Bunge Live! J KIKWETE Tutakukumbuka

Bunge Live! J KIKWETE Tutakukumbuka

Jana kwa mara ya kwanza waandishi wa habari walizuiwa kurekodi shughuli za vikao vya Bunge. Hawakuwa na sababu ya kuwepo bungeni. Nikiwaza kwa sauti na kiujinga ujinga tu nashindwa kuelewa.

1. Pamoja na uozo na ubovu na umizigo wa watendaji wa serikali ya JM Kikwete lakini hatukuona hata mara moja rais mcheshi JK akiwaficha watendaji wake nyuma ya pazia.

Serikali ya JPM na wateule wake wamejinabaisha mbele ya ulimwengu kwamba wako makini na wenye kuichukia rushwa na ufisadi. Tangu mapambano ya dhidi ya ufisadi yaanze hapa nchini, huchokonolewa kwanza bungeni. Sasa, hawa wa utawala huu wanachokificha au wanachotaka kukificha ni nini? Kwa nini wanataka mambo yao yatendeke nyuma ya pazia?

2. Imejulishwa kuwa serikali ya JK haikuwa na makusanyo makubwa ya mapato kama hii ya JPM. Pamoja na umasikini wa serikali ya JK haikuinyima fedha TBC. Alitaka muhimili mwingine wa utawala uonwe na uonekane.

Sasa vipi, serikali ya JPM yenye kukusanya mara dufu mapato kuliko ile ya JK ishindwe kuipatia fedha TBC ioneshe moja kwa moja shughuli za vikao vya muhimili huu- Bunge?

Haya, serikali haina fedha. Wapo wenye fedha, Azam TV, StarTV nk basi waruhusuni hao waoneshe! Hamtaki! Kumbe mnachotaka kuficha nini?

3. Imedaiwa kuwa mara kadha serikali imetumia mabavu na mbinu kadha kuudhibiti muhimili huu (Bunge). Pamoja na hayo, JK hakufika pahala akalizima bunge. Imekuwaje awamu hii mnataka kulizima bunge? Nini mnatafuta? Je! Mnataka serikali tu mwonekane, bunge je?

Kwa mwendo huu, wa kukosa kuliona bunge live hakika Kikwete tutakukumbuka. Serikali yako ilikuwa wazi. Ililiacha bunge liiumbue serikali yako iliyojaa mawaziri mizigo.
Ati serikali hii haina mawaziri mizigo ILA haitaki kuumbuliwa hadharani!

HEKO zako Kikwete kukubali kukosolewa na kuikosoa serikali yako hadharani. Hakika katika hili la Uhuru wa Vyombo vya Habari ulijitahidi kuwa muungwana; japo mwishoni ulijikwaa kuja na sharia ya mitandaoni.

UTAKUMBUKWA JK!
Hata Msigwa ETI anamkumbuka Kikwete!!!!
Acheni unafiki, juzi tu mlisem akili ndogo haiongzi akili kubwa (yenu)!
Leo mnamsifia JK, kweli akili ni mali!!!
 
Nilitegemea JPM aliposema nisaidieni kupasua majipu angeliacha Bunge kwa asilimia 100,huru,ili Wabunge wamsaidie,kumbe ni kinyume chake,nina wasi wasi kama kuna uhalali wowote kwenye hoja ya kutumbua majipu,kuna watu wachache maalum wa kutumbuliwa,naona kama ukanda fulani hivi ndiyo wameongoza kwa kutumbuliwa majipu,wengine majipu yao hayaguswi.

Tumeliona la Kabwe la bilioni 3 limetumbuliwa haraka sana lili la bilioni 37 +40 mwenye nalo kesha sepa,na liko njia panda ya kwenda theatre au kuachiwa barabarani tu
 
S

Muda hautoshi kufafanua lakini upo totally wrong. Kuzuia uhuru hakuleti stability, kinyume chake ndiyo sahihi. Hizo nchi ulizozitaja Misri na Libya zimeparanganyika kutokana na udikteta wa hao viongozi wa mwanzo, siyo kutokana na uwepo wa demokrasia. Hata Rwanda, leo hii ikitokea ghafla Kagame hayupo, kama hakuna taasisi za kiuongozi na za demokrasia zilizoundwa, nchi inaparanganyika.

Madikteta huwa hawapendi kutengeneza taasisi wanataka kazi za kitaasisi wazitende wenyewe ili kulinda sifa binafsi na mamlaka. Kwa hiyo mambo mengi yanafanywa na mtu binafsi. Yeye huwa ndiye mtawala, sera na katiba.
mkuu ni sehemu gani ambayo Africa demokrasia na uhuru wa habari imeleta faida? sana huleta machafuko na confusion,na gharama kubwa, u dikteta una hasara zake lakini naona nchi ndio zinakuwa stable zaidi..nchi zinazofuata hiyo demokrasia baada ya miaka 5 uchaguzi ukikaribia huwa ni woga kwa sababu ya wananchi wake wanakuwa charged na wale wanasiasa
 
Tawala za kidikteta huwa zina sifa kuu kubwa 3:
1) Kudunisha nguvu ya mihili mingine ya kiutawala na kuhodhi madaraka na maamuzi
2) Kupenda kusifiwa na kuzuia ukosoaji
3) Kuzuia uhuru wa habari. Watawala wataamua usikie nini, nini usisikie, usikie wakati gani, usikie kwa namna gani, nani wasikie, nani hawatakiwi kusikika.
Hayo mawili ya mwanzo hayawezi kupata mafanikio ukiruhusu uhuru wa upashanaji habari.

Makonda alifanya mkutano wake na viongozi live, hata wananchi waishio Namtumbo wanaoangalia TBC walilazimishwa kumsikia Makonda wa Dar, japo anayoyaongea hayawahusu. Jana wananchi wote walishuhudia live ufunguzi wa daraja na kufukuzwa kazi kwa Kabwe, wengi wa waliokuwa wakiangalia hawajui hata Kinondoni ni wapi, wala Kabwe ni nani. Wakati huo huo hawaruhusiwi kumwona mbunge wao wanayemfahamu, live.

Sasa tunaamuliwa nini tusikie, toka kwa nani, na kwa namna ipi. Hakuna jambo baya duniani kama mtu mwingine kukufanya mtumwa wake wa fikra.
 
Hio Bunge tv aliyozungumza Nape jana na waandishi wa habari sijui itatengemaa lini. But still, awamu ya tano inawapa matumaini zaidi watanzania kuliko awamu iliyopita.
utawapa matumaini makubwa sana maana mtakuwa hamna taarifa kinzani.
hiyo tv mpaka ije itengemae serikali ya awamu ya 5 itakuwa inafikia ukingoni. endelea kusubiri.
Mh. Magufuli keep it up as much as you can.
 
Jana kwa mara ya kwanza waandishi wa habari walizuiwa kurekodi shughuli za vikao vya Bunge. Hawakuwa na sababu ya kuwepo bungeni. Nikiwaza kwa sauti na kiujinga ujinga tu nashindwa kuelewa.

1. Pamoja na uozo na ubovu na umizigo wa watendaji wa serikali ya JM Kikwete lakini hatukuona hata mara moja rais mcheshi JK akiwaficha watendaji wake nyuma ya pazia.

Serikali ya JPM na wateule wake wamejinabaisha mbele ya ulimwengu kwamba wako makini na wenye kuichukia rushwa na ufisadi. Tangu mapambano ya dhidi ya ufisadi yaanze hapa nchini, huchokonolewa kwanza bungeni. Sasa, hawa wa utawala huu wanachokificha au wanachotaka kukificha ni nini? Kwa nini wanataka mambo yao yatendeke nyuma ya pazia?

2. Imejulishwa kuwa serikali ya JK haikuwa na makusanyo makubwa ya mapato kama hii ya JPM. Pamoja na umasikini wa serikali ya JK haikuinyima fedha TBC. Alitaka muhimili mwingine wa utawala uonwe na uonekane.

Sasa vipi, serikali ya JPM yenye kukusanya mara dufu mapato kuliko ile ya JK ishindwe kuipatia fedha TBC ioneshe moja kwa moja shughuli za vikao vya muhimili huu- Bunge?

Haya, serikali haina fedha. Wapo wenye fedha, Azam TV, StarTV nk basi waruhusuni hao waoneshe! Hamtaki! Kumbe mnachotaka kuficha nini?

3. Imedaiwa kuwa mara kadha serikali imetumia mabavu na mbinu kadha kuudhibiti muhimili huu (Bunge). Pamoja na hayo, JK hakufika pahala akalizima bunge. Imekuwaje awamu hii mnataka kulizima bunge? Nini mnatafuta? Je! Mnataka serikali tu mwonekane, bunge je?

Kwa mwendo huu, wa kukosa kuliona bunge live hakika Kikwete tutakukumbuka. Serikali yako ilikuwa wazi. Ililiacha bunge liiumbue serikali yako iliyojaa mawaziri mizigo.
Ati serikali hii haina mawaziri mizigo ILA haitaki kuumbuliwa hadharani!

HEKO zako Kikwete kukubali kukosolewa na kuikosoa serikali yako hadharani. Hakika katika hili la Uhuru wa Vyombo vya Habari ulijitahidi kuwa muungwana; japo mwishoni ulijikwaa kuja na sharia ya mitandaoni.

UTAKUMBUKWA JK!
Binafsi hata simlaumu Magufuli. swali ni je ana moyo mgumu kama wa Kikwete? Kikwete alitukanwa kila kona lakini akasema acheni wanitukane maana mie ndo kiongozi wao wa juu kabisa.
Kuwanyima wananchi habari ni njia sahihi ya kuwaongoza bila bugdha na usumbufu usiowalazima au wa lazima. na kwa usalama wake Magufuli namshauri asirushe live hayo ya bungeni kama alivyofanya mtangulizi wake. maana humo kuna kila aina ya matusi mara ataitwa dhaifu, dikteta, mkabila, mdini, mkanda na mengine mengi.
Hilo la mitandao haikuwa na jinsi maana JK alikuwa anaondoka ila alikuwa anamhurumia ajaye. maana huenda asiwe na kifua kizito kama chake.
 
Kwa suala la uhuru wa habari, asante sana baba JK, mwangi wa shutuma, vijembe, lawama, ukosoaji wa serikali yako haukukuzuia kuturuhusu sisi wananchi kuwafuatilia watendaji wetu bungeni LIVE
Mkuu wa Kaya wa sasa yeye mara nyingi anaobeshwa LIVE lakini sisi wananchi mambo yetu yanakuwa Edited, recorded au yapotezewe tu.
Nakuomba wewe kama Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mumueleze mzee kuwa ameturudisha miaka kibao nyuma, na ikibidi mumkumbushe kuwa kwa kufanya vile anatunyima wananchi uhuru mpana.
Naomba mumuambie kuwa maendeleo siyo vitu tu, bali uhuru, uwazi, ushiriki wa jamii katika mambo ya nchi yao kwa wakati.
Namiss mjadala wa richmond, Operation tokomeza, escrow, Buzwagi. Laiti ingekuwa mwingine amekalia kiti najua angepiga marufuku bunge kurushwa Live, lakini ndugu Mwenyekiti uliweka sifa zako na serikali yako binafsi pembeni, ukaturuhusu Tujionee na sisi wenyewe. nasema hivyo ndivyo serikali yenye kujiamini inapaswa iwe, Serikali Oga hupenda watu wawe brainwashed!

ASANTE SANA JAKAYA!
 
Nadhani ni jambo jema tu kupata yaliyozungumzwa in summary kuliko kuangalia kitu kizima, kwa jamii zetu ambazo bado hatujakua na uwezo wa kumanage matumizi hata ya simu zetu sio vibaya serikali ikitusaidia katika hili, ili tuweke akili zetu katika kuzalisha na tuache wale tuliowachagua wafanye kazi ya kutuwakilishs vyema huko bungeni. Kungangania kutazama bunge live inamaana sisi wananchi hatuna hata imani na wale tuliowachagua kama wanafanya vyema kazi zao, sasa na tuwekeze katika kuchagua wawakilishi sahihi.
Kwa mawazo kama haya ni dhahiri yule mgombea Urais wa Marekani alikuwa sahihi sana kuhusu sisi waafrika.
 
nimeshakutana na watanzania wengi tu kama wewe wenye ujuaji kupitiliza , hivyo sioni ajabu sana wewe unapojifanya mjuaji ilhali hamna lolote unalojua zaidi sana ya kukariri tu maisha kwa kutazama tv, tv waachie watoto wa kike watazame
 
Jenga hoja acha viroja. The late Mwl Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema ukiona mtu mwenye akili timamu anakimbilia kauli za matusi au kashfa basi ujue mtu huyo kaishiwa hoja..
 
Hoja yangu ni kwamba, hua nashangazwa sana na mtoto wa kiume kulilia tv, sasa sijui kina mama, watoto na wadada wa nyumbani watakua wanafanya nini, sijui nyie wenzangu hua mnapata wapi huo muda wa kukaa na kuangalia tv siku nzima hua hainiingii akilini, such a wastage of energy and time, huo muda unatakiwa uwe mtu unafanya kazi za kuzalisha...hiyo tv yenyewe hata sina, kwahiyo sioni hata tabu kulikosa bunge live...kwakua nikitaka kujua ninikilijadiliwa siwezi kosa namna ya kujua, kwakua yote yatasikika tu...kwa namna moja ama nyingine...
 
Nadhani ni jambo jema tu kupata yaliyozungumzwa in summary kuliko kuangalia kitu kizima, kwa jamii zetu ambazo bado hatujakua na uwezo wa kumanage matumizi hata ya simu zetu sio vibaya serikali ikitusaidia katika hili, ili tuweke akili zetu katika kuzalisha na tuache wale tuliowachagua wafanye kazi ya kutuwakilishs vyema huko bungeni. Kungangania kutazama bunge live inamaana sisi wananchi hatuna hata imani na wale tuliowachagua kama wanafanya vyema kazi zao, sasa na tuwekeze katika kuchagua wawakilishi sahihi.

Historia ndio humhukumu mtu kwa mazuri au mabaya ,Bungeni pamoja na kuona live wakati uliopita tuliona namna ambavyo Bunge liliendeshwa bila ya usawa ndani ya Bunge kati ya wapinzani na watawala..

Yapo mambo mengi yaliibuliwa Bungeni kama sakata la ESCROW na tuliwajua wachawi wetu ktk Uchumi wa taifa hili,maisha ya kuchaguliwa kipi uangalie na kipi usikitizame yana tofauti gani na zama zileee za Udikteta na ndugu yake Ukoloni!?Zama zimebadilika mkuu usiishi kizamani ,huku kuminya Uhuru wa habari kuna athari zake na mbaya zaidi Serikali haijatoa sababu za MSINGI za kuvunja haki ya Kikatiba.

Sijajua unatetea kwa akili gani.
 
Kwa suala la uhuru wa habari, asante sana baba JK, mwangi wa shutuma, vijembe, lawama, ukosoaji wa serikali yako haukukuzuia kuturuhusu sisi wananchi kuwafuatilia watendaji wetu bungeni LIVE
Mkuu wa Kaya wa sasa yeye mara nyingi anaobeshwa LIVE lakini sisi wananchi mambo yetu yanakuwa Edited, recorded au yapotezewe tu.
Nakuomba wewe kama Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mumueleze mzee kuwa ameturudisha miaka kibao nyuma, na ikibidi mumkumbushe kuwa kwa kufanya vile anatunyima wananchi uhuru mpana.
Naomba mumuambie kuwa maendeleo siyo vitu tu, bali uhuru, uwazi, ushiriki wa jamii katika mambo ya nchi yao kwa wakati.
Namiss mjadala wa richmond, Operation tokomeza, escrow, Buzwagi. Laiti ingekuwa mwingine amekalia kiti najua angepiga marufuku bunge kurushwa Live, lakini ndugu Mwenyekiti uliweka sifa zako na serikali yako binafsi pembeni, ukaturuhusu Tujionee na sisi wenyewe. nasema hivyo ndivyo serikali yenye kujiamini inapaswa iwe, Serikali Oga hupenda watu wawe brainwashed!

ASANTE SANA JAKAYA!

Huoni kuwa mlipewa huru ili msikumbuke ya kina Kabwe, Kitilya Lugumi na mengine mengi yanakuja, leo ndiyo mnagundua kama kuna ESCROW ya GESI Wadanganyika bana. People just think broader.Watanzania hawana uelekeo kama upepo.poleni
 
Hoja yangu ni kwamba, hua nashangazwa sana na mtoto wa kiume kulilia tv, sasa sijui kina mama, watoto na wadada wa nyumbani watakua wanafanya nini, sijui nyie wenzangu hua mnapata wapi huo muda wa kukaa na kuangalia tv siku nzima hua hainiingii akilini, such a wastage of energy and time, huo muda unatakiwa uwe mtu unafanya kazi za kuzalisha...hiyo tv yenyewe hata sina, kwahiyo sioni hata tabu kulikosa bunge live...kwakua nikitaka kujua ninikilijadiliwa siwezi kosa namna ya kujua, kwakua yote yatasikika tu...kwa namna moja ama nyingine...
Once again your argument is irrelevant and immaterial. The fact that you don't own a TV set does not justify stopping of live bunge coverage. If you don't have time to follow what your MPs are discussing that is your problem and don't make it other people 's problem as well.
 
Mimi ni mwanzo na mwisho sipigi tena kura siwezi kumchagua mtu alafu nisijue uwajibikaji wake hakuna haja tena
 
Once again your argument is irrelevant and immaterial. The fact that you don't own a TV set does not justify stopping of live bunge coverage. If you don't have time to follow what your MPs are discussing that is your problem and don't make it other people 's problem as well.
mwanaume huwezi lilia kuangalia tv namna hii. utakua na tatizo mahali.
 
Ila huyu amefunga bunge kuonyeshwa live Ila mapato juu....jpm yupo juu ndugu tumuungeni mkono
 
utawapa matumaini makubwa sana maana mtakuwa hamna taarifa kinzani.
hiyo tv mpaka ije itengemae serikali ya awamu ya 5 itakuwa inafikia ukingoni. endelea kusubiri.
Mh. Magufuli keep it up as much as you can.
I take back my Words Mkuu!! . Khaa!!
 
Back
Top Bottom