Bunge: Mtikila ruksa kwenda mahakamani

Bunge: Mtikila ruksa kwenda mahakamani

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
BAADA ya mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupitia kundi la vyama vya siasa, Mchungaji Christopher Mtikila, kutishia kufungua kesi katika mahakama ya kimataifa kuzuia vikao vya Bunge hilo, ameambiwa ni ruksa kufanya hivyo.

Mchungaji Mtikila ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP) alieleza kusudio hilo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, akidai Bunge hilo ni batili kutokana na wajumbe wake kuteuliwa na mtu mmoja ambaye ni Rais Jakaya Kikwete.

Akielezea tishio la mjumbe huyo, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alisema ni haki yake kufanya hivyo na kwamba mahakama ndiyo itakayotoa uamuzi.

Source:
Tanzania Daima
 
...ni kawaida yake! Na HOJA yake MOJA ya kukibilia Mahakani ili aendelee kuwepo kwenye ramani ya DURU ZA SIASA
 
Mtikila anasumbuliwa na kitu fulani siku nitawaambia hapa hapa jf.
 
BAADA ya mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupitia kundi la vyama vya siasa, Mchungaji Christopher Mtikila, kutishia kufungua kesi katika mahakama ya kimataifa kuzuia vikao vya Bunge hilo, ameambiwa ni ruksa kufanya hivyo.

Mchungaji Mtikila ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP) alieleza kusudio hilo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, akidai Bunge hilo ni batili kutokana na wajumbe wake kuteuliwa na mtu mmoja ambaye ni Rais Jakaya Kikwete.

Akielezea tishio la mjumbe huyo, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alisema ni haki yake kufanya hivyo na kwamba mahakama ndiyo itakayotoa uamuzi.
Huyu pastor akishasahau tuu kumeza dawa basi kila neno linalokuja mdomoni yeye anawaza lazima lifike mahakamani.Sio ajabu akawapeleka wazazi wake kama wapo mahakamani kanini wamemzaa mwafrika.:biggrin1::biggrin1:
 
Mzee anajua kuchalenji japo mda mwingine anapayuka but some times anasaidia sana
 
Nina wasiwasi na mfumo wa Ubongo wa huyu anayejiita Mchungaji...

Kama bunge batili inamaana, wajumbe ni batili; pamoja na yeye na posho zote ni batili.

Amefata nini dodoma??
 
He is right how can we discuss marriage prosperity in absence of one member
 
Huyu hakupaswa kuwa mwanasiasa bali kiongozi wa NGO ya kisiasa. Ana hoja ya haja maana muungano unakuwepo vipi wakati mmoja anejitangazia uhuru?
Kwa nini uweze kutamka Zanzibar na usiweze kutamka Tanganyika?
Serikali ya Tanzania iwepo na serikali ya Tanganyika iwepo pia!!
 
nafikiri hoja yake ni ya msingi tatizo uelewa wetu,kwenda kwake mahakamani kumesaidia mambo mengi sana,tumvumilie naamini atafafanua na tutamwelewa tu
 
Huyo ndio Muasisi wa Tanganyika mpya.
Asimamie kura ya siri na serikali tatu.
Hilo la wajumbe kachelewa
 
Huyu mtukila na Pimbi wa sani mwenye hatakati kibaooo lakini haikamatiki hata moja
 
Back
Top Bottom