unamashaka Na Hyo Rangi Labda.
 
Mleta uzi, kwa nini usiutafute uhalali wa rangi nyekundu kutumika bungeni hasa katika zulia na viti? Hivi unadhani kuupamba ukumbi huo kwa rangi za bendera ndiyo kutaongeza uzalendo? Halafu nyakati zingine tujiongeze. Hivi ukifikiria ukumbi uwe wa rangi nyeusi tii, utaonekanaje? Kila sehemu tukiweka rangi zilezile mbona zitachusha? Hata hivyo upangiliaji wa rangi unahitaji utaalamu.
 
Maana yake Ccm wanategemea majini.majini wanapenda rangi nyekundu Mtu mzito mm na mshana jr ndio tunaweza kuelewa
Wanajitia kumtukana jamaa lakini akija Mshana Junior hapa akasupport na kufafanuavwote wanatulia, kuna vitu vina ukweli ni bora uhoji wazo hilo kwanza kiutafiti ndipo ujue ama ukubali ama ukatae, unaweza ukapangiwa facts na wanaoelewa, wakakuporomoshea maevidence usiyoelewa mpaka ukakubali hoja,
 
Kweli, mleta uzi, fanya utafti kwanza ili kujua kwanini ukumbi wa bunge kwa ndani umepanbwa kwa rangi nyekundu
 
wakuu

Bunge ni chombo kikubwa sana katika nchi hii pia kinaitambulisha taifa kwa muonekano wake tu

nimekuwa nikijiuliza sipati jibu huku tu muhimili ulioenda chini katika serkali hii ukiongozwa na rais unabendera yenye rangi zinazoelekea sawa na zile za taifa

Muonekano wa bunge la Tanzania ukiingia ndani limetawaliwa na rangi nyekundu, viti na zuria lilotawala bunge linarangi nyekundu!

hii rangi imepoteza kabisa rangi za taifa bungeni, ingefana zaidi tungewekewa miongoni mwa rangi zetu pendwa ndio zitawale ambazo ni Nyeusi, njano, bluu na kijani

Nyekundu inawakilisha nini bungeni katika taifa hili lenye rangi zake?

ni nani aliyesanifu na kupendekeza rangi nyekundu isiyo na picha nzuri, mvuto na maana yoyote kwa taifa hili
Umegusa mulemule.!
Hilo swali nilishajiulizaga siku nyingi tangu nilipoangalia bunge kwa mara ya kwanza.
 
Nyekundu huwa ina maanisha authority au mamlaka mkuu na ukitaka kuelewa kwa undani zaid angalia hata kwa majaji huwa wanakalia na kuvalia mavazi ya rangi nyekundu vilevile Rais nae huwa huvaliaga tai nyekundu na kukaa ktk kit cha rangi nyekundu na hta katk vyombo vya usalama km jesh na polis ffu nao huvalia kofia za rangi nyekundu hvyo hvyo km ilivyo kwa bunge nilazima iwe hvyo kutokana na kuwa n mhimili wa dola na walioko kule wana power kubwa kwa taifa hili
 
Jibu rahisi

Kwamba hiyo rangi nyekundu haina chama kwa tanzania. na chama chochote hakitakiwi kutumia hiyo rangi nyekundu kama nembo yake ya chama.

Nashukuru kama utakuwa umenielewa.
 
Nyekundu huwa ina maanisha authority au mamlaka mkuu na ukitaka kuelewa kwa undani zaid angalia hata kwa majaji huwa wanakalia na kuvalia mavazi ya rangi nyekundu vilevile Rais nae huwa huvaliaga tai nyekundu na kukaa ktk kit cha rangi nyekundu na hta katk vyombo vya usalama km jesh na polis ffu nao huvalia kofia za rangi nyekundu hvyo hvyo km ilivyo kwa bunge nilazima iwe hvyo kutokana na kuwa n mhimili wa dola na walioko kule wana power kubwa kwa taifa hili
Pia zuria wanalo kanyaga hawa viongoz wa juu iwe wandan au wa nje iwe bungeni au wanapo pokelewa uwanja wa ndege na kukagua gwaride huwa linatandikwa dhuria Jekundu maik utakuta ninyekundu pia.so tusi zarau mawazo ya mleta uzi watalam wa mambo mkuje huku mtupatie ufafanuzi juu ya hili.
 
Asante kwa kuliona hili mkuu.Mimi nilichaona utata huu na nikamuomba Mshana atupe maana ya rangi hasa nyekundu,nyeusi na nyeupe,lakini naona yuko kimya.Ni vema hata hivyo watu wakajua kwamba si kila mtu anatumia rangi au nembo yeyote bila kuwa na maana yeyote.Ni wale mbumbu tu wa mambo ndio wanao fanya hivyo.

Mshana uko wapi,tusaidie tafadhali.
 
nadhani hapo ulipotoa wazo la kuwa wangepamba kwa rangi ya bendera ya nchi yetu,upo sahihi sana.hayo mengine au maana ya rangi nyekundu wengine hatujui na wala kufahamu kwanin wameamua hvyo?
 
Rangi nyekundu ni rangi sawa kabisa kwa eneo Tukufu kama Bunge

Mleta mada siyo mtu mbaya, ila ni mmoja wa wale wasiokuwa na taste sahihi ya rangi. Ndiyo hawa huwa wanajenga ghorofa la maana sana halafu wanalipaka rangi ya kijani. Ni hawa hawa wanataka kila kitu Tanzania kipakwe rangi za bendera. Waelewe kuwa kila kitu na mahala pake, kila rangi na mahala pake.
 
Back
Top Bottom