Bunge Maalum linajadili Rasimu ipi?

Bunge Maalum linajadili Rasimu ipi?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Nimefuatilia,nimesikia na kujua kinachoendelea Bunge Maalum la Katiba. Pamoja na kujua kwangu,bado nina swali kwa watanzania wenzangu: Bunge hilo linajadili Rasimu ipi? Iko wazi kuwa Rasimu ya Tume ya Katiba iliyokuwa chini ya Jaji Joseph Sinde Warioba inabeba mapendekezo ya Serikali tatu.

Kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zinazoliongoza Bunge hilo, Bunge Maalum linapaswa kujadili na kuipitisha Rasimu ya Tume ya Warioba. Hakuna la zaidi. Ilidhaniwa kuwa Wajumbe wangejadili serikali tatu tu na kuona uimara na udhaifu wa mapendekezo hayo. Halafu,kura zingepigwa.Kama mapendekezo yangepita;yangebaki kama yalivyo.Yangekataliwa,pangefunguliwa milango ya mapendekezo mengineyo katika kuirekebisha na kuiboresha Rasimu husika.Na kura ingefuatia.

Lakini,mambo yamekuwa kinyume.Tangu mwanzo,Rasimu inajadiliwa kana kwamba kuwa mapendekezo-chaguo ya serikali tatu au serikali mbili. Kuchanganya hoja za serikali tatu na mbili pamoja hakuwezi kutupa Katiba. Kufanya hivi kutakwamisha namna ya kupiga kura za kupitisha mapendekezo. Wajumbe wataulizwaje?

Ifike mahali,Bunge Maalum litumie Sheria zake na hekima katika jambo hili. Kama limeshindwa,liseme na kila mmoja arudi kwao. Mchafukoge uliopo juu ya Bunge Maalum kwasasa si mzuri na ni wa hatari. Wananchi wanaweza kuandika Katiba yao nje ya utaratibu na kuifuata.Yaweza kuwa hata mioyoni mwao tu.Ikitokea hivyo,Katiba inayoandikwa Bungeni haitafuatwa na kuheshimiwa.Nchi itakuwa kwenye hali gani?

cc Mchambuzi Yericko Nyerere Ngekewa FaizaFoxy Mamndenyi Chris Lukosi zumbemkuu Dingswayo Ben Saanane na wengineo karibuni tujadili
 
Lukuvi amesema Serikali Tatu ni Sera Ya Uamsho na CUF.

Mzee Warioba siku hizi ni Uamsho. Hapo sasa!
 
Hapo ndo umemaliza kuchangia au utarudi tena? Usituangushe mtalaam wetu tunahitaji msaada wako katika kulikomboa taifa hili.
 
Nipo, natoa dozi ndogo ndogo kuna nyuzi nyingi zinaongelea swala hili la Lukuvi naona wengi wamesahahu kuwa si Lukuvi pekee kwani kakiri kuwa katumwa kwenda pale kanisani na Waziri Mkuu.

Aliwataka Watanzania kuipuuza Rasimu ya Katiba katika suala la Muungano na Serikali tatu kwa madai kuwa kutaka kuwapo mfumo huo ni kutaka Watanzania waingie vitani.

Lukuvi: Tukipitisha serikali tatu jeshi litatawala nchi - Katiba - mwananchi.co.tz
 
Ingekua Kenya,wanaharakati wataalam wa sheria wangekua tayari wamekimbilia mahakamani..wapi mama Bisimba,Sungusia,Mtikila,Kibamba, et al?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Nimefuatilia,nimesikia na kujua kinachoendelea Bunge Maalum la Katiba. Pamoja na kujua kwangu,bado nina swali kwa watanzania wenzangu: Bunge hilo linajadili Rasimu ipi? Iko wazi kuwa Rasimu ya Tume ya Katiba iliyokuwa chini ya Jaji Joseph Sinde Warioba inabeba mapendekezo ya Serikali tatu.

Kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zinazoliongoza Bunge hilo, Bunge Maalum linapaswa kujadili na kuipitisha Rasimu ya Tume ya Warioba. Hakuna la zaidi. Ilidhaniwa kuwa Wajumbe wangejadili serikali tatu tu na kuona uimara na udhaifu wa mapendekezo hayo. Halafu,kura zingepigwa.Kama mapendekezo yangepita;yangebaki kama yalivyo.Yangekataliwa,pangefunguliwa milango ya mapendekezo mengineyo katika kuirekebisha na kuiboresha Rasimu husika.Na kura ingefuatia.

Lakini,mambo yamekuwa kinyume.Tangu mwanzo,Rasimu inajadiliwa kana kwamba kuwa mapendekezo-chaguo ya serikali tatu au serikali mbili. Kuchanganya hoja za serikali tatu na mbili pamoja hakuwezi kutupa Katiba. Kufanya hivi kutakwamisha namna ya kupiga kura za kupitisha mapendekezo. Wajumbe wataulizwaje?

Ifike mahali,Bunge Maalum litumie Sheria zake na hekima katika jambo hili. Kama limeshindwa,liseme na kila mmoja arudi kwao. Mchafukoge uliopo juu ya Bunge Maalum kwasasa si mzuri na ni wa hatari. Wananchi wanaweza kuandika Katiba yao nje ya utaratibu na kuifuata.Yaweza kuwa hata mioyoni mwao tu.Ikitokea hivyo,Katiba inayoandikwa Bungeni haitafuatwa na kuheshimiwa.Nchi itakuwa kwenye hali gani?

cc Mchambuzi Yericko Nyerere Ngekewa FaizaFoxy Mamndenyi Chris Lukosi zumbemkuu Dingswayo Ben Saanane na wengineo karibuni tujadili

Ninachojuwa mimi ni kuwa iwapo Katiba utatafutwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa, hakuna katiba mpya na kama huu ulikuwa ni uwekezaji basi tuseme tumefilisika.

Bunge limekubali kuingizwa kwenye ugomvi wa Wazanzibari na hata Watanganyika nao kushiriki matusi baina ya pande mbili za Wazanzibari, hapa hakuna makubaliano.

Sijui kwa makusudi au kwa bahati mbaya CCM wanaamuwa kuwatukana Wazanzibari ili kujibu ukweli wanaoambiwa lakini wanasahau kuwa unapowatukana Wazanzibari basi unawajengea wapinzani faida! Unapotukana Wapemba huku wamekupa kura ambazo zimesaidia Rais unakuwa unajiumiza mwenyewe!
 
Nipo, natoa dozi ndogo ndogo kuna nyuzi nyingi zinaongelea swala hili la Lukuvi naona wengi wamesahahu kuwa si Lukuvi pekee kwani kakiri kuwa katumwa kwenda pale kanisani na Waziri Mkuu.

Aliwataka Watanzania kuipuuza Rasimu ya Katiba katika suala la Muungano na Serikali tatu kwa madai kuwa kutaka kuwapo mfumo huo ni kutaka Watanzania waingie vitani.

Lukuvi: Tukipitisha serikali tatu jeshi litatawala nchi - Katiba - mwananchi.co.tz

Kwa akili yake kutokana na kuihusisha CUF na UAMSHO anafanya counter attack kwa yeye kuiunganisha CCM na makanisa.
 
Hivi hakuna taasisi au kundi lolote lonaloweza kwenda mahakamani kupinga hili Bunge kuendelea na upuuzi wao.
 
Rasimu inapowasilishwa bungeni kujadiliwa maanake ni kuwa inaweza kutopita ama kufanyiwa marekebisho fulani ama kubadilishwa kifungu kwa kifungu.
Ndo maana ya kuileta bungeni.
Watu wako within the law hapa.
 
Mimi naona wenye uzalendo wa nchi yetu na uchungu ni wale waliobaki bungeni. Hawa UKAWA SI LOLOTE NA WALA SI CHOCHOTE. KWAO WANANCHI KUUWAWA ILI WAPATE MADARAKA NDIYO JAMBO LA MAANA. NIJUAVYO MIE HOJA HUJIBIWA KWA HOJA NA ASKARI ANAEKIMBIA VITA SI MZALENDO WA KWELI BALI NI MBABAISHAJI TU. KINA UKAWA NANI ASIYEWAJUA KUWA NI WABINAFSI NA WANA PEPO KUU LA MADARAKA. KILICHOWAONDOSHA BUNGENI NI KUONA KWAMBA SERIKALI TATU HAZITAPITA NGO, SISI WATANZANIA HATUKO RADHI NAO. SERIKALI MBILI MPANGO MZIMAAAAAAAAAAAAAA. MUUNGANO UDUMU MILELE
 
Back
Top Bottom